Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Mhe. Sivangilwa Sikalaliwa Mwangesi (Jaji wa Mahakama ya Rufaa) kuwa Kamishna wa Maadili.
Mhe. Mwangesi ameteuliwa kushika nafasi hiyo baada ya Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mstaafu Harold Nsekela kufariki.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohammed amesema katika harakati za kurekebisha Mtaala wa elimu ya Maandalizi na Msingi Wizara yake imejipanga ifikapo mwaka 2022 kupunguza idadi ya masomo ambapo Wizara itahakikisha inaingiza somo la historia kwa msingi pia.
Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametoa wito kwa Wataalamu wa lugha ya Kiswahili kutumia taaluma yao
Amewaambia Wataalamu hao wahakikishe Sheria na Sera za Serikali zinakuwa katika lugha ya Kiswahili ili kuwawezesha wananchi kuzifahamu vyema.
#zanzibar24habari
TANZIA: MKongwe wa Tasnia ya Maigizo nchini Tanzania Mohammed Fungafunga maarufu Kama Mzee Jengua amefariki dunia asubuhi ya leo huko Mkuranga Marehemu alikua akisumbuliwa na Maradhi ya Kuparalaizi.
#mzeejengua
#BREAKINGNEWS Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya Motisun Group ambaye pia ni mfanyabiashara mkubwa nchini, Subhash Patel amefariki dunia.
#zanzibar24breakingnews
Wawakilishi wa Zanzibar katika Mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika timu ya Mlandege Fc watacheza Mchezo wao wa kwanza na Club Sportif Sfaxien ya nchini Tunisia tarehe 28 ,11, 2020 Mchezo huo utakaochezwa katika uwanja wa Amaan Stadium majira ya saa kumi kamili 10:00 Alasiri.
ZPL R 1
Leo
Amaan: 10:00 Alasiri
JKU VS KIPANGA
MAU A: 10:00 Alasiri
KVZ VS Black sailor
Nov/ 21, 2020
MAU A: 10:00 Alasiri
Chuoni vs Malindi
Amaan:10:00 Alasiri
Polisi vs Mafunzo
Nov/ 22,2020
MAU A:10:00 Alasiri
Mlandege VS Hard Rock
Amaan:10:00 Alasiri
Zimamoto VS KMKM
Shirikisho la mpira wa miguu Zanzibar (ZFF) @zffzanzibar limetangaza Nembo mpya ya ligi kuu ya Zanzibar (ZPL).
Kwa mujibu wa ratiba ya ZFF leo Ijumaa 20/Nov/2020 msimu wa ligi kuu ya Zanzibar (ZPL) 2020-2021 unaanza Rasmi.
Kwa wale wanaohitaji nafasi za Ofisi na maduka katika jengo jipya la MICHENZANI MALL .
Fomu zinapatikana katika ofisi za ZSSF @ZanzibarZssf zilizopo kilimani Mnara wa Mbao.
Mechi ya Kirafiki Uhuru Stadium
FT: KMC -1 KMKM - 2
⚽ Matheo Anton Simon
⚽Iliasa Suleiman Mohammed
Goli moja pekee la KMC limefungwa na Kapalata dakika ya 37.
Kmkm wapo Tanzania Bara kwa ajili ya maandalizi ya ligi kuu ya Zanzibar (ZPL).
#zanzibar24michezo
Mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar (ZSSF) @ZanzibarZssf umeanzisha kutoa mkopo wa elimu kwa ngazi zote tokea cheti hadi shahada za juu.
Mkopo huu unalengo kuwapa fursa wanachama wa ZSSF ambao wamekosa fursa ya kujiendeleza kielimu kutokana na ukosefu wa fedha.
#zssfmkopowaelimu
Njia Rahisi ya kupakua App ya @ZanzibarZssf . Kama simu yako ni ya Android Ingia Playstore andika ZSSF MOBILE APPLICATION.
Kama ni mtumiaji wa Simu ya Iphone ingia App Store andika ZSSF MOBILE APPLICATION
#zssfapplication
@SabzMachano
Fao hili hutolewa kwa Mwanachama wa ZSSF ambaye amepata Maradhi ya kudumu.
Kwa hiyo mwanachama wa ZSSF atalazimika athibitishwe na Bodi ya Madaktari kulingana na maradhi yake au ulemavu alioupata uliomfanya ashindwe kufanya kazi.
#zssffaolaulemavu@ZanzibarZssf @SabzMachano