Wananchi na wadau mbalimbali wakiendelea kujitokeza kwa wingi kutembelea banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) lililopo kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Juma Mkomi, ni miongoni mwa viongozi na wadau waliotembelea banda la WCF katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, 2026 kwenye viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma.
Bodi ya Wadhamini, Menejimenti na Wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wanawatakia Waislamu na Watanzania wote Kheri ya Sikukuu ya Eid-Al-Adha
Mfanyakazi Hodari wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa mwaka 2026 Bw. Omar Juma Omar amekabidhiwa rasmi cheti chake na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya.
Zoezi hilo la kukabidhi cheti hicho kwa Mshindi limefanyika leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mafunzo kuhusu huduma zinazotolewa na WCF kwa Chama cha Wafanyakazi kwenye Vyombo vya Habari nchini(JOWUTA) kutoka mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Chama cha Wafanyakazi kwenye Vyombo vya Habari nchini (JOWUTA) kutoka mikoa ya Dar es Salaam na Pwani wamepatiwa elimu kuhusu huduma na mafao yanayotolewa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).
Mafunzo hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam ambapo Washiriki walipatiwa elimu na wataalam kutoka WCF kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo taratibu za madai ya fidia.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi, alipongeza ushirikiano huo kati ya WCF na JOWUTA na kutoa wito kwa pande zote mbili kushirikiana katika kuongeza juhudi za kutoa elimu kwa umma kuhusiana na umuhimu wa huduma zinazotolewa na WCF kwa wafanyakazi wanaopata ajali, ugonjwa ama kufariki kutokana na kazi.
WCF Yaendelea Kuunga Mkono Dhamira ya Serikali Kulinda Haki za Wafanyakazi
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umeendelea kuunga mkono dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuhakikisha haki za wafanyakazi zinalindwa.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma, wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa Rasilimali Watu na Utawala pamoja na Maafisa wa Usalama na Afya kutoka mikoa mbalimbali nchini, kilichofanyika hivi karibuni mjini Singida.
Amesema mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa WCF wa kuwajengea uwezo wadau mbalimbali kutoka sekta ya Umma na binafsi ili kuongeza uelewa kuhusu huduma zinazotolewa na Mfuko ikiwemo kuijua sheria ya fidia kwa wafanyakazi na mifumo ya kidijitali inayotumika katika kushughulikia ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.
“Tunapowekeza katika elimu ya fidia kwa wafanyakazi tunalinda nguvu kazi ya taifa na kuongeza tija katika uzalishaji; ni wajibu wa kila mmoja wetu kuhakikisha kuwa wafanyakazi wana uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya fidia kwa wafanyakazi”. Amesema Dkt. Mduma
Aidha, amewataka washiriki kutumia mifumo ya kidijitali ya WCF ili kurahisisha upatikanaji wa huduma na kuongeza ufanisi kwa waajiri na wafanyakazi kote nchini.
Vilevile, amewaasa washiriki kutumia mafunzo hayo kama chachu ya mabadiliko katika taasisi zao ya kuzingatia kanuni za usalama na afya mahali pa kazi ili kupunguza ajali na magonjwa yatokanayo na kazi hivyo kuongeza ustawi wa wafanyakazi na kuchochea maendeleo endelevu ya uchumi wa Taifa.
Mmoja wa washiriki wa kikao kazi hicho, Bi. Neema Msuya kutoka Wilaya ya Iramba, alisema mafunzo hayo yamekuwa na manufaa makubwa katika kuwaongezea uelewa kuhusu masuala ya fidia na taratibu za kuwasilisha madai ya wafanyakazi pale mfanyakazi atakapo ugua au kuumia kutokana na kazi.
“Tumepata elimu muhimu kuhusu namna ya kushughulikia ajali kazini na kutumia mifumo ya kidijitali ya WCF. Hii itatusaidia kutoa huduma bora zaidi kwa wafanyakazi katika taasisi zetu,” alisema Bi. Msuya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete, akimkabidhi tuzo Mkuu wa Kitengo cha Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Festo Kandonga, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo kwa kutambua mchango wao katika kufanikisha Mkutano wa Pili wa Mwaka wa Jumuiya za Wataalamu wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Utumishi wa Umma (AAPAM). Tukio hilo limefanyika tarehe 6 Mei jijini Arusha wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo.
HONGERA
Bodi ya Wadhamini, Menejimenti na Watumishi wa WCF tunakupongeza Mhe. Dkt. Evaline Wilbard Munisi kwa kuteuliwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Mahusiano. Tunakuahidi ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemkabidhi tuzo ya shukrani Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma, wakati wa sherehe za Mei Mosi zilizofanyika katika viwanja vya Halmashauri ya Mji wa Njombe, eneo la Lunyanywi, Mei 1, 2026.
WCF Yashiriki Maadhimisho ya Mei Mosi Njombe
Menejimenti na Wafanyakazi wa WCF, walijumuika na wafanyakazi wengine katika kusherehekea Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi 2026), iliyofanyika katika viwanja vya Halmashauri ya Mji wa Njombe, eneo la Lunyanywi.
Bodi ya Wadhamini, Menejimenti na Wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) tunakupongeza kwa kuchaguliwa kuwa Mfanyakazi bora nafasi ya tatu wa Taasisi kwa mwaka 2026.
Bodi ya Wadhamini, Menejimenti na Wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) tunakupongeza kwa kuchaguliwa kuwa Mfanyakazi bora nafasi ya tatu wa Taasisi kwa mwaka 2026.
Bodi ya Wadhamini, Menejimenti na Wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) tunakupongeza kwa kuchaguliwa kuwa Mfanyakazi bora nafasi ya pili wa Taasisi kwa mwaka 2026.
Bodi ya Wadhamini, Menejimenti na Wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) tunakupongeza kwa kuchaguliwa kuwa Mfanyakazi bora wa Taasisi kwa mwaka 2026
Bodi ya Wadhamini, Menejimenti na Wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wanawatakia kheri watanzania wote katika kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani (Mei mosi).