Mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa mradi kwa vikundi vya uzalishaji chini ya mradi wa EBARR yanayoendelea muda huu leo juni 22, 2024 kwa wanufaika wa mradi wa Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara.
Mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa mradi kwa vikundi vya uzalishaji chini ya mradi wa EBARR yaliyofanyika juni 20, 2024 kwa wanufaika wa mradi wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ktk ukumbi wa VETA Kishapu.
Mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa mradi kwa vikundi vya uzalishaji chini ya mradi wa EBARR yaliyofanyika juni 18, 2024 kwa wanufaika wa mradi wa Wilaya ya Mpwapwa, Dodoma. Mafunzo yalifanyika katika shule ya Sekondari Ng'ambi.
Mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa mradi kwa vikundi vya uzalishaji chini ya mradi wa EBARR yakiendelea muda huu kwa wanufaika wa mradi wa Wilaya ya Mvomero, Morogoro.
Khadija Said Kanyundo ni mjasiriamali na mnufaika wa jiko banifu kutoka kijiji cha ikrujiti wilayani Simanjiro, Mkoa wa Manyara. Jiko hilo linatumia kuni chache ambapo lina saidia kuepusha uharibifu wa mazingira kwa kukata miti hovyo.
Pichani ni miti iliyopandwa na Mradi wa EBARR (Mradi wa Kuhimili mabadiliko ya Tabia Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia vijijini) katika Shule ya Msingi Orkesumet iliyopo wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Nanyori Samwel Mollel na Maria Christopher Malo toka kikundi cha Enyoito Kitongoji cha Mukumbi wilayani ya Simanjiro,mkoani Shinyanga ni moja ya wanaufaika wa mradi wa kuku chotara kutoka katika mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia vijijini(EBARR)
Sinyati Paul Kosindyo ni Mwenyekiti wa kikundi cha Namilok kutoka kijiji cha Irikujiti wilayani Simanjiro, Mkoa wa Manyara. Kikundi hicho kimenufaika na mradi wa ufugaji wa nyuki kutoka Mradi wa kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia vijiji(EBARR).
Pichani ni Familia inayojihusisha na Ufugaji wa kuku kutoka Kijiji cha Beledi, kata ya Lagana wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga iliyowezeshwa kupata Mafunzo ya ufugaji bora wa kuku katika kujiongezea kipato ili kuepukana na shughuli za uharibifu wa mazingira.
Zao la Mkonge ni moja ya zao linalo himili hali ya ukame..Pichani ni shamba la Mkonge lililopo shule ya Msingi Mihama kata ya Lagana wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga. Shamba hilo ni manufaa kutoka katika Mradi wa EBARR.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kiholeli wilaya ya Kishapu, mkoa wa Shinyanga Kuhwema Mashala Masanja akikagua lambo la maji lililopo katika mtaa wake ambapo lambo hilo ni manufaa ya mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo Ikolojia vijijini (EBARR).
Mnufaika wa jiko banifu Mama Teleza John, mkazi wa Kijiji cha Kiloleli wilayani Kishapu, Shinyanga akitumia jiko lake hilo linalotumia nishati ndogo ya kuni. Majiko hayo yamejengwa ili kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi, kupitia Mradi wa EBARR.
Kuanzishwa kwa Vikundi vya ufugaji wa nyuki vijijini ni moja ya njia inayotumiwa katika mradi wa wa kuhimili mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia mifumo Ikolojia vijijini(EBARR), ikiwa ni njia mojawapo ya kuhimili athari za mabadiliko ya Tabianchi katika maeneo yao.
Mwanakijiji Modesta Mussa, mnufaika wa lambo la maji kutoka kijiji cha Kiloleli kata ya Kiloleli wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga akichota maji katika lambo la kijiji hicho. Pichani ni lambo ambalo limejengwa kupitia mradi wa EBARR.
Kikundi cha vijana cha kuchakata ngozi Kilangale kutoka kiwanda kidogo cha kutengeneza bidhaa za ngozi kilichopo kijiji cha Kiloleli wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanya wakiwa kazini. Ujuzi huo ni moja ya manufaa waliyopata vijana kumi toka kijijini hapo kupitia mradi wa EBARR.
Kikundi cha wakina mama wa Kijiji cha Kiloleli kata ya Itilima wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, wakiwa katika kazi ya ujasiriamali wa utengenezaji wa bidhaa mbalimbali kupitia mradi wa Kuhimili mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini ( EBARR ).
Wakazi wa shehia tatu za Matemwe, katika Wilaya ya Kaskazini A Unguja, wamenufaika na upatikanaji wa maji ya uhakika kupitia kisima kirefu kilichochimbwa na mradi wa EBARR. Mradi wa huu unatekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wakazi wa kijiji cha Mingo, wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro wamenufaika na upatikanaji wa maji ya uhakika kupitia kisima kirefu kilichochimbwa na mradi wa EBARR. Mradi wa huu unatekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.