Zanzibar Female Lawyers Association is Non Government organization which deals with legal aid and human understanding for women and children's affairs.
Wanafunzi wapatiwa Mbinu mpya ya Utengenezaji Sabuni za Miche n karafuu
Katika juhudi za kukuza ujuzi wa ujasiriamali, wanafunzi wamepatiwa mafunzo ya vitendo ya kutengeneza sabuni za miche na sabuni za kuogea zenye viungo vya karafuu.
Scrub ya kahawa yawavutia Wanafunzi ki biashara
Wanafunz wa kike wa ujasiriamali wameonyesha ubunifu wao kwa vitendo kwa kutengeneza bidhaa ya scrub ya kahawa baada ya kupewa mafunzo ya nadharia na Mkufunzi katika mafunzo ya siku Nne ya kuwajenga kiuchumi huko Kwerekwe Unguja
Day 3
Mapema leo hii Septemba 19 katika mwendelezo wa mafunzo ya Ujasiriamali huko katika ukumbi wa Malaria Kwerekwe, Wanafunzi wamepata nafasi ya kujifunza kwa vitendo mbinu mbalimbali za Uaandaji wa Pishi la achari kwa ajili ya biashara.
Day 3
“Lazima tuzingatie kanuni za maandalizi ya mapishi ya achari ya mbirimbi na embe; usafi ni jambo la kwanza na la msingi. Vifaa vyote vya kupikia vinapaswa kuoshwa vizuri, matunda yachaguliwe yaliyo mabichi na safi, na viungo viwekwe kwa uwiano sahihi.
Day 2
*Kutoka Soya kuwa Maziwa kimiminika : Wanafunzi waanza mafunzo kivitendo*
Katika muendelezo wa Mafunzo ya Ujasiriamali,leo Septemba 18 wanafunzi wanawake 30 wamepatiw mafunzo ya vitendo ya maandalizi ya maziwa ya soya.
Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Malaria
Day 2
*DARASA LANUKIA SPICES*
Baada ya kujifunza kutengeneza maziwa ya soya ya kimiminika, wanafunzi hao pia wanapewa ujuzi wa kuchanganya viungo vya chai, pilau, na biriani kwa vipimo maalum vinavyohakikisha ladha bora na ubora wa chakula.
“Spices zina soko pana kuanzia mitaani mwetu hadi kwa watalii. Sisi Wazanzibari tunapenda spices, na wageni wetu pia wanazithamini. Tuchangamkie fursa hii ya kuzalisha, kubuni na kuuza ili kuinua kipato na jamii zetu.”Mwanaisha Mustafa- Afisa Mradi -ZAFELA
ZAFELA Yazindua Rasmi Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia Kaskazini Pemba
Leo, tarehe 26 Novemba 2024, Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) imezindua rasmi Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia Kaskazini Pemba.