Falsafa ;
Katika siasa, propaganda si tu kuhusu kushawishi watu; pia ni kuhusu kujenga mazingira ambayo wapinzani wanajipima mbele ya umma. Ndiyo maana kila uamuzi wa kisiasa unaweza kuwa na matokeo yaliyokusudiwa na mengine yasiyokusudiwa.
Falsafa;
Wanasiasa 95% wanafanana siasa ni ajira kwao wanatumia siasa kuendesha maisha yao. Siasa kwao ni mradi/biashara. Wakati mwingine siasa ndio biashara inayolipa zaidi bila kufuata kanuni za kibiashara.
Falsafa;
Sayansi ya siasa hufundisha kuwa propaganda yenye mafanikio si ile inayomzuia mpinzani kuonekana, bali ile inayomwezesha umma kujionea tofauti za uwezo, uadilifu na sera, kisha wananchi wafanye uamuzi wao kwa taarifa walizoziona wenyewe.
Falsafa ;
Katika siasa, propaganda si tu kuhusu kushawishi watu; pia ni kuhusu kujenga mazingira ambayo wapinzani wanajipima mbele ya umma. Ndiyo maana kila uamuzi wa kisiasa unaweza kuwa na matokeo yaliyokusudiwa na mengine yasiyokusudiwa.
Falsafa;
Kwa hiyo, swali la msingi si kama kuzuia mikutano ni sahihi au si sahihi pekee. Swali ni kama mkakati huo unatimiza malengo ya kisiasa yaliyokusudiwa au kama unazalisha athari ambazo hazikutarajiwa katika mtazamo wa wananchi.
Falsafa:
Kuna matatizo(problems) na kunachangamoto(challenges) ni viwili tofauti vinafanana au vyenye uhusiano wa karibu. Changamoto wkt mwingine zikikosa kufanyiwa kazi ugeuka kuwa tatizo. Ila Changamoto ndizo zinafanya maisha kuwa na ladha.
Maisha ni kama mfululizo wa kutatua matatizo.
Unapokuwa unamalizana na moja, jingine tayari linafanya warm up๐
Tofauti si kukosa matatizo, bali kujifunza kuyakabili kwa hekima, uvumilivu na moyo wa kusonga mbele.๐ค๐ผ
Falsafa:
Hoja zako ungezijenga kuhusu yeye kuifanya CDM kuwa agenda yake ila kusema nafasi yake ipo mashakani sidhani kama ni sahihi maana anaweza kuondolewa hapo ambako hana power akapewa nafasi ingine yenye power mifano ipo mingi.
Katika mabadiliko yanayotarajiwa ndani ya CCM, nina taarifa kwamba nafasi ya huyu bwana si salama. Ndiyo maana siku hizi amegeuza CHADEMA kuwa ajenda yake ya kila siku. Anatafuta relevance kwa kuwataja viongozi wa upinzani na CHADEMA akiamini kelele zinaweza kuziba upungufu wa upumbavu alionao. Yuko kwenye kampeni ya kupigania nafasi yake.
Falsafa:
Tatizo si kuwa na kipato , bali pale ambapo ulinzi wa kipato unakuwa muhimu zaidi kuliko ulinzi wa mahusiano. Fedha ni rasilimali, lakini upendo, uaminifu na muda wa pamoja ndio mtaji wa mahusiano. Wkt mwingine ni vigumu Ku balance.
Umasikini ni kishikizo kikubwa cha mahusiano mengi. Ukishatatua tatizo la umasikini wa kipato watu wengi wanagundua kumbe wanaweza kuwa โsingle and happy.โ
Falsafa;
Ukiona mateso, chagua huruma.
Ukiona udhaifu, chagua ukimya au msaada. Kwa sababu katika mizani ya maisha, si unachosema tu kinahesabiwa, bali roho iliyobeba maneno hayo.