@YerickoNyerereT Tangia uliposema mbowe atashinda na hakushinda nilishajiridhisha kuwa uwezo wako wa ku evaluate mambo na kufanya rational juggement nj wa chini sana
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 351
Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia cross examination, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Amani Golugwa.
Katuga: Kwahiyo Chadema haikushiriki kutokana na haki ya kikatba?
Golugwa: Ni kutokana na msimamo wetu wa no reforms no election
Katuga: Akitokea mtu anasema Chadema haikushiriki uchaguzi kwasababu katibu mkuu hakusaini kanuni za maadili ya uchaguzi atakuwa yuko sahihi au sio sahihi?
Golugwa: ni kweli kabisa tulizuiwa
Katuga: Haya majibu ya mlizuiwa na kuwa chadema kutokushiriki uchaguzi ni haki yake kikatiba yanafanana au hayafanani?
Golugwa: hayafanani
Katuga: Ulielezea jana hapa maushenzi katika chaguzi ulizosema mojawapo ni kama vile mawakala kutokupewa viapo, wasimamizi kutokupokea fomu za wagombea wa chadema, kubadili taatifa za wagombea wa chadema uliyaona pia katika uchaguzi wa 2015, 2019, 2020?
Golugwa: ndio nilieleza?
Katuga: Je mambo hayo pia uliyaona kwenye uchaguzi wa 2025?
Golugwa: Hatukushiriki uchaguzi ila kwa niliyoyaona na kuyasikia na kuyasoma yalinishangaza na kuniogopesha
Katuga: Mwaka 2024 na 2015 ni mwaka upi unaanza?
Golugwa: 2015
Katuga: Mwaka 2024 na 2020 upi unaanza?
Golugwa: 2020
Katuga: Jana ulisema yale mambo ya kishenzi uliyoyaona 2024 uliyaonaje mwaka 2015?
Golugwa: Kwa akili ya kawaida na memory ya kawaida tu si mtu unakuwa na kumbukumbu za nyuma?
Watu wanamcheka katuga anauliza swali la kishenzi๐๐๐๐๐
Katuga: Waambie Majaji kama Chadema ilishiriki uchaguzi Mkuu wa 2015
Golugwa: Ndio
Katuga: Mwaka 2015 chadema ilipata wabunge 35?
Golugwa: Ni zaidi ya wabunge 30
Katuga: Katiba ipi ilikuwa inatumika?
Golugwa: Katiba hii hii ya JMT
Katuga: Wewe unasema mwaka 2025 hamkushiriki uchaguzi, yale maushenzi ya 2024 uliyaonaje wakati chadema haikushirki uchaguzi?
Golugwa: Kama nilivyosema, niliyasikia, kuyasoma na kuyaona na vyama vingine vya upinzani aisee yalikuwa ni mambo mabaya sana
Katuga: Jana ulisema mgombea wa CCM hujawahi ona akienguliwa ?
Golugwa: Kabisa kabisa
Katuga: Nani custodian wa wagombea kuenguliwa?
Golugwa: Tume ya Uchaguzi na Chama cha siasa ambacho mgombea ameenguliwa
Katuga: Je taarifa za waaangalizi wa uchaguzi ni sahihi zinatambulika kwa tarehe zilizotolewa?
Golugwa: Ni kweli
Katuga: Je taarifa za waangalizi wa uchaguzi zipo kwenye mitandao ya kijamii?
Golugwa: Zipo kwenye public domain kabisa na kila mtu anaweza kuzisoma
Katuga: Je ulitaja tarehe ya ripoti kutolewa?
Golugwa: Nilitaja mwaka kuwa zilitolewa 2025 mara baada ya uchaguzi mkuu
Katuga: Je ulieleza Mahakama kama Thabo Mbeki Foundation walikuwa observer wa uchaguzi mkuu wa 2025?
Golugwa: Nimesema nilisoma maoni yao kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2025
Katuga: CEO wa Thabo Mbeki Foundation ni nani?
Golugwa: Max Boqwana
Katuga: Ilikuwa na page ngapi?
Golugwa: Page 2
Katuga: Naomba nimuonyeshe shahidi taarifa ya Thabo Mbeki Foundation, anamuonyesha aya ya tatu ili Golugwa asome
Golugwa: Anasoma inarejea pia taarifa ya SADC na AU
Katuga: Kwa mujibu wa hiyo aya, ni wapi wansema wao walikuwa observer wa uchaguzi wa Tanzania??
Golugwa: Kwenye aya ya kwanza na sio hii ya tatu naomba niisome , katuga anamzuia Golugwa asisome, shahidi amekomaa na anaongea kwa ukali sana anasema bwana Katuga sikiliza wewe usinilazimishe nisome aya moja tu, tulia nikuonyeshe waliposema kuwa wao walikuwa observer,
Jaji Ndunguru: Shahidi soma aya ambayo unaona na ni relevant, Katuga anasoma aya ya kwanza ambayo inasema Thabo Mbeki Foundation walisikitishwa sana na maovu yaliyotokea kwenye uchaguzi wa Tanzania wa 2025 na kwa jinsi walivyofatilia
Katuga: Wamekuwa wafatiliaje tena sio waangalizi?
Golugwa: Kazi ya observer ni kufuatilia
Watu kicheko๐๐๐๐๐
Katuga: Jana ulisema Rais alichaguliwa kwa asilimia ngapi?
Golugwa: 98.6 na upinzani ni 2.4
Part 352 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 350
Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia cross examination, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Amani Golugwa
Katuga: Utakuwa hujui aina za vikao vya aina za Chama.
Golugwa: Ukitaka nikuelezee utofauti wa hilo utaelewa.
Katuga: Lakini neno vikao vya Uchaguzi halipo na aina mbili hazipo.
Golugwa: Kwa maana ya maneno hayo hapo hayapo lakini ukitaka kuelewa utaelewa na nitakuelewesha.
Katuga: Umesema kwenye ushahidi wako neno Ushenzi mara nyingi sana. Kwahiyo ni sahihi wewe ni shahidi wa Ushenzi.
Golugwa: Mimi ni shahidi niliyeelezea Ushenzi wa kweli uliofanyika kwenye chaguzi mbalimbali.
Katuga: Mtu atakaetoa hoja specific atalazimika kuithibitisha kwa mujibu wa kifungu cha ushahidi?
Golugwa: Mimi sio mwanasheria.
Katuga: Hivi ulikuwa na wajibu wa kupokea report za kanda zingine?
Golugwa: Niliratibu makatibu wa kanda zingine kujua maendeleo yao na sio kuzipokea.
Katuga: Ulisema Freeman Mbowe alisema hatutakuwa tayari kwenda kwenye uchaguzi mwingine wowote kabla ya mabadiliko ya mifumo ya Uchaguzi?
Golugwa: Alisema ndio.
Katuga: Mbowe alisema hamtakuja kushiriki uchaguzi hadi hayo mabdiliko yafanyike kuna lingine tofauti?
Golugwa: Niliyoyasema unayajua. Ingawa alisema mengi.
Katuga: Maneno kwamba huu uchaguzi tunaenda kuuzuia kwenye maneno ya Mbowe yapo?
Golugwa: Hayapo.
Katuga: Tunaenda kukinukisha. Yapo au hayapo?
Golugwa: Ukitaka neno hilo hilo hutaliona.
Katuga: Shahidi Mwema sasa nisikilize
Golugwa: Mimi mwema kwako. Hakuna wema wowote. Mimi sio shahidi mwema. Una roho mbaya hauwezi kusema mimi ni shahidi mwema.
Katuga: Ni haki ya Kikatiba kushiriki uchaguzi?
Golugwa: Ni haki.
Katuga: Sio haki kumlazimisha mtu pia kushiriki uchaguzi na kumlazimisha ni kosa kisheria?
Golugwa: Sasa kuwa kosa kisheria hapo ndio siwezi kusema.
NB. NAAMBIWA NA WAKILI HAPA KUWA TOKA ASUBUHI HAYA MASWALI YA JAMHURI SIO KESI NI SIASA TU.
Kesi ni Uhaini wa Kuchapisha na Kusambaza na kuitisha Serikali. Huko hatujafika kabisa.
Katuga: Kwahiyo hizi Haki tulikuwa tunazungumzia za Katiba ya Chadema au ipi?
Golugwa: Kwamba ulikuwa hujui tunazungumzia katiba gani? Ni ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katuga: Jana ulisema kuwa wasimamizi wa Uchaguzi walishirikiana na wagombea wa CCM kubadili fomu za wagombea wa chadema, je ulikuwepo au hukuwepo?
Golugwa: Nilikuwepo
Katuga: Jana ulieleza mahakamani kama ulikuwepo ofisi yoyote ya uchaguzi na ukashuhudia msimamizi wa uchaguzi akibadili fomu ya mgombea wa chadema?
Golugwa: sikusema
Katuga: Je ulitaja jina la mtendaji au msimamizi wa uchaguzi aliyekuwa anabadili fomu za wagombea wa chadema?
Golugwa: sikumtaja
Katuga: Halafu unasema mimi nina roho mbaya?
Golugwa: Ni kweli una roho mbaya na sura pia mbaya
Watu kicheko๐๐๐๐๐
Katuga:Jana ulisema kuwa wasimamizi wa uchaguzi walikuwa wanafunga ofisi ili wagombea wa chadema wasipokelewe fomu zao, ulitaja ofisi au jina la msimamizi wa uchaguzi?
Golugwa: Nilitaja matendo yao hao wasimamizi wa uchaguzi
Katuga: Jana ulisema kuwa mawakala wa chadema hawakukuta viapo vyao kwenye vituo vya kupiga kura, na mawakala wa CCM pekee ndio walipewa viapo, uliiambia mahakama wakala fulani wa chadema hakukuta kiapo?
Golugwa: Nilielezea matukio yote kwa ujumla ambayo mawakala wetu mambo ya kishenzi waliyokuwa wanafanyiwa na wasimamizi wa uchaguzi
Katuga: Umesema wewe huna taaluma ya sheria lakini uligusia sheria za uchaguzi?
Golugwa: Nilizigusia
Katuga: Ulizigusia Kanuni zilizotungwa na waziri wa TAMISEMI?
Golugwa: Nilizitaja na nikasema zilitungwa na mkwe
Katuga: Ulitaja mapungufu ya Kanuni hizo?
Golugwa: Sikuainisha moja moja ila nilitaja kwa ujumla
Katuga: Chadema ilishiriki uchaguzi wa 2025?
Golugwa: Haikushiriki
Katuga: Ni sahihi kuwa Chadema haikushiriki kwasababu ya No Reforms No Election
Golugwa: Ni sahihi na huo ndio msimamo wa Mkutano Mkuu mpaka leo
Part 351 itaendele kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 349
Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia cross examination, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Amani Golugwa
Mwinuka: Maudhui ya taarifa yanaweza kuathiriwa na fasili ya mtu.
Golugwa: Yanawezekana. Ukiwa umetafsiri vibaya itakuwa ni vibaya. Na kama ametafsiri vizuri basi ndio itakuwa vizuri.
Mwinuka: Umeeleza chochote kuhusu uwezo wako wa kutafsiri kingereza?
Golugwa: Naweza kutafsiri vizuri tu.
Mwinuka: Title ya ripoti ya Jumuiya ya Madola ikoje?
Golugwa: Nilisema nimeona tamko sio ripoti umesahau tena.
Mwinuka: Kichwa cha habari cha Thabu Mbeki ripoti yake?
Golugwa: Ilisema Ripoti ya Thabu Mbeki kuhusu matukio ya 2025 siwezi kukumbuka neno kwa neno?
Mwinuka: Ripoti ya Afrika Mashariki kuhusu uchaguzi uliangalia?
Golugwa: Sikuangalia hiyo.
Mwinuka: Una imani na ripoti ya Chande?
Golugwa: Sina imani nayo.
Mwinuka: Kwahiyo ulichokieleza kilichopo kwenye ripoti huna imani nacho pia?
Golugwa: Niliyosema kuna mambo nakubaliana nayo lakini sio kukubaliana na ripoti yote.
Mwinuka: Kuhusu sababu za machafuko vipi?
Golugwa: Hata saa mbovu huwa inasema ukweli kwenye kipande cha sababu za Machafuko nakubaliana nayo.
Mwinuka: Kikao cha Tar. 03/04 kwa mujibu wa kikao kile kulikuwa na kinachogusa unyunyu na manukato.
Golugwa: Unyunyu kama neno haikuwepo.
Amemaliza Ignas Mwinuka ameenda Kukaa amemaliza maswali.
Anasimama Ajuaye anasema anafuata Nassoro Katuga.
Katuga: Kuulizwa maswali ya Dodoso ni suala la kisheria na sio roho mbaya ya mawakili wa serikali?
Golugwa: Nakubaliana na wewe lakini wapo mawakili wa Serikali wana roho mbaya wanasingizia watu kesi za uongo. Roho mbaya ipo.
Katuga: Kesi ya Jinai ni ushahidi na sio ushabiki?
Golugwa: Nafahamu.
Katuga: Kuna taarifa zako ziko kwenye public domain?
Golugwa: Nilisema ugomvi wangu na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha. Nimesema hilo.
Katuga: Taarifa zako na waandishi ziko kwenye Public Domain?
Golugwa: Zipo.
Katuga: Wewe ni mjumbe wa Kamati kuu ya Chadema?
Golugwa: Ndio toka January 22, 2025.
Katuga: Tar. 29/08/2025 Kamati Kuu iliketi kujadili mambo mbalimbali.
Golugwa: Iliketi lakini sio kujadili mambo mbalimbali.
Katuga: Ulitangaza maazimio ya Kamati Kuu?
Golugwa: Ni kweli
Katuga: Hiyo taarifa ipo kwenye public domain?
Golugwa: Ni kweli
Katuga: Miongoni mwa vitu ulivyotangaza ni kuhusiana na kesi hii?
Golugwa: Kweli
Katuga: Ulisema mmekusudia kumtetea mheshimiwa mwenyekiti wa Chama?
Golugwa: Tulisema viongozi waelekeze nguvu zao hapa wasifanye mambo mengine. Tumtetee Mwenyekiti.
Katuga: Kwahiyo umeleekeza nguvu kumtetea?
Golugwa: Nguvu nyingi kabisa.
Katuga: Kuteuliwa na kuchaguliwa utofauti?
Golugwa: Kuchaguliwa kuna mchakato lakini kuteuliwa anakuteua.
Katuga: Katibu Mkuu wa Chama wa sasa anaitwa nani?
Golugwa: Anaitwa John Mnyika na ameteuliwa na Mwenyekiti?
Katuga: Akitokea mtu akisema aliteuliwa na kuidhinishwa je na Kamati Kuu?
Golugwa: Hatakuwa sahihi.
Nb. Viongozi Wakuu wa Chadema hawaidhinishwi na Kamati kuu.
Katuga: Kuwa Muhasibu tangu 2001 na kufanya kazi za kihasibu toka 2001 kuna utofauti? Si umesema kuna mawakili wa serikali wana roho mbaya.
Golugwa: Wewe kweli kabisa roho mbaya unayo. Ni kweli kabisa.
Katuga: Ulichukua minutes za kikao cha Tar. 03/04?
Golugwa: Kile hakikuwa kikao cha kuandika minutes.
Katuga: Aina za vikao?
Golugwa: Kuna vikao vya uchaguzi na vikao vya kawaida.
Katuga: Vikao vya ndani na hadhara akitokea mtu akisema ni aina ya vikao vya Chadema kama ilivyo vikao uchaguzi na kawaida atakuwa sahihi?
Golugwa: Yuko sahihi. Ni vikao vyote vya Chadema.
Katuga: Ulisema hukumbuki kwamba vikao viko sura ya ngapi ya Katiba?
Golugwa: Sahihi niletewe nitaisoma nione.
Katuga: Kutakuwa na vikao vya aina nne kwa mujibu wa Katiba Soma?
Golugwa: Vikao vya aina nne na vinahitaji maelezo
Part 350 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
@barakawamb Mi naona Ww hakuna kitu ufafahafu zaidi ya kusoma na kuandika!Tanzania ina sheria zake lakini kama yalivo mataifa mengind iko subjected na mikaba,kanuni na sheria za jumuia ambako ni mwanachama na pia mikataba mbalimbali ya haki za bnadamu
#TANZANIA: MIMI SIO MUOGA, WENYE HATIA HUWAGA WAOGA - LISSU
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu anayekabiliwa na mashitaka ya uhaini leo Septemba 03, 2026 amesema yeye sio muoga, na kuongezea kusema kuwa watu wenye hatia ndio huwa waoga, "mimi sio muoga, siku zote watu wenye hatia ndio huwa waoga"
Zaidi: https://t.co/sFvpN0JFRu
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 347
Mhe. Lissu anaendelea kumuongoza Shahidi wake ambae ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA upande wa Tanganyika Amani Golugwa.
Mhe. Lissu: Katika Matukio yote ya mimi kukamatwa uliyoyasema, waeleze majaji kumbukumbu zako za mimi kutiwa hatiani kwa kosa lolote nililowahi kukamatwa nalo
Golugwa: sina kumbukumbu yoyote ya wewe kutiwa hatiani kwa matukio yote uliyokamatwa wala kushtakiwa nayo
Mhe, Lissu: Umenifahamu kwa muda gani?
Golugwa: Nimekufahamu kwa miaka 20
Mhe. Lissu: leo nashtakiwa kwa uhaini, kosa kubwa kuliko yote nchi hii, waeleze majaji kwa ufahamu wako uwezekano wa mimi kuwa mhanini kwenye nchi yangu
Golugwa: Waheshimiwa majaji kwa namna ambavyo namfahamu Lissu kwa hiyo miaka 20, ni mtu mwema sana na sioni uwezekano wa Tundu Lissu kuwa mhaini
Hapa shahidi ametiririka sana mpaka Majaji wamefurahi. Jaji Nduguru amesema CV yake Lissu ameshaitoa hapa Mahakamani.
Watu wamefurahi sana hizi dakika za jiooooni kabisa.
Mhe. Lissu: Kwa shahidi huyu nimemaliza maswali
Wakili wa Serikali Ajuaye amesimama anasema hivi sasa ni saa kumi na moja kamili na kwa vile muda umeisha tunaomba ahirisho hadi kesho saa tatu kamili asubuhi kwaajili ya maswali ya Dodoso kwa shahidi huyu.
Jaji Nduguru: Shauri linaahirishwa hadi kesho saa tatu kamili asubuhi.
Inapigwa High Coouuuuuurt
Majaji wanatoka nje.
Mhe. Lissu anapack makablasha yake huku akiagana na Viongozi, Wanachama na Wafuasi wa CHADEMA waliokuja Mahakamani siku ya Leo.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 346
Mhe. Lissu anaendelea kumuongoza Shahidi wake ambae ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA upande wa Tanganyika Amani Golugwa.
Mhe. Lissu: Wakili wa Serikali Katuga anapenda kutoa mifano ya hovyo kabisa yani, kama shahidi alioa na akaingiliwa na Polisi ni ushahidi unaohusiana na kesi. Ushahidi wangu na ushahidi wa Mnyika unahusu kampeni ya uonevu wa Serikali dhidi yetu na Chama chetu. Kesi hii ni ya uonevu, ni ya uongo ni ya kisiasa na Serikali wamekuwa wanakamata watu na Viongozi wetu bila kufuata sheria, bila kuwafungulia mashtaka kwa nia ya kudhoofisha Chama chetu. Kifungu sahihi ni cha 7 , 8 , 9 cha Sheria ya Ushahidi. Hawa mawakili wa Serikali hawataki Jeshi la Polisi la Serikali wanayoitumikia liwe exposed, uchafu wao wanaoufanya kunyanyasa watu hawataki uwe exposed, sisi hatutakubali maana tumenyanyaswa sana mimi binafsi, Mbowe, Mnyika, Dr. Slaa na viongozi wengine.
Katuga: Anachokisema Lissu ndio maana ya kukinukisha sasa ; sisi tunaomba maelekezo ya Mahakama ila kama ushahidi huo ni wa muhimu kwa upande wa utetezi hatuna shida kwasababu tutapata nafasi ya kuuliza maswali ya dodoso.
Jaji Ndunguru anashauriana na majaji wenzake ameanza na Jaji Kareyamaha leo, kaenda kwa Jaji Kiwonde ngoja tuona, ila wamechukua dakika nyingi sana ni zaidi ya 10.
Jaji Nduguru baada ya majadiliano ya muda mrefu anasema tumesikia hizo hoja, tunaelekeza tuwe focused, wajibu wa prosecution ni kuthibitisha kesi, Mshtakiwa hana wajibu wa kuthibitisha utakatifu wake, shida ni kwamba upande wa utetezi huwa hawana statement kwamba labda ina guide upande wa utetezi. Jamhuri mna haki ya kufanya cross examination na hiyo ndio fair trial.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji tukio jingine la kukamatwa kwako.
Golugwa: Tarehe 08/11/2025 nikiwa nyumbani kwa wazazi wangu Arusha nilikamatwa na Polisi na nilipohoji kwanini wananikamata wakanitajia makosa matatu: ugaidi, kula njama ya kuharibu miundombinu ya umma na mali ya umma, kula njama ya kuwapiga askari wa vyombo vya dola, eti mimi huyu nipange kupiga askari? Shahidi anaongea kwa hisia na kujiuliza swali
Mhe. Lissu: Nini kilitokea baada ya hapo?
Golugwa: Nilikaa Central Police Arusha kama masaa mawili na baadae nilisafirishwa hadi Oysterbay Police Dar es Salaam majira ya saa moja usiku, nilikataa kutoa maelezo hivyo niliwekwa lock up. Ilipofika saa nane usiku tena nilitolewa nikaambiwa kutoa maelezo, sikutoa maelezo na niliwaambia aje ZCO Mafwele ambaye nimefahamiana nae akiwa Arusha aje aseme kwa anavyonifaham kama mimi huyu Golugwa ninaweza kuwa gaidi.
Waheshimiwa Majaji kesho yake ZCO Mafwele alikuja akanishawishi nitoe maelezo na wakili Hekima alikuja nae akanishawishi nitoe maelezo, sikutoa maelezo na niliowaona na wenzangu hapo Lema, Boni Yai na John Heche. Tuliambiwa nendeni na kesho yake tulitakiwa kwenda kwa ZCO Mafwele Central Police station na baada ya kuripoti tuliambiwa nendeni na ikawa hivyo hadi leo
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji hatua gani Jeshi la Polisi limeshachukua hadi leo
Golugwa: hakuna hatua yoyote mpaka leo
Mhe. Lissu: Waeleze majaji hii kamatakamata inamaanisha nini kwako
Golugwa: nia yake ilikuwa kunitisha mimi na viongozi wenzangu ili tusifanye kazi yetu ya chama.
Mhe. Lissu: Waeleze ufahamu wako kuhusu matukio ya mimi kukamatwa ukichilia tukio hili lililoniweka gerezani
Golugwa: Mwaka 2012 nakumbuka tulikamatwa wote na kumwagiwa maji ya washawasha na kipigo Arusha, nakumbuka mwaka 2024 tulikamatwa Mbeya ulipoenda kwenye Maadhimisho ya siku ya vijana, tukio jingine lilitokea Arusha ulipokuja kumtetea Lema nakumbuka ulikamatwa, ulipotoa maoni yako kuhusu utawala wa Magufuli pia ulikamatwa uliposema Magufuli ni Dikteta Uchwara.
Part 347 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 345
Mhe. Lissu anaendelea kumuongoza Shahidi wake ambae ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA upande wa Tanganyika Amani Golugwa.
Mhe. Lissu: Shahidi endelea kuhusu kilichokutokea 13/05/2025
Golugwa: Tarehe 13/05/2025 nilipokuwa Airport wakati tayari nimeshapewa boarding pass, nikiwa kwa afisa uhamiaji nilifuatwa na watu wawili wakasema twende ofsiini tuzungumze, wakati tunaelekea ofsini kwenye kibaraza walisema niko chini ya ulinzi, mmoja hakuwa na kitambulisho na alikuwa amevaa nguo za kiraia ndio alisema niko chini ya ulinzi, waliniingiza kwenye chumba na kuniacha. Kabla ya hapo walitaka simu zangu na huyu ambaye hakuwa na unifomu wala kitambulisho alizichukua zote.
Waheshimiwa majaji baada ya dakika kama 5 nikiwa kwenye chumba walikuja watu zaidi ya watano mmoja akiwa na bunduki, walifungua mlango wakapekua begi langu na wakachukua karasi mbili ambazo zilikuwa na hotuba ambayo nilipanga kwenda kuzungumza kule kwenye mkutano.
Waheshimiwa majaji pamoja na kwamba niliwauliza kwanini wamenikamata, kwanini wananipekua, kosa langu nini? Hawakunijibu kabisa, walinishusha underground pale airport , mwendo ulikuwa wa kasi sana, walinitukana sana โnaomba nisiyaseme maneno haya mbele ya mahakama tukufuโ mmoja aoiyekuwa na bunduki aliniwekea kwenye sikio la kulia na akasema โnyie wajinga ndio mnapanga safari zenu kwenda kuichafua nchi huko nje, sasa leo ndio utaelewaโ. Sikupigwa ila nililazimishwa kutembea , naomba majaji mniangalie niwaonyeshe
Amani Golugwa anawaonyesha Majaji jinsi alivyoningโinizwa kwa kushikwa maeneo ya maungoni miguu ikawa haifiki chini ameonyesha kwa umaridadi kabisa
Waheshimiwa majaji baada ya hapo niliingizwa kwenye gari nikazungushwa kwa zaidi ya masaa mawili Airport na baadae nikapelekwa Stakishari Police station, niliwahoji kwanini mnanileta huku? Wakasema wewe ndio Lissu huwa anakutuma kwenda kuisema serikali huko nje na kupewa hela chafu kutoka nje hivyo wewe cybercrimes inakuhusu na money laundering.
Golugwa anaendelea kusema ilipofika saa nane usiku watu 10 walikuja kunichukua na walikuwa wote wapya nikawauliza mnanipeleka wapi wakawa hawajui na wakawa wananishangaa, walikuwa na radio call wakawa wanaongea wanasema tuko na mwewe, tulielekea kushoto kutoka Stakishari mimi nikiwa nimelala chini kwenye gari, baada ya muda tulifika Central Police Station Dar es Salaam na yule aliyekuwa anaongea na radio call akamwambia ZCO Mafwele kuwa mzigo huo.
Waheshimiwa majaji sikuwa sawa wakati huo kutokana na magumu niliyopitia na ZCO aliniongelesha kwa lugha nzuri ingawa mimi nilikuwa katika hali ngumu sana maana nilikuwa sielewi hatima yangu na nilipofikishwa tu wakasema cybercrimes na money laundering.
Waheshimiwa majaji niliulizwa kuhusu safari zangu mbili za huko nyuma za Mombasa na waliniambia kuwa nimekuwa nasafiri na kurudi bila kufuata taratibu na sheria za nchi, walinitaka nitoe maelezo, nilihoji sana na sikuwa tayari kutoa maelezo lakini mwishoni nilitoa maelezo na nikatakiwa nilete uthibitisho wa safari ya Mombasa ambayo nilisafiri na familia na wazazi wangu na nilipeleka uthibitisho kwa kupeleka nakala za passpoti.
Mhe. Lissu: mambo yote haya yaliishia wapi?
Golugwa: nilidhaminiwa na viongozi wa chama na nikaambiwa nenda nyumbani kwa amani. Hivyo safari ya kikazi ilivurugika na sikufanikiwa kusafiri.
Mhe. Lissu: waeleze kuhusu ukweli wa tuhuma hizo kama ni kweli au sio kweli
Golugwa; tuhuma hizo sio za kweli
Mhe. Lissu: waeleze majaji kama kuna sheria inazuia wewe kusafiri kwenda nje ya Nchi
Golugwa: Hakuna sheria
Part 346 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 344
Mahakama Imerejea
Inapigwa High Coooouuurt
Majaji wanaingia Mahakamani
Wakili wa Serikali Ajuaye anasimama anasema mawakili wa Serikali tuko vilevile
Jaji Nduguru anamuuliza Mhe. Lissu uko tayari?
Mhe. Lissu: Niko niko tayari
Jaji Nduguru twendelee
Mhe. Lissu: Wakati tumenda Break ulikuwa unaelezea kuhusu hotuba ya 3/4/2025 naomba uendelee
Golugwa: Mwenyekiti Tundu Lissu alielezea pia matukio ya mauaji katika chaguzi za nchi yetu mfano wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 Mgombea wa Chadema aliuwawa kwa kupigwa risasi , mwingine wakati wa marudio ya uchaguzi mdogo kinondoni,
Mhe. Lissu: Baada ya kuelezea mauaji katika chaguzi zetu nilisema nini?
Golugwa: Ulisema kuliko kupitia mabalaa haya yote, ya watu kuuwawa kwenye chaguzi, vurugu na fujo tupo tayari uchaguzi uahirishwe na usogezwe mbele ili kama taifa tuweze kushughulikia matatizo haya yaliyopo kwenye mifumo yetu ya uchaguzi. Tundu Lissu pia alisema tunamaanisha, tupo tayari na sheria zetu zinaruhusu uchaguzi kusogezwa mbele.
Mhe. Lissu: Jambo lingine nililolizungumzia naomba endelea kuelezea
Golugwa: Jambo lingine Mhe. Lissu alisema ambaye anawaza kugombea uchaguzi huu asahau, aende akafanye kazi ya kuwaelimisha wapiga kura wake juu ya msimamo wetu wa No Reforms No Election ili watanzania wote watuunge mkono. Jambo lingine Mhe. Lissu alisema hata yeye alikuwa anafikiria kugombea Urais ila hatagombea na kuwa upo tayari uchaguzi usogezwe mbele na utakwenda kuwaelimisha watanzania nchi nzima
Mhe. Lissu: Kwa mazungumzo yangu yote ya siku hiyo ambayo umeyasema hapa, mtu akikuletea maneno machache ambayo yapo kwenye hati ya mashtaka wewe unasemaje?
Golugwa: Mimi naona kabisa ni ya kutengeneza na yana nia ovu dhid yako, nia ya kukuonea wewe na chama chetu ili tusifanye siasa tunazoruhusiwa kisheria.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kwa ufahamu wako maneno ya hotuba yangu yote kama kulikuwa na uwepo wa nia ya kutenda uhaini
Golugwa: Kwa ufaham wangu hakuna nia kabisa ya uhaini au kuitishia serikali
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kwa kumbukumbu zako hayo maneno niliyozungumza 3/4/2025 kama ilikuwa ni mara yako ya kwanza kuyasikia
Golugwa: Kwa kweli umeshayasema mara nyingi sana ikiwemo Mkutano na wahariri wa vyombo vya habari ulioongozwa na Deodatus Balile y wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ulisema pia ulipokutana na viongozi wa dini ya kiislamu Shura ya Maimamu mbele ya kiongozi Shikhe Ponda Issa Ponda, na mimi nilikuwepo na nilisikia maneno hayo ukiyasema.
Golugwa anaendelea kusema kuwa Mhe. Lissu pia ulisema maneno hayo tulipokutana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadmau mbele ya wakili Fulgence Massawe, nilikuwepo na uliyasema. Vilevile uliyasema mbele ya Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba ofisini kwake Masaki na uliyasema maneno hayo nilikuwepo na niliyasikia na Mzee Warioba alituunga mkono kabisa
Mhe.Lissu: Waeleze majaji hizo ziara zote na kusema maneno yote hayo, je nilikuwa nasambaza nia ya kutenda uhaini?
Golugwa: haikuwa kusambaza uhaini ila ilikuwa ni kuwaelimisha msimamo wetu ili watuunge mkono ili mabadiliko yatokee kabla ya uchaguzi kufanyika , wote walituelewa isipokuwa Serikali
Mhe.Lissu: Baada ya tarehe 09/4/2025 mimi kukamatwa, waeleze majaji mambo gani yalitokea kwa chama na nyie viongozi mliobakia
Golugwa: Chama kilifunguliwa kesi na kuzuiwa kufanya kazi za chama, viongozi tulikamatwa na kutuhumiwa kwa makosa ya kubambikiza kama ugaidi n.k
Mhe. Lissu: wewe kilikutokea nini binafsi?
Golugwa: Tarehe 13/05/2025 nilikuwa na safari ya kwenda Ubeligiji kukiwakilisha chama kwenye mkutano wa vyama vya kidemokrasia duniani (IDU)
Katuga anasimama: Mhe Jaji shahidi anachosema ni kinyume cha kifungu cha 156 cha Sheria ya Ushahidi kwasababu hauhusiani na kesi, shahidi atakuja pengine kutoa mifano kama alioa au hakuoa
Part 345 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo September 3, 2026
Last time tuliishia part 337 so leo tunaendelea na -;
Part 338.
Majaji wanaingia.
Mheshimiwa Lissu nae ameingia.
Ajuaye Zengeli anawatambulisha mawakili wa Serikali na Jaji anasema Shahidi apande kizimbani.
Shahidi Amani Sam Golugwa anapanda kizimbani.
Majaji wanateta na kusikilizana pale juu. Shahidi kiapo chako kinaendelea.
Golugwa: Sawa Ahsante anatikisa na kichwa kukubali.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kwa ufahamu wako taarifa ya watazamaji wa SADC ilisemaje kuhusu huo uchaguzi?
Golugwa: Uchaguzi wa Tanzania haujakidhi vigezo vya chaguzi za kidemokrasia. Pia kulikuwa na vitisho na uonevu kwa viongozi wa vyama vya upinzani kwahiyo mazingira ya kiushindani hayakuwa sawa. Na tatu, hakukuwa na uwazi katika mchakato mzima wa Uchaguzi. Nne, kulikuwa na udanganyifu katika mchakato wa uchaguzi, vurugu siku ya uchaguzi na hivyo uchaguzi wa Tanzania umekosa uhalali wa kuitwa uchaguzi.
Mhe. Lissu: Watazamaji wa Jumuiya ya Ulaya (EU) walisemaje kuhusu uchaguzi huo?
Golugwa: Walisema wamesikitishwa na matukio ya vurugu yaliyotokea, kuuwawa kwa watu walisikitishwa nako sana. Uchaguzi wa Tanzania uligubikwa na watu kutekwa kabla ya uchaguzi, kupotezwa na mazingira ya uchaguzi hayakuwa yenye ushindani ulio sawa. Na mazingira yalionekana kupendelea Chama cha Mapinduzi. Na mwisho kutokana na udanganyifu na vurugu zilizotokea uchaguzi wa Tanzania waliona haukuwa huru na haukuwa na uwazi.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji watizamaji wa jumuiya ya madola (Common wealth) walisemaje?
Golugwa: Niliona kauli ya Katibu wa Jumuiya ya Madola niliyoisoma alisema amesikitishwa na amehuzunishwa kwa vurugu na kauli zilizotokea na mauaji yaliyotokea na hivyo jumuiya ya madola itafuatilia kwa karibu kuhusu tukio hili.
Mhe. Lissu: Matokeo ya Uchaguzi wa mwaka jana yakikuwaje ya U Rais?
Golugwa: Mgombea wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi alitangazwa amepata kura Milioni 31.6 na asilimia 98.6 na wagombea wengine kwa ujumla waligawana kipande kidogo kilichobaki yaani 2.4.
Mhe. Lissu: Ya ubunge yalikuwaje
Golugwa: Sifahamu
Mhe. Lissu: Udiwani yalikuwaje?
Golugwa: Sifahamu
Mhe.Lissu: Thabu Mbeki Fiundation walisemaje kuhusu matokeo ya Uchaguzi huo wa Tanzania?
Golugwa: Thabu Mbeki foundation walisema mambo manne.
1. Uchaguzi wa Tanzania uko chini ya viwango na miongozo ya chaguzi za Kidemokrasia kama zilivyowekwa kwa mujibu wa SADC na umoja wa Afrika.
2. Wapiga kura hawakupata uhuru wao wa kidemokrasia wa kupiga kura kwasababu ya vurugu zilizokuwa zimetokea.
3. Matokeo ya Urais na Ubunge yaliyotangazwa sio ya kweli na hayana uhalisi wa utashi wa watu kwenda kupiga kura.
4. Tanzania hakuna serikali yenye uhalali na hii iliyopo imejiweka kwa kutumia mabavu na udanganyifu kupitia uchaguzi usiokuwa halali.
Mhe. Lissu: Sasa shahidi katika watizamaji wote hao uliowataja. Waeleze majaji kwa ujumla wao walizungumziaje matukio ya mauaji ya wananchi kwenye uchaguzi huo?
Golugwa: Kwa ujumla wake waangalizi walisema vyombo vya dola kwa maana ya askari Polisi waliwapiga risasi waandamanaji na waliwazuia waangalizi kutimiza wajibu wao kwa kuwapiga na kuwanyang'anya vifaa vyao.
Mhe. Lissu: Kuhusu mauaji ya wananchi ndio swali langu?
Golugwa: Walisema vyombo vya dola wamehusika katika mauaji ya waandamanaji na hivyo walitaka kuwepo na uwajibikaji kwa waliohusika na masuala hayo.
Mhe. Lissu: Huu uchaguzi ulisimamiwa na kuendeshwa na chombo kinachoitwaje?
Golugwa: Chombo kinachoitwa Tume Huru ya Uchaguzi.
Mhe. Lissu: Viongozi wa hiyo tume wanapatikanaje?
Golugwa: Waheshimiwa Majaji wanapatikana kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhe. Lissu: Mkurugenzi je wa hiyo tume anapatikanaje?
Golugwa: Anateuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.?
Part 339 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
@TanzaniaAnalyst Hivi huwa unafeed ubongo wako au ni tumbo tuu?Kama ni ujasririamali basi washauri hao wanaokulipa ww wakate mirija kwa kuondoa hii kesi inayowaaibisha nahakamani.