@Elsukay0 Nyie wapwa ndio mmetunuku, ila amini nakwambia bado ujajuana na pisi za X mzee, kuna pisi huku hatari halikisha kwenye circle yako kila siku unafolow watu tofauti, fl wachungaji,vijana wa hovyo, maskini wa humu, matajiri wa humu na uhakikishe una engage nao mzee utakutana na pisi
AFRICA UNITED: (AFRICA IKIUNGABA).itakuwaje hivi bara la africa likiungana na kuwa sauti moja?
๐:THREAD (UZI)
1/.Bara la africa ni moja ya mabara tajiri duniani lenye jumla ya nchi 54 likiwa na ukubwa wa kilometers za mraba milion 30.3 , ukubwa huu ni sawa na 20% ya eneo la nchi kavu duniani, linalofanya bara hili kuwa bara la pili kwa ukubwa duniani baada ya bara la Asia, najaribu kufikiria siku ambayo nchi za africa zitaungana na kuweka kando mipaka na kuanza kufanya kazi kama umoja wa kiuchumi pamoja na kisiasa kwa kuzingatia usalama wake.
2/. Bara la africa lina idadi kubwa ya watu kwa kukadiriwa kuwa 1.4bilion, hii inaweza kuwa ishara kubwa kwa nchi za kiafrika kuwa africa ingekuwa moja ya masoko makubwa zaidi duniani .
3/.Biashara kati ya nchi zingekuwa rahisi sana, mfanyabiashara kutoka Dar es salaam, au kutoka Nairobi, au kutoka Entebe ingekuwa rahisi kufanya biashara Lagos, Johannesburg , Cairo, Dakar, Nk bila kuwa na vikwazo vikubwa ,
4/. Bara la africa lingekuwa na mfumo mmoja wa kifedha au kuwa na ushirikiano imara wa sarafu, nafikiri ingepunguza utegemezi wa sarafu nje na kuimarisha biashara ya ndani.
5/. Bara la africa lina Dhahabu nyingi, mafuta, madini ya lithiam, almasi, misitu mikubwa, na ardhi yenye rotuba,nk, hii ingesaidia africa kuwa na nguvu kubwa mno kwenye mazungumzo muhimu kwenye maswala ya kimataifa na ingechochea ushindani mkubwa wa kutambiana na mataifa mengine makubwa kama USA, CHINA, NA mataifa mengine ya umoja wa ulaya.
6/.Bara la africa lingetokea likaungana , lingeweza kujadiliana kwa usawa na mataifa makubwa kama China, marekani, na umoja wa ulaya badala ya kila nchi kujadiliana kivyake.
7/.Bara la Africa likitokea kikaungana Usalama ungeimarika kupitia mfumo mmoja wa ulinzi na kupunguza mogogoro ya ndani pamoja na uingiliaji wa nje.
8/. Bara la Africa likitokea likaungana, miradi mikubwa ya miundombinu kama reli, barabara ya nishati, ingeunganisha bara zima kwa urahisi zaidi, hivyo ingeweza kuchochea shughuli za kiuchumi kukuwa maradufu.
NB: Pamoja na Bara hili kungana ๐
9/.Bado umoja huo ungekutana na changamoto nyingi kama tofauti ya mifumo ya uongozi , rushwa, siasa pamoja na lugha.
10/.Licha ya changamoto hizo, Wazo la Africa kuungana bado lina nguvu na nguvu hiyo tumeziona kulingana na ufafanuzi yakinifu kwenye kipande cha 1 na 5 cha mchambuzi wako Diplomat Kilesi,hivyo nguvu tayari tunayo kilichobaki ni utayari na umoja wa kuifungua.
Back to you mwana africa, wewe unaonaje, Africa inaweza kuungana kweli katika maisha yetu?.