WAMASAI, WAHADZABE, WADATOGA NA WAIRAQW WANAPOKUTANISHWA NA URITHI WA DUNIA
Maadhimisho ya siku ya Urithi wa Dunia Afrika yaliyofanyika katika Makumbusho ya Urithi Jiopaki mjini Karatu tarehe 5 Mei, 2026 yameyakutanisha makabila makuu manne yanayounda Jiopaki ya Ngorongoro Lengai ambayo ni wamasai, wahadzabe, wairaqw na wadatoga na hivyo kuunganisha kutaniko kubwa la urithi wa dunia katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Dkt Lameck Karanga amesema uwepo wa makabila hayo, historia yao pamoja na kuenzi tamaduni zao ni utajiri mkubwa kwa Tanzania na kutoa wito kwa wadau na jamii kwa ujumla kuendelea kulinda maeneo ya urithi wa dunia na kuibua maeneo mapya yatakayoingizwa katika orodha ya Urithi wa Dunia ili kuongeza thamani ya ubora wa kipekee ulimwenguni (Outstanding Universal Value) na kuvutia wageni wengi zaidi.
Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Utalii na Maendeleo ya Jamii Ngorongoro Joas Makwati ameeleza kuwa mamlaka itaendelea kuongeza juhudi za kulihifadhi eneo la Ngorongoro ambalo ni urithi wa dunia na kultangazia zaidi kama eneo pekee lenye Ushahidi wa kisayansi kuhusu historia ya binadamu unaoeleza kuwa binadamu kwa kuthibitishwa na ugunduzi wa masalia ya binadamu wa kale na zana za mawe zilizopatikana katika bonde la Olduvai.
Kwa upande wake Naibu Katibu wa Tume ya Taifa ya UNESCO Tanzania Dkt. Khamis Said ameeleza kuwa tangu Tanzania ijiunge na UNESCO imepata mafanikio mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuridhia mikataba kumi (10) ya UNESCO,Kuwepo kwa Hifadhi Hai za Mwanadamu na Mazingira sita (6) na Kuwepo kwa maeneo saba (7) ya urithi wa Dunia.
Kauli mbiu ya siku ya urithi wa dunia kwa mwaka huu ni “Kusherekea siku ya Urithi wa Dunia na kukuza Viongozi wa baadaye”. (Celebrating Africa’s Heritage, Mentoring the Leaders of Tomorrow).
Tanzania’s Parliamentary Standing Committee on Lands, Natural Resources and Tourism has commended Dr. Agnes Gidna after her detailed presentation on archaeology, geology and human origins at the Ngorongoro Geopark Museum, as Parliament urged the government to promote the site as a tourism and education hub. @SuluhuSamia@UNESCO@bunge_tz@AGidna READ MORE: https://t.co/bhQtvKaomF
Wahadhiri na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) tarehe 21 Novemba, 2025 wamefanya ziara maalumu ya mafunzo katika Makumbusho ya Jiopaki ya Ngorongoro Lengai iliyopo Karatu Mkoani Arusha ili kuongeza uelewa wa wanafunzi kuhusu masuala ya akiolojia, utamaduni, Jiografia, jiolojia pamoja na historia ya sayansi na mazingira.
Wakiwa katika makumbusho hiyo wanafunzi walikutana na wataalam wa fani mbalimbali na kupata elimu kuhusu jiopaki ya Ngorongoro, elimu ya miamba, sayansi na mazingira, tamaduni za makabila yaliyopo jirani na hifadhi ya Ngorongoro pamoja na vivutio vinavyopatikana katika hifadhi hiyo.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha SUZA na mkuu wa Msafara huo Dkt. Abdallah Mkumbukwa amesema ziara hiyo ni darasa kubwa kwa wanafunzi wa SUZA hasa kuunganisha masomo waliyosoma kwa nadharia kuwa ya vitendo kwa uhalisia wa kisayansi na kimazingira na kuita makumbusho hiyo kuwa ni kisima cha elimu ya miamba, jiolojia na utamaduni.
“Tumepata maarifa mengi mapya na ya kisasa kupitia makumbusho ya jiopaki ya Ngorongoro Lengai, wanafunzi wetu wameelimika masuala mbalimbali kuhusu muonekano wa dunia kwa miaka mingi iliyopita na ilivyo sasa, maumbile asilia yanayopatikana katika ukanda wa bonde la ufa, mwamba wenye umri wa miaka milioni tatu iliyopita unaopatikana hifadhi ya Jiolojia ya Ngorongoro-Lengai na tamaduni za makabila ya Wahadzabe, Wairaqw, Wadatoga na Wamasai ambayo yote unayapata hapa" aliongeza Dkt. Mkumbukwa
Msimamizi wa Makumbusho ya Jiopaki ya Ngorongoro Lengai, Afisa Uhifadhi Mkuu Dkt. Agness Gidna amesema tangu makumbusho hiyo kufunguliwa mwezi Oktoba, 2025 imeendelea kuvutia wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ambao wanakuja kutalii na kujifunza masuala ya Jiolojia, akiolojia na urithi wa utamaduni wa makabila mbalimbali kupitia maonesho na taarifa zilizowekwa katika Makumbusho hiyo. @visitngorongoro@VisitTanzania1@MNRT_Tanzania@TTBTanzania
So delighted to witness the handover ceremony of the China-Aided Project of Ngorongoro-Lengai Geopark with H.E. Dr. Philip Mpango, Vice President of Tanzania. This project is the first China-Aided cultural and tourism project, constructed by China Raiway 25th Bureau Group. Wish TZ’s tourism industry will achieve greater development!
A new chapter in Tanzania’s heritage has been written under the wide skies of Karatu. On this historic day, the Vice President of the United Republic of Tanzania, H.E Dr. Philip Isdor Mpango, officially inaugurated the Urithi Geo-Museum, a modern sanctuary dedicated to celebrating and preserving the geological and cultural legacy of the Ngorongoro-Lengai UNESCO Global Geopark. This landmark institution is the first of its kind in Sub-Saharan Africa and a profound reminder that Tanzania’s story is deeply rooted in the very earth beneath our feet.
#urithigeomuseum #ngorongorolengaiglobalgeopark
DKT.MPANGO AZINDUA MAKUMBUSHO YA KISASA YA URITHi WA JIOLOJIA.
Na Mwandishi wetu, Karatu Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango, leo tarehe 16, 2025, amezindua Makumbusho ya kisasa ya Jiolojia ya Ngorongoro-Lengai (Urithi Geo Museum) baada ya mradi huo kukabidhwa na Serikali ya China kwa Serikali ya Tanzania katika eneo la Karatu mkoani Arusha.
Mradi huo uliogharimu shilingi Bilioni 32 ni msaada kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ambao ulilenga kuboresha miundombinu ya utalii, ujenzi wa makumbusho ya kisasa ya jiolojia na kuendeleza shughuli za uhifadhi katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro na maeneo mengine ya hifadhi ya jiolojia ya Ngorongoro-Lengai (Ngorongoro-Lengai Geopark Development Project)
Akifungua makumbusho hiyo Dkt. Mpango ameeleza kuwa Tanzania kupitia eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ilipewa hadhi ya kuwa eneo lenye utalii wa Miamba “Geopark” mwaka 2018 na kuwa Geopark Pekee katika nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara na ya Pili kwa Afrika na kusisitiza kuwa kukamilika kwa makumbusho hiyo kutavutia wageni kutembelea na kupata taarifa za Jiolojia.
Dkt. Mpango, amesisitiza kuwa uendeshaji wa mradi wa makushusho hiyo mpya uende sambamba nakutoa mafunzo kwa watumishi watakaohudumia wageni wanaotembelea makumbusho hiyo, kutunza na kuboresha miundombinu, kusaidia na kushirikisha Jamii inayozunguka eneo la Hifadhi ya Ngorongoro na kusisitiza watanzania kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii ambavyo ni hazina ya nchi.
Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian, amesema mradi huo ambao ni wa aina yake barani Afrika chini ya mpango wa “Belt and Road Initiative”, unadhihirisha ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Tanzania ulioanza tangu mwaka 1964.
Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana, amesema eneo la Ngorongoro pamoja na kuwa na hadhi ya Jiopaki pia limeshinda tuzo ya kuwa kivutio cha utalii Barani Afrika mwaka 2023 na 2025 kupitia mtandao wa World Travel Awards.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Venance Mabeyo ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuboresha miundo mbinu ya hifadhi ya Ngorongoro na kusema makumbusho ya Urithi ni moja ya kazi kubwa ya serikali katika kuendeleza mazao mapya ya utalii.
🚨 New paper out!
We present new stratigraphy and OSL dating from the Ndutu and Naisiusiu type sites at Olduvai Gorge (Tanzania), shedding light on the Middle and Later Stone Age occupations in the region:
📄 https://t.co/46meiwtgGe
A (very) brief thread👇
📍Dar es Salaam
▪️RAIS WA FINLAND ATEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA
Rais wa Jamhuri ya Finland, Mhe. Alexander Stubb, ametembelea Makumbusho ya Taifa la Tanzania jijini Dar es Salaam na kuonesha kufurahishwa na maonesho ya historia ya mwanadamu yaliyopo katika jumba hilo la kihistoria.
Akizungumza katika ziara hiyo leo, Mei 15, 2025, Rais Stubb amesema kuwa amepata fursa ya kujionea historia ya mwanadamu, jambo lililomgusa sana na kumpa uelewa wa kina kuhusu asili ya binadamu.
"Nimejionea historia ya mwanadamu, sasa najua tulikotoka," alisema Rais Stubb huku akisisitiza kuwa mashirikiano ya kihistoria kati ya Tanzania na Finland yalianza tangu nchi hizo zilipopata uhuru—Finland mwaka 1917 na Tanzania miaka ya 1960,"amesema.
Ameongeza kuwa uhusiano huo wa kihistoria ulianza tangu enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, pamoja na Rais wa kwanza wa Finland.
Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, amesema kuwa ujio wa Rais Stubb ni matokeo ya uongozi thabiti wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
"Rais Stubb ameona fuvu la Zinjanthropus, zana za jadi, na hatua mbalimbali za maendeleo ya mwanadamu. Hili ni jambo la heshima kubwa kwa taifa letu," amesema Mhe. Chana.
Aidha, ameeleza kuwa kupitia ziara hiyo, Tanzania na Finland zimekubaliana kuendeleza mashirikiano katika maeneo ya mafunzo, tafiti za pamoja, na kubadilishana uzoefu katika sekta ya makumbusho na malikale.
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania, Noel Luoga, amesema kuwa ziara hiyo imekuwa chachu na hamasa kubwa kwa taasisi hiyo kuendelea kutangaza utalii wa malikale.
"Tunatarajia kushirikiana na Finland katika tafiti, kuboresha maonesho kwa kutumia teknolojia za kisasa, pamoja na kuhakikisha makumbusho yanafika kwa jamii," amesema Luoga.
Ziara hiyo pia imehudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, pamoja na watendaji wa baadhi ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
NCAA YASHIRIKI WARSHA YA KUHAMASISHA UANZISHWAJI WA JIOPAKI KATIKA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI.
Na Mwandishi wetu, Addis Ababa, Ethiopia
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) inashiriki warsha ya kimataifa iliyolenga kuhamasisha uanzishwaji wa hifadhi za jiolojia (UNESCO Global Geoparks) katika nchi za Afrika Mashariki iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (@UNESCO ) kwa kushirikiana na Wizara ya Utalii ya Ethiopia.
Warsha hiyo inayofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia kuanzia tarehe 12 hadi 15 Mei, 2025 imewakutanisha wataalamu wa Jiolojia, urithi wa asili, malikale na watunga sera kutoka nchi mbalimbali za Afrika Mashariki ambazo ni Ethiopia, Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, na Djibouti, kwa lengo la kujadili na kuweka mikakati ya kuanzisha na kukuza hifadhi za jiolojia katika ukanda wa nchi za Afrika.
Akizungumza katika ufunguzi wa warsha hiyo, Waziri wa Utalii wa Ethiopia, Bi. Selamawit Kassa, alieleza dhamira ya serikali yake kuanza hatua za awali za kuanzisha jiopaki nchini humo, kutokana na urithi mkubwa wa jiolojia uliopo nchini Ethiopia na kusisitiza kuwa jiopaki ni njia muhimu ya kuhifadhi urithi wa asili na kuchochea maendeleo ya kiuchumi kupitia utalii endelevu.
Hifadhi ya Ngorongoro ambayo ni hifadhi pekee katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara yenye hifadhi ya Jiolojia ya Ngorongoro Lengai (Ngorongoro Lengai UNESCO Geopark) kupitia kwa Afisa Uhifadhi Mkuu Dkt. Agness Gidna imewasilisha uzoefu na mafanikio yake katika kuanzisha, kusimamia na kuendeleza Hifadhi ya Jiolojia ya Ngorongoro Lengai ambayo ni jiopaki pekee iliyopo kusini mwa Jangwa la Sahara na ya pili barani Afrika ikitanguliwa na M’Goun UNESCO Global Geopark ya Morocco.
Akitoa uzoefu wa usimamizi wa Jiopaki ya Ngorongoro Dkt. Agness @AGidna ambae ni mtaalam wa Urithi wa Utamaduni NCAA, alieleza wajumbe wa mkutano huo kuwa hifadhi ya jiolojia ya Ngorongoro Lengai upekee wake unatokana na urithi wa kijiolojia, kiikolojia na kiutamaduni unaojumuisha Mlima Lengai wenye volkano hai ya kipekee duniani na eneo la Ngorongoro lenye historia ya binadamu wa kale pamoja na vivutio vya utalii vilivyopo na jinsi unavyosaidia jamii zinazozunguka hifadhi hiyo. Kwa mujibu wa UNESCO, hadi sasa kuna UNESCO Global Geoparks 229 katika nchi 50 duniani, Geopark mbili tu kati ya hizo ndio zilizopo Afrika.
Hali hii inatoa fursa kubwa kwa bara hili kuwekeza zaidi katika kutambua, kuhifadhi na kuendeleza maeneo ya urithi wa jiolojia, ambayo mengi bado hayajatambuliwa kikamilifu.
Katika warsha hiyo, washiriki wanatarajiwa kuibua mikakati ya pamoja ya kitaifa na kikanda, pamoja na kuanzisha mitandao ya ushirikiano katika kukuza jiopaki kama njia ya kuhifadhi mazingira, kuendeleza elimu, kuimarisha uchumi wa jamii na kuboresha utalii barani Afrika.
Tanzania kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ambayo ilitambuliwa na UNESCO kupata hadhi ya Jiopaaki mwaka 2018 imepata fursa ya kuhamasisha nchi nyingine kufuata nyayo zake katika uanzishaji wa hifadhi za jiolojia, ikiendelea kuwa mfano wa kuigwa na kinara wa uhifadhi endelevu barani Afrika. @unescodar@visitngorongoro@GlobalGeoparks
Glad to see that Tanzania's #Ngorongoro Lengai UNESCO Global Geopark is experiencing a revival through China's first foreign-aid geological park project. The geopark's museum will open in June as a landmark building, introducing visitors to an exhibition of Tanzania's rich geological and cultural heritage.
Vote for Ngorongoro Conservation Area (NCA) as Africa’s Leading Tourist Attraction 2025; https://t.co/o0bWGr5oKJ
#wta2025#voteforngorongoro#visitngorongoro
#unforgettableexperiences
#worldtravelawards2025
Join us for What’s Cooking in the Pastoral Neolithic? New Approaches to African Foodways, Friday, February 28, 4-6pm, Sewall 570 and Zoom.
To register for the Zoom meeting, click here: https://t.co/3nbBxUkcUU
Read more about the event below