Tunasikitika kuwataarifu Show ya @cookwithwema Jumatano ya leo itachelewa kuruka hewani kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu, jitihada za haraka bado zinaendelea.
Kutokana na sababu zilizopo nje ya uwezo wetu, Cook with Wema Sepetu show ya Leo itachelewa kuruka hewani, Tunaomba radhi kwa usumbufu huu. Tunaendelea na jitihada za kuhakikisha inaenda hewani haraka iwezekavyo.
Nilifungua Kampuni ya matangazo na Client wangu mkubwa ni GSM. Naandaa Album itakuwa One of the Best na majina makubwa ya ndani na nje ya nchi. #OmmyDimpoz#CookWithWemaSepetu
Maisha lazima uwe na Plan B wakati nimeumwa nilipoteza sauti nikajiuliza kumbe kile kitu unachojivunia Mungu anaweza kukichukua anytime, Nikaona nijaribu kuingia kwenye Biashara. #OmmyDimpoz#CookWithWemaSepetu
Me mnyamwezi kabisa sababu nimelelewa upande wa Mama, Baba alikutana na Mama Tabora, niliambiwa Baba alienda kupanga nyumbani kwao na Mama sema mpangaji akajiongeza kwa mtoto wa mwenye nyumba. #OmmyDimpoz#CookWithWema
Marehemu Mama yangu alikuwa ananipikia sana Makande, sasa sijajua ilikuwa ni kulingana na hali ya kimaisha lakini ikaja kuwa ndio My Favorite Food. #OmmyDimpoz#CookWithWemaSepetu
Tunaomba radhi kipindi cha Cook with Wema Sepetu Episode 06 itachelewa kuruka hewani badala ya saa 7:30pm itakuwa 8:30pm - 9:00pm kutokana na sababu zisizoweza kuzuilika, Bado tunaendelea na jitihada za haraka zaidi. Tunakusii usikae mbali na @wemaapp
Mtu machachari sana huyu... Jikoni kulikuwa kuna raha mno... Asante kwa kuja baby... Sio baby baby sasa usije ukazua balaa... Go to Wema App, Show ipo ON tayari... 😂😂😂 Mwenyewe anajiita Chawa Pro Max... @wemaapp@bestizzo
Rommy alikuwa boyfriend wangu tangu mwaka 2009, Nilivyokuwa nipo single mwenzangu alivyo jipitisha Tukapitiana, Upendo wa kweli uwa haufi maisha tu ndio yalifanya tukaachana. #Shilole#CookWithWemaSepetu
Sijawahi kukata tamaa in real life, I appreciate ninachokifanya, namkaribisha sana Mungu kwenye Maisha yangu na ninatumia nguvu nyingi sana kufanya kazi zangu. #Shilole#CookWithWemaSepetu
Ndoa ya Kiislam haihitaji kelele, tulikubaliana na mwenzangu, tukakubaliana na ndugu zake, tukaenda kufunga Ndoa, hadi watoto wangu walikuwepo kwenye ndoa. #Shilole#CookWithWemaSepetu