Akaunti rasmi ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam / Official Twitter Account for CCM Youth League Dar es Salaam Region.
TUMEBADILI!
Tunasikitika kutangaza mabadiliko ya akaunti yetu rasmi ya mtandao wa twitter kutokana na changamoto ya kimtandao iliyotukuta.
Sasa tunapatikana rasmi kupitia @uvccmdar tafadhali tufuate (follow) ili kuendelea kuwa pamoja nasi.
#NitachaguaMafanikio#Tumebadili
Tunatoa pole kwa wananchi wote walioathirika na mafuriko na waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki kutokana na mafuriko.
Tunaiomba Serikali, Asasi za kiraia na Wananchi kwa ujumla kuungana kwa pamoja katika kuwasaidia watanzania wenzetu katika kipindi hiki kigumu tunachokipitia.
Kuelekea miaka 43 ya CCM sisi vijana wa CCM Mkoa wa Dar es salaam tunajivunia kuona namna ilani ya Chama Chetu imejikita katika usawa wa kijinsia kwa kuwawezesha wanawake kupitia miradi mbalimbali kufikia 50/50.
#Kulindanakujengaujamaa#Miaka43yaCCM#2020mitanotena
Kuelekea Miaka 43 ya CCM sisi vijana wa Mkoa wa Dar es salaam tunajivunia kuona serikali ya CCM imevuka lengo katika kutoa elimu msingi bila malipo kwa kujenga madarasa 612 ya elimu ya awali katika shule za msingi sambamba na uandikishwaji wa watoto kwa 166% kwa elimu ya awali
Naungana na Watanzania wenzangu kuomboleza kifo cha Ndugu @amufuruki . Binafsi nimepokea taarifa za kifo chake kwa masikitiko makubwa. Nawapa pole familia na @tpsftz kwa msiba huu. Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya Ndugu Mufuruki mahala pema, peponi.
1961 usafiri wa reli ulisimamiwa na East Africa Railway & Harbours. Reli ilikuwa meter gauge yenye upana wa mita 1 na kasi 30km/h
Miaka 58 ya uhuru tuna TRC. Tunajenga SGR yenye upana wa mita 1.435, urefu wa km 1,800 na kasi 160 km/h. Itabeba tani milion 17 za mzigo kwa mwaka
1961 hatukuwa na chombo kilichosimamia akiba ya chakula ya Taifa. Ukame wa 1973 hadi 1975 ilitulazimu kuagiza chakula kutoka nje kibiashara na kutegemea misaada
Miaka 58 ya uhuru, nchi ina Chombo maalum (NFRA). Ina maghala 33 yenye uwezo wa kuhifadhi tani 251,000 za chakula
Kabla ya Uhuru, huduma za afya nchini zilikuwa zinatolewa zaidi kwenye maeneo ya shughuli za kiuchumi kama miji na mashamba makubwa
Miaka 58 ya uhuru, tuna hospitali zaidi ya 269, zahanati 6,640, na vituo vya afya 8,119
Huduma za afya zimeendelea kuboreshwa kwa kasi sana.
Katibu Mkuu Dkt Bashiru Ally amekutana na ujumbe kutoka Chama cha Kijamaa cha Vietnam (CPV) ulioongozwa na Mr. Pham Minh Chinh. Mazungumzo yao yamelenga kuimarisha uhusiano wa kichama na Kitaifa.
Katibu wa HK ya Taifa, Itikadi na Uenezi Ndg. @hpolepole ameshiriki mazungumzo hayo.
@uvccmdar@hpolepole@Tz_Kwanza @KahundaRebeca @wizara_elimuTz@uvccm_tz Unisamehe lakini upande wa wingi wa vyuo, haitoshi kuangalia idadi ya vyuo tu. Inabidi kuzingatia economies of scale na vilevile uwepo wa rasilimali watu wa kutosheleza vyuo vyote hivyo
1961 mtandao wa barabara ulikuwa na km 33,600
Miaka 58 ya uhuru, mtandao wa barabara una km 87,581. Km 35,000 ni barabara kuu na km 52,581 ni barabara za wilaya
Mtandao wa barabara unasimamiwa na Tanroads kwa barabara kuu za kitaifa na Tarura kwa barabara za mijini na vijijini
Tulipopata uhuru tulikuwa na chuo kikuu kimoja tu. Kilikuwa na kitivo kimoja tu (kitivo cha sheria). Chuo kilidahili wanafunzi 14 tu kutoka Tanganyika (7), Kenya (4)na Uganda (3)
Miaka 58 ya uhuru, tuna vyuo vikuu 49 vyenye fani mbalimbal vinavyodahili wanafunzi 63,000 kwa mwaka
ATC lilianzishwa 11 March 1977 likiwa na ndege moja tu aina ya Douglas DC-9-32
Miaka 58 ya uhuru, ATCL inamiliki ndege 9 aina tofauti (Airbuss 220-300, Fokker 50, De Havilland Canada Dash 8-300, De Havilland Canada Dash 8-400 na Boeng 787 Dreamliner.)
Nyengine ziko njiani!
Wakati tunapata uhuru tulikuwa na uwanja wa ndege wa JK Nyerere terminal 1 wenye uwezo wa kuhudumia abiria 500,000 kwa mwaka leo tuna terminal 3 yenye uwezo wa kuhudumia abiria 6,000,000 kwa mwaka.
#NitachaguaMafanikio#T2020JPM@ccm_tanzania@uvccm_tz@hpolepole