SIMU NI ZIMWI LIKUJUALO
Kuna wakati ukisikiliza maneno ya wahenga unaweza kucheka ukijiuliza waliwaza nini. Wahenga waliwahi kusema Kikulacho ki nguoni mwako. Sijui wahenga walikutana na mikasa gani hadi wakasema hivyo.
Kila anayeusikia msemo huu anawawaza ndugu wa karibu na jamaa zake. Kilichopo nguoni mwako kinajua siri zako, kinajua nguvu yako na kinajua udhaifu wako, kinajua furaha yako na huzuni yako, kinajua malengo yako na mikakati yako. Hakuna anayetamani kukutwa na mkasa wa kuliwa na kilichoko nguoni mwake.
Kwa zama za leo basi kama kuna kitu kimemganda kila mtu nguoni ni Simu yake ya mkononi, Simu za mkononi zimebadili mifuno ya maisha. Simu zimekua kama ndugu wa mtu, zinajua siri, zinajua furaha na huzuni, zinajua matamanio na majuto.
Wahenga walishasema pia Zimwi likujualo halikuli likakwisha. Inawezekana walikua sahihi japo kuna mtu siku moja aliwahi kuuliza swali, kama Zimwi likujualo likaamua kuanza kula kichwa chako hata lisipokumaliza utaendelea kuishi kweli? Hapa wahenga sijui waliwaza nini…..
Katika kipindi ambacho teknolojia imekua kwa kasi, simu za mkononi zimetawala maisha ya mwanadamu wa karne ya 21 kwa kiwango kikubwa sana. Simu zimekua Kompyuta, Zimekua Saa, zimekua hifadhi ya kumbukumbu, Zimekua Vibubu, Zimekua kumbi za mikutano, zimekuwa mihadhara, zimekua karibu kila kitu.
Kutokana na kuwa karibu sana na maisha ya kila siku zimehifadhi mambo mengi sana ya siri ambayo pengine mtu asingeweza kuruhusu kwa namna yoyote mtu mwingine kuyafahamu. Mengine yamewahi kuwa ya aibu kiasi cha mmiliki mwenye kushindwa kuyavumilia na kuamua kuyafutilia mbali ili yasije kuonekana.
Edward Snowden alipata umaarufu sana mwaka 2013 baada ya kuibua suala la usiri na usalama wa taarifa za watumiaji wa simu za mkononi, wengi walipigwa na butwaa.
Ni hadithi ndefu sana, ila kilichonishangaza zaidi ni moja ya nukuu zake alizowahi kusema kwa kingereza "The truth, though, is that deletion has never existed technologically in the way that we conceive of it. Deletion is just a ruse, a figment, a public fiction, a not-quite-noble lie that computing tells you to reassure you and give you comfort“ nikinukuu kwa kiswahili
"Ukweli ni kwamba, kufutwa kamwe hakujawahi kuwepo kiteknolojia kama tunavyofikiria. Kufutwa ni hila tu, ni uongo, ni , ni udanganyifu kwa umma, ni uongo usiokuwa kamili ambao kompyuta inakuambia ili kukuhakikishia na kukupa faraja." Najua umeshtuka ila ndio ukweli.
Sasa ni muhimu kujiuliza maswali kadhaa, je umewahi kuipa simu yako siri zako kiwango gani? Je, Ulifuta? Je una uhakika Zilifutika? Utajisikiaje siku ukikutana nazo? Kama bado umepigwa na butwaa kumbuka wahenga walishasema maji yakimwagika hayazoleki, suala la msingi ni kuhakikisha huyamwagi tena ili usianze kuhangaika kuyazoa. Huwezi kuepuka kutumia simu na kuhifadhi taarifa zako muhimu, ila unaweza kuepuka kuipa simu yako mambo yanayoweza kukupa aibu siku moja.
Wako Msakatonge
El~Campeón
🚨 OFFICIAL: Lionel Messi, TOP SCORER EVER in World Cup history joint with Miro Klose. 🎞️⭐️
16 goals at the World Cup. 💥🇦🇷
In one night, on 6th World Cup debut game at 38, Messi surpasses Mbappé (14), Müller (14) and Ronaldo Nazario (15).
The problem that has always come with being a high achiever especially in academics is everyone has high expectations from you,wheather you like it or not. And there are others waiting for you to fail so that they can feel satisfied because their parents compared them to you so now they want to prove their parents wrong. The ones who have less on their plates is us,the bare minimum achievers. Mimi kwanza nilipata D+ namna hii ata mama yangu alisema nimejaribu,it could have been worse. Sababu kwanzia form 2 hesabu sikuwai pata above 21% aki. As a bare minimum achiever I can fail and nobody will judge me,not even myself. This is the modest place you want to be in life.