SALA YA JIONI.
Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina.
Tunakushukuru ee Mungu kwa mema yote uliyotujalia sikuu hii ya leo.
BABA YETU.
Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina.
SALAMU MARIA.
Salam Maria umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Maria Mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
SALA YA IMANI.
Mungu wangu, nasadiki maneno yote. Linayosadiki na linayofundisha Kanisa Katoliki la Roma. Kwani ndiwe uliyetufumbulia hayo. Wala hudanganyiki, wala hudanganyi. Amina.
SALA YA MATUMAINI.
Mungu wangu, natumaini kwako, nitapewa kwa njia ya Yesu Kristo. Neema zako hapa duniani, na utukufu mbinguni. Kwani ndiwe uliye agana hayo nasi, nawe mwamini. Amina.
SALA YA MAPENDO.
Mungu wangu, nakupenda zaidi ya chochote. Kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza. Nampenda na jirani yangu, kama nafsi yangu, kwa ajili yako. Amina.
UNGAMO LA DHAMBI.
Na tuwaze katika moyo makoda yote ya leo tuliyomkosea Mungu, kwa mawazo, kwa maneno na kwa matendo(………………………)
Namuungamia Mungu Mwenyezi, nanyi ndugu zangu, kwani nimekosa mno, kwa mawazo, kwa maneno, kwa vitendo na kwa kutokutimiza wajibu, nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana. Ndio maana nakuomba Maria mwenyeheri, Bikira daima, malaika na watakatifu wote, nanyi ndugu zangu, niombeeni kwa Bwana Mungu wetu.
+Mungu Mwenyezi atuhurumie, atusamehe dhambi zetu na atufukishe kwenye uzima wa milele, Amina.
SALA YA KUTUBU.
Mungu wangu, nimetubu sana niliyokosa kwako. Kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza. Wachukizwa na dhambi, basi sitaki kukosa tena. Nitafanya kitubio, naomba neema yako nipate kurudi. Amina.
Ee Mungu mwenye huruma, uwashushie baraka zako, Baba Mtakatifu wetu Francis na maaskofu, na mapadre, na mashemasi, wakulima, wafanyakazi wote, wanafunzi na jamii yote unaowafanya kuwa watu wako . Uwaokoe wale wasiokujua bado, uwafariji wagonjwa, waelekee wanaozimia waweze kuona mwanga wa milel, Amina.
ANGELUS.
Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria,naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
~Salamu Maria umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
Ndimi mtumishi wa Bwana, nitendewe ulivyosema.
~Salamu Maria umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
Neno wa Mungu akatwaa mwili,akakaa kwetu.
~Salamu Maria umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
Utuombee mzazi Mtakatifu wa Mungu,tujaliwe ahadi za Kristo.
Tuombe:
Tunakuomba ee Bwana utie neema yako mioyoni mwetu,ili sisi tuliojua kwa maelezo ya malaika,kwamba Kristo mwanao amejifanya mtu;kwa mateso na msalaba wake,tufikishwe kwenye utukufu na ufufuko.
Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Bikira Maria Malkia wa amani~Utuombee!
SALA KWA MALAIKA MLINZI.
Malaika mlinzi wangu, unilinde katika hatari zote, za roho na za mwili. Amina.
Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Kama mwanzo na sasa na siku zote na milele. Amina
Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina🙏
ROZARI TAKATIFU MATENDO YA UTUKUFU (Jumatano na Jumapili)
1. Yesu anafufuka. Tumwombe Mungu atujalie kugeuka watakatifu.
2. Yesu anapaa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kwenda mbinguni.
3. Roho Mtakatifu anawashukia Mitume. Tumwombe Mungu atujalie bidii katika dini yetu.
4. Bikira Maria anapalizwa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kufa vizuri.
5. Bikira Maria anawekwa Malkia mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia njema.
I hope tumejifunza kitu leo kwenye hii issue ya Miss Grand.
Mmefanyishwa kampeni, Mwisho wa siku kampeni inatumika kumsafisha muuaji wa Watanganyika…….
Tunapowaambia hawa watu wanatumika na wauaji kuwatoa kwenye focus muwe mnaelewa……..
Msikubali kutumika kama condom
Hii ni TARIME wananchi wanataka KATIBA MPYA na LISSU aachiwe.
Hii nyomi inawaumiza sana WAKOLONI WEUSI. Chama kinaendelea kupendwa kila kona ya NCHI.
Repost 200
Naona viwaandishi uchwara vinawashwa na mimi.
Ni hivi sitoi kiki…..
WAMENISHINDWA MABOSI WENU MTANIWEZA NYIE MA HOUSEBOY???
NAONGEA NA MWENYE MBWA, SIONGEI NA MBWA!!!!!!!!!!!!
🚨TAARIFA
Mwanangu @Thereal_taivina kaibiwa Simu yake maeneo ya BUGURUNI na VISHANDU.
Wamekuwa wakitumia watu jumbe za KUOMBA PESA. Naomba usitume pesa yeyote kama ukitafutwa kwa namba ya Taivina.
REPOST 200.
Leo Jijini Brussels, jina la Mh Tundu Lissu anayekabiliwa na kesi feki ya uhani Tanzania limewasilishwa rasmi kwa Bunge la Ulaya kwa ajili ya Tuzo ya Uhuru wa Mawazo ya Sakharov 2026.
Mh Lissu amependekezwa na wabunge wa @EPPGroup na wale wa @ecrgroup.
USHAURI WANGU KWA VIJANA WANAOFAHAMIANA NA WANASIASA WALIOPATA TEUZI
Anaandika Mr Ben
Kijana, unapokuwa na ukaribu na mwanasiasa au kiongozi kabla hajapata nafasi kubwa ya uongozi, usifikiri kwamba ukaribu huo ni tiketi ya kudumu ya kuwa karibu naye katika kila hatua ya maisha yake ya kisiasa.
Wakati mwingine katika safari ya uongozi, unaweza kuwa sehemu ya safari ya mtu kwa kipindi fulani, unaweza kumsaidia, ukawa kiungo, ukawa daraja, ukafungua njia au ukawa mtu muhimu katika hatua fulani ya maisha yake. Lakini akishafika kwenye nafasi nyingine, mazingira hubadilika na mahusiano pia yanaweza kubadilika.
Ndiyo maana ni muhimu kujua wakati wa kusogea mbele na wakati wa kurudi nyuma kwa heshima. Mwanasiasa anapopata nafasi kubwa ya uongozi, mpe nafasi afanye kazi, atekeleze majukumu yake na ajenge taasisi yake. Usitumie historia ya ukaribu wenu kumlazimisha aendelee kukuchukulia kama zamani.
Kumbuka, si kila mtu aliyekuwa karibu na kiongozi kabla hajawa mkubwa ataendelea kuwa karibu naye baada ya kupata nafasi. Wengine walikuwa sehemu ya safari, wengine walikuwa daraja, wengine walikuwa wasaidizi wa kipindi fulani, na wengine walikuwa marafiki wa wakati huo. Hilo si lazima liwe jambo baya, ni sehemu ya mabadiliko ya maisha na uongozi.
Kijana mwenye hekima anatambua kwamba heshima ni muhimu kuliko kulazimisha ukaribu. Usimfuate kiongozi kila mahali kwa sababu tu mliwahi kuwa karibu. Usijenge tabia ya kumtafuta kila mara kwa sababu unahisi una haki kutokana na historia yenu.
Wakati mwingine, kurudi nyuma kimkakati ndiyo njia ya kuhifadhi heshima yako, utu wako na hata uhusiano wenu. Endelea na maisha yako, jenga uwezo wako, fanya kazi zako na usubiri kama siku moja atahitaji uwepo wako au ushauri wako.
Na zaidi ya yote, usijenge maisha yako yote juu ya mtu mmoja kwa sababu tu leo ana nafasi kubwa. Jenga jina lako, uwezo wako, mtandao wako na thamani yako mwenyewe. Maana yake ni kwamba hata kama mazingira yakibadilika, wewe bado unabaki kuwa wewe.
Ukaribu unaweza kukufungulia mlango, lakini uwezo wako ndiyo utakaoamua utakaa ndani kwa muda gani..!
ROZARI TAKATIFU, ALHAMISI (MATENDO YA MWANGA)
1. Yesu anabatizwa mto Yordani.
2. Yesu anageuza maji kuwa Divai huko Kana.
3. Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu.
4. Yesu anageuka sura.
5. Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristi.
Bikira Maria Malkia wa Rozari Takatifu, Utuombee!