Mambo mengine huja katika hali ambazo hatuzipendi. Hapo ndipo mtu anapaswa kuwa na subra njema.
Na mnaweza kuchukia kitu nacho ni Kheri kwenu, na mnaweza penda kitu nacho ni shari kwenu. Na Allah anajua nanyi hamjui. ( Al-Quran)
#Ramadan #2
#SubraNjema
Swiyyam.
Tumemuusia mtu kwa wazazi wake wawili. Mama yake ameichukua mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na kumuachisha ziwa baada ya miaka miwili. Tumemuusia! Nishukuru Mimi ( Mola wako ) na wazazi wako. Ni kwangu mimi ndio marudio. ( Qur'an 31:14 )
Wema kwa wazazi ni masiku yote.
Mola wetu Mlezi! Umekienea kila kitu kwa rehema na ujuzi. Basi warehemu waliotubu na wakaifuata njia yako, na waepushe na adhabu ya #Jahanamu. ( Qur'an 40:7 )
Amiyn.
Basi someni kilicho chepesi katika Qur'an. Allah! Anajua baadhi yenu watakuwa wagonjwa, na wengine wana safiri katika ardhi wakitafuta fadhila za Allah. Kwa hiyo someni kilicho chepesi humo, na mshike Sala, na mtoe Zaka, na mkopesheni Allah mkopo mwema. ( Qur'an 73:20 )
Sheikh #Mselem_Ally anatumia lugha nyepesi mmno kwa kila mmoja wetu kukielewa achokifikisha. #Allah azilainishe nyoyo zetu ziwe ni zenye kusikia mazuri na tukayafuata.
Swadaqa haimalizi Mali.