“Katikati hapa, tumedanganywa tukadangayika. Tumeletewa lugha laini ya uongo ya maridhiano. Tukakubali kupigwa maneno, tukaacha hoja za msingi: katiba mpya na mfumo mpya wa uchaguzi.” —
Tundu Lissu
Taifa letu na jamii yake, mfumo wetu wa haki jinai hautafaidika kwa Tundu A.M Lissu kuendelea kuwekwa kizuizini au kufungwa kwa mashtaka ya uongo ya uhaini.
Mwendelezo wa kutumia sheria vibaya kukandamiza wapinzani. Kwa sababu hizo, mnasababisha mitengano ya kijamii na kudhoofisha umoja wa kitaifa.
Tukiruhusu mbinu za kubuni mashtaka ya uhaini kunyamazisha wapinzani zifanikiwe, tunatoa mwanya mifumo ya kidikteta kutawala na kuzika haki za raia.
Mifumo ya kisheria ilitumiwa kama silaha (lawfare) kudhibiti upinzani katika tawala za KIDIKTETA za Amerika ya Kusini, Ulaya Mashariki na Afrika Kusini.
Ulaya ya Mashariki (katika zama za pazia la chuma). Amerika ya Kusini (katika zama mbaya za operation condor). Afrika Kusini (katika zama za Apartheid).
Mfano, utawala wa kibaguzi ulitumia sheria ya Suppression of Communism Act (1950) na Terrorism Act (1967). Aliyepinga ubaguzi wa rangi aliitwa GAIDI.
Lazima tulinde haki za raia dhidi ya mifumo inayotaka kufifisha demokrasia yetu. Taifa letu ni Taifa la Kidemokrasia. Haki ya watu kuchagua na kuchaguliwa.
Tukinyamaza leo, tunaruhusu misingi dhalimu ya kidikteta izike haki za raia na kurejesha mbinu za kibeberu katika ardhi ya nchi yetu. Tujisahihishe.
📍
Inawezekaneje Mbunge wa EAC, kuteuliwa kuwa Mbunge wa JMT?. Mtu mmoja anakuwaje na kofia mbili katika Taifa lenye watu zaidi 61m?, Mamlaka ya UTEUZI haikuona mtu mwingine tofauti na Kizigha?. Mwanasheria Mkuu wa Serikali anatimiza kweli wajibu wake wa Kikatiba (Ibara ya 59B).
DEAR African men, guard your heart against cheap theology. Gently teach your wife to walk in the ways of the LORD. Love your children and show them how to walk carefully in the world full of luring prosperity preachers. Teach them to look at you even as they choose to follow the LORD. Set a godly example for your home.
Have a happy Easter, kings.
Mnamtesa baba yao mlipotaka kumuuwa kwa risasi.
Familia ya LISSU ina maumivu na inateseka na baba yao kutoka hosp. hadi mahabusu.
VIONGOZI WA CCM, SERIKALI na vyombo vya dola mnaoshabikia mateso haya; laana hii mtailipa ndani ya familia zenu.
LISSU HANA HATIA MPENI UHURU WAKE.
Usipotuambia ni nani:
1. Alitoa amri ya kutumia risasi za moto kuuwa Watanzania?
2. Maiti zilitupwa wapi?
3. Wanaoitwa waandamanaji toka nje ni wa wapi? walilipwa na nani kiasi gani?
4. Amri ya kutotembea ilitolewa kwa mamlaka gani muda ulitosha?
5. Nani alitoa amri watu
JE, TUMESAHAU OKTOBA 29 HARAKA HIVI?
Leo ni Machi 29, 2026. Ni jumla ya siku 152. Wastani wa miezi mitano tangu mauaji ya kinyama ya raia kufanywa na Serikali kwa raia waliokuwa wanaandamana.
Hakuna ambaye anahusika na kutoa na kutekeleza amri amewajibika/amewajibishwa. Ni wazi hawajutii kwa kilichotokea. Leo najadili na wananchi wenzangu.
Ndugu zetu walipoteza maisha wakipigania haki. Wasanii wengi waliamua kusimama upande wa watawala na kuwapa sifa/utukufu wakati damu ilipomwagika.
Leo tunashangilia nyimbo zao siku nzima. Je, hii ndiyo ile “cancel culture” tuliyokesha na kujadili usiku kucha? Je, zile zilikuwa hasira za muda tu, na sasa zimepoa?
Tuliahidi kutozika kumbukumbu zao, lakini tumeshazika utu wetu kwenye “playlists” za wasanii waliochagua vipande vya shilingi kuliko uhai wa mashabiki wao.
Hao wasanii huwezi kuwatenga na uovu. Wakati wa maandamano, risasi zikirindima, hofu ikitawala. Wao walichagua kuimba sifa na kuachana na ukweli.
Ukishabikia na kueneza kazi za wasanii wanaotumika na Serikali ya CCM, utakuwa umesaliti kumbukumbu ya wale waliofia ardhi, haki, na mustakabali wetu.
Kususa kazi za wasanii lilikuwa hitaji la kimaadili, wito wa uwajibikaji (accountability). Tulihitaji kuwaona wasanii wakitambua wajibu wao kwa jamii/mashabiki.
Hii si kuhusu kuupenda au kutoupenda muziki. Ni kuwakumbusha usanii si burudani tu. Ni sauti ya jamii. Wakati wa shida, sauti hiyo itumike kwa niaba ya watu
Ni suala la hekima na uwajibikaji wa kijamii. Wasanii wana sauti yenye nguvu. Wanaweza kuwa sauti ya watu wakati wa shida, au kuwa zana ya propaganda.
Wakati damu ilipomwagika na hofu ilipotawala, kuchagua kuimba sifa tu (bila kutambua maumivu ya watu) kulionekana kama kuwatelekeza mashabiki.
Kabla ya kubishana nani msanii mkali, tukumbuke Oktoba 29, 2025. Damu ya ndugu zetu zisipuuzwe. Maisha yaliyopotea hayafai kufutwa na melody nzuri.
Tusiwape promo waliotupa kisogo wakati wa mateso. Tusipagawe na midundo na kuwaneemesha wale ambao hawaoni tatizo lao na bado hawajajirekebisha.
Hakuna muziki mzuri unaoweza kuzima kilio cha wanawake wajane na watoto yatima. Hakuna muziki unaoweza kufuta damu ya ndugu zetu iliyomwagika.
Wakati kodi zetu zilinunua risasi zilizowatoa roho ndugu zetu, wasanii hawa walitunga beti za sifa kwa watawala. Huwezi kutenganisha sanaa yao na uovu.
Kila mara unapocheza, ku-share, au kusifia kazi ya msanii aliyewapa kisogo wakati wa dhiki, unawazomea wajane na mayatima walioachiwa viti wazi mezani.
Unacheza dansi juu ya makaburi ya wale ambao hawakupata hata fursa ya kuzikwa. Wengine maiti zao hazikupatikana. Ndugu wamezika picha na nguo.
Msanii wa kweli ni kioo cha jamii, si pazia la kuficha ukatili. Msanii anayesimama na adui wa shabiki wakati wa mateso, amepoteza sifa ya kuwa sauti ya watu.
Usikubali ‘melodi’ nzuri iwe kilema cha kumbukumbu yako. Haki haijapatikana, na damu bado mbichi. Tusiwashangilie waliotusaliti kwa vipande vya fedha.
Let us never forget October 29, 2025. 💔
Labda wamuue ila akibaki hai huyu jamaa atakuwa Rais wa Tanzania, tena sio Urais wa kufosi kwa bunduki na uwizi wa uchaguzi ila Rais wa kuchaguliwa kidemokrasia na Watanzania wenyewe tena kwa raha zao.
Stay Strong @TunduALissu . Wataichelewesha haki ila hawawezi kuizuia.
Lissu amewauliza mashahidi WOTE wa kificho kama wametishiwa maisha na mtu yeyote, na wote wamejibu HAPANA. Kwa msiofahamu, DPP aliiomba mahakama kuficha mashahidi hawa kwa sababu WAMETISHIWA maisha yao. Anachokifanya Lissu ni kuithibitishia mahakama kuwa DPP & POLISI ni waongo.