Kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Miaka 30 ya Bongo Flava imetangaza kuwa Dodoma ndicho kituo kinachofuata cha Maadhimisho hayo, baada ya kufanyika kwa mafanikio Jijini Mwanza.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa Niaba ya Kamati na Hamadi Ally Seneda, tamasha linalofuata litafanyika Agosti 22, 2026 katika Chinangali Park, Dodoma.
Kamati imetoa shukrani kwa Washiriki na Wadau mbalimbali waliofanikisha Maadhimisho ya Mwanza, ikieleza kuwa lengo la sherehe hizo si kutoa burudani pekee, bali pia kuwawezesha Wasanii na Wanajamii kiuchumi pamoja na kuimarisha uchumi wa ubunifu Nchini.
Aidha, Kamati imesema Maadhimisho hayo yanalenga kuendelea kuuenzi na kuutangaza urithi wa muziki wa Bongo Flava, huku safari hiyo ikiendelea katika Mikoa mbalimbali Nchini.
#MillardAyoUPDATES
Jana nilitangaza kwamba nina FREE Training ambayo itakuonyesha fursa zinazopatikana ukijifunza jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii vizuri.
Mpaka leo kuna watu 1000+ wamejisajili!
Wow! Menipa hamasa kufanya hili jambo kwa Nguvu.
Usajili Hapa: https://t.co/ko0stFQBU1