🎥 VIDEO RECAP || Shukrani za dhati kwa wote waliohudhuria kikao chetu na Maafisa Maendeleo ya Jamii (CDOs), viongozi wa vikundi vya mradi wa Youth Economic Empowerment, Msajili wa Vikundi kutoka Dodoma, na mwakilishi wa Restless Development.
#YouthEmpowermentTz | #Mulika255
Zawadi kutoka Mulika Tanzania bado zinaendelea! 🎁✨
Na kupata nafasi ya kushinda ni rahisi unachotakiwa kufanya ni kufollow ukurasa wetu, kulike machapisho, kurepost na kucomment kwa wingi.
Ukifanya hivyo mara kwa mara, nafasi yako ya kujipatia zawadi kabambe inaongezeka zaidi!
Jumla ya wasichana waliozaa katika umri mdogo 418 wamewezeshwa kupitia mafunzo ya ujasiriamali, usimamizi wa fedha, Pamoja na kuunganishwa kwenye vikundi vya mikopo ya 10% kutoka halmashauri.
#YouthEmpowermentTz | #Mulika255
Our end-of-year dinner was a moment to reflect, appreciate,and celebrate what we have achieved together throughout the year.From shared milestones to meaningful impact, this journey would not be possible without the commitment and passion of everyone.
#happynewyear | #mulika255
Elimu ni msingi wa ajira bora, ubunifu, uchumi imara na maendeleo endelevu. Bila kuwekeza kwa vijana leo, tunahatarisha kesho ya Tanzania.
#ElimuKwaVijana | #mulika255
In this season of renewal, may we commit to growth, not only personally, but how we uplift those around us.
"From dust we came, and to dust we shall return.”
#AshWednesday | #mulika255
Kupitia sera jumuishi, uwekezaji sahihi, na programu zinazoweka vijana katikati ya maendeleo, tunaweza kubadilisha takwimu kuwa mafanikio.
Mulika Tanzania tunaamini kuwa: Vijana si tatizo ni suluhisho, Uwezeshaji wa vijana ni uwekezaji wa Taifa.
#YouthEmployment | #mulika255
Allah aikubali saumu na ibada zetu, atusamehe makosa yetu, na atujalie rehema Zake katika mwezi huu wenye baraka.
Tunawatakia Ramadhani yenye amani na baraka tele.
#RamadhanMubarak | #Mulika255
Dhumuni kuu la kikao kilikuwa:
✓ Kuweka mikakati madhubuti ya kuboresha utekelezaji wa mradi
✓ Kuimarisha uratibu kati ya CDOs, vikundi, na watekelezaji
✓ Kuongeza ufanisi katika kuwawezesha vijana kiuchumi
#YouthEmpowermentTz | #Mulika255
Mulika Tanzania tumefanya kikao muhimu na Maafisa Maendeleo ya Jamii (CDOs) kutoka wilaya za mkoa wa Dodoma, pamoja na viongozi wa vikundi tulivyoviunda kupitia mradi wa Youth Economic Empowerment.
#YouthEmpowermentTz | #Mulika255
Heri ya Kilele cha Wiki ya Vijana 2025 Kitaifa, tunapoadhimisha wiki hii yenye kauli mbiu “Nguvu Kazi ya Vijana kwa Maendeleo Endelevu,” tunatambua nguvu, ubunifu, na mchango mkubwa wa vijana katika kuijenga Tanzania yenye maendeleo na usawa.
#WikiYaVijana2025 | #Mulika255
Tunapozungumzia maendeleo shirikishi, hatuwezi kuyaona bila kuhakikisha kwamba kila kundi la kijamii linapewa nafasi ya kushiriki na kushika nafasi za uongozi.”—Jennifer Kayombo, Mkufunzi wa masuala ya afya na jinsia
#YouthLeadership | #Mulika255
Maneno ya kuvutia (‘captions’) yanapaswa kuwa makini na yenye mvuto, huku ‘hashtags’ zikitumika kwa usahihi ili kuongeza mwonekano na ushiriki wa hadhira.”—Wilbgeorge Bahati, Mkufunzi wa masuala ya Mawasiliano na mitandao ya kijamii.
#YouthLeadership | #Mulika255
“Mitandao ya kijamii ni zana muhimu kwa kila kiongozi kijana hasa katika kujijengea jina. Kila kijana kiongozi anaweza kutumia jukwaa hili kufanya kampeni za kidigitali.”—Wilbgeorge Bahati, Mkufunzi wa masuala ya Mawasiliano na mitandao ya kijamii
#YouthLeadership | #Mulika255
Baadhi ya Washiriki waliohudhuria katika mradi wa Youth Leadership Dodoma nakuonyesha ushiriki wa hali ya juu kupitia mijadala, maoni na ubunifu wao. Ushiriki wao madhubuti ni kielelezo cha ari ya vijana katika kujifunza.
#YouthLeadership | #Mulika255
📽 SANDE SANA BHAGOGO, Mulika Tanzania inapenda kutoa shukrani za dhati kwa washiriki wote wa programu ya YOUTH LEADERSHIP TRAINING iliyofanyika jijini Dodoma.
#YouthLeadership | #Mulika255
Baadhi ya washiriki waliopata zawadi kutoka kwenye mradi wa YOUTH LEADERSHIP TRAINING uliofanyika Dodoma, hasa kwa kuwa wa kwanza kutufollow, kulike na kucomment kwenye mitandao yetu ya kijamii.
#YouthLeadership | #Mulika255