โGhalib ni Bilionea ambaye amewekeza kwa muda mfupi na timu inakaribia kwenda nusu fainali, kuna watu wamewekeza pesa, masimango, vichambo, minuno na kila aina ya gubu na wanaishia robo fainali,โ Ally Kamwe
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua @victoria.mwanziva kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe.
#WasafiDigital
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Tanga Mhe. Halima Abdallah Bulembo, amehamishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni iliyoko mkoani Dar es Salaam.
#WasafiDigital
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar Es Salaam, Mhe. Kherry Denis James, amehamishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbulu iliyoko mkoani Manyara.
#WasafiDigital
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Shaka Hamdu Shaka kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro.
Shaka Amewahi kuwa Katibu wa NEC itikadi na Uenezi CCM.
#WasafiDigital
Mchezo Ulikuwa Mzuri Kweli. Tumecheza Vizuri Kweli. United ni tishio kubwa kwenye mabadiliko, Nawapongeza sana, nimefurahi kuja Trafford na Kucheza, wametuadhibu kwenye mabadiliko,โ Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola
#WasafiSports
"Tuma kwa namba hii" ikiwa imetumwa kwa namba tofauti tofuati .
Pia wamekamatwa wakiwa na pesa taslimu shilingi laki saba ambazo ni pesa walizokuwa wamekwisha tapeli watu, huku wakiwa wanasubiri wengine kutuma kisha zinapotumwa zinatolewa haraka kwa wakala wa mitandao husika.
Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 11 kwa tuhuma za utapeli wa kutumia simu kwa kupokea hela kupitia jumbe za "Tuma kwa namba hii"
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani kilimanjaro ACP Simon Maigwa amesema watuhumiwa hao wamekamatwa katika eneo la
Matindigani manispaa ya Moshi wakiwa chumbani wakitapeli kwa njia ya mtandao.
Watuhumiwa hao wamekamatwa na simu za aina tofauti 19 ambapo kati ya hizo simu nane ni (Smartphone) na simu 11 ni simu ndogo ambapo baada ya kupekuliwa zilikutwa jumbe