HUDUMA ZA AFYA ZA KIBINGWA ZINAONGEZAKA NCHINI
Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imezindua huduma ya kibingwa ya matibabu ya maumivu sugu ya mgongo na kichwa bila upasuaji.
Huduma hiyo ya kwanza Tanzania tayari imewanufaisha mamia ya Watanzania.
#MamaYukoKazini
𝐔𝐇𝐀𝐊𝐈𝐊𝐀 𝐖𝐀 𝐔𝐒𝐀𝐅𝐈𝐑𝐈 𝐍𝐀 𝐔𝐒𝐀𝐅𝐈𝐑𝐈𝐒𝐇𝐀𝐉𝐈 𝐁𝐈𝐃𝐇𝐀𝐀
Daraja la Kiyegeya, Morogoro ni kiungo muhimu cha kiuchumi kwa mikoa ya Kanda ya Kati, Kanda ya Ziwa na nchi jirani za Rwanda na Burundi.
#MamaYukoKazini
Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mwanasoka wa Karne kutoka Brazil Edson Arantes do Nascimento “Pelé”. Mchango wake katika soka Duniani utakumbukwa daima. Pole kwa Rais wa Brazil @jairbolsonaro, familia & mashabiki wote wa soka. Mungu amweke mahali pema peponi, Amina.
Vijana ni nguvu kazi na chachu ya ukuaji uchumi wakiwekewa mazingira wezeshi. Mpango wa Mhe. Rais Samia Suluhu kwa kushirikiana na AfDB ni kuwapa vijana maeneo bora ya biashara, huduma za kifedha na misaada ya kiufundi katika biashara zao. #MamaYukoKazini
Dua | Sala
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akishiriki dua ya kuomba ulinzi na mwongozo wa Mwenyezi Mungu kabla ya kuanza kwa Mkutano Mkuu wa 10 wa Jumuiya ya Wanawake Taifa (UWT). #MamaYukoKazini
"Kama mnavyojua uwezo wa kiuchumi unainua uwezo wa siasa, kwahiyo tusiposimama vizuri na kwa sababu hatuna nguvu ya kiuchumi, huwenda tukanunuliwa kisiasa, naomba twende tukajipange na miradi mizuri ambayo inaweza ikatupa nguvu". - Mheshimiwa Rais Samia Suluhu
#MamaYukoKazini
"Nasema tusimame na serikali kwa sababu ya kwenda kufanya malengo ya Taifa bila kujali itikadi zetu za kisiasa, wote kama watanzania tunatakiwa twende tusimame na serikali tukafanye maendeleo ya kitaifa". - Rais Samia Suluhu.
#MamaYukoKazini
Nina heshima kubwa sana kwa SSH so far. Kutoa nchi ilipokuwa hadi hapa ilipo, yenye amani bila clashes za elites (maana tawala zinapobadilika hii ndo chanzo cha moto) naamini kuna siku watu wataandika historia ya haya. Keep going Mama. History Will Absolve You. Keep going.
Nimeshtushwa na vifo vya Watu 14 wakiwemo Wanahabari 6 vilivyotokea leo asubuhi baada ya gari lililokuwa katika msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kugonga na Daladala. Poleni Wafiwa, Wanahabari na jamaa wote. Mungu aziweke mahali pema roho za Marehemu na Majeruhi wapone haraka.
"Mapinduzi ya kisiasa yamekwisha, yaliyopo sasa ni mageuzi ya kiuchumi na mapinduzi ya kimaendeleo. Twendeni kama Wazanzibari tukashikane mkono kwa mkono, tujenge nchi yetu, tupate maendeleo, kila mtu aishi kwa kiwango anachopaswa kuishii."- Mhe. Rais Samia Suluhu #MamaYukoKazini
Mheshimiwa Rais, Samia Suluhu ametuma salamu za pole kwa familia na Watanzania wote kufuatia vifo vya watu 14 katika ajali ya barabarani mkoani Simiyu.
Kampuni ya Australia, BHP inawekeza TZS bilioni 230 katika mradi wa Kabanga Nickel mkoani Kagera, kuzalisha madini yanayohitajika kutengeneza betri na magari ya umeme. Tanzania itanufaika kwa kuongeza mapato ya serikali, ajira na kukua kwa biashara ya madini. #MamaYukoKazini
Tarehe 22/04/2021, Rais Samia Suluhu akihutubia bungeni aliahidi kufikisha maji kwa wananchi kwa 95% mijini na 85% vijiji ifikapo mwaka 2025.
Kuelekea kufikia malengo hayo leo hii wananchi wa Longido wanapata maji kwa 100% kutoka 15% walizokuwa wakipata awali.
#mamayukokazini
Rais, Samia Suluhu kuhudhuria Mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi.
Tarehe 2/11/2021, Rais Samia atahutubia mkutano huo.
Pia atafanya mazungumzo na viongozi mbalimbali ili kuimarisha ushirikiano na kuitangaza Tanzania.
#mamayukokazini
Athari za mabadiliko ya tabianchi kwa Watanzania:
1. Kuongezeka kwa majanga ya asili (mafuriko, ukame, joto kali na vimbunga)
2. Kuhatarisha afya za watu
Ziara ya Rais Samia nchini Scotland ni ya kuweka mikakati ya kukabiliana na janga hilo ili kuokoa maisha. #mamayukokazini