Kama kuna mwenye taarifa tofauti na hizi alizotaja Eng Hersi tunaomba atusaidie. Hapa hajazungumiza kikosi, wadhamini, wanachama na bonus za mafanikio.
Nimeona msg nyingi za watu DM wanaomba namba ya muamla ili wanipe ya soda sasa badala ya kumtumia mtu mmoja mmoja naomba niiweke hapa.
Kila anaewiwa kunipa soda aweke kwenye hii namba
Airtel 0684775121
Jina Hilda Newton
Baada ya mechi ya Rayon v Yanga kila Kolo aligeuka kuwa mchambuzi. Mlisema pengo la Aucho ni kubwa sana, timu haijaunga, mbinu za mwalimu hazionekani. Si tuliwaambia timu imekaa kambini siku 10? Nyinyi mlioungana na kuzoea mbinu za mwalimu hongereni kwa ushindi na cleansheet. ๐
Ni mapema sana kutoa maoni kuhusu sajili za Msimbazi ila kama timu yenu haitabadilika zaidi ya hapa basi mnakwenda kuwa na msimu wa tabu na mateso mengi sana. Hawa ndio mliwaficha pre season? ๐
Afrika Mashariki hakuna timu ambayo inaongoza kwenye maswala ya FANS ENGAGEMENT na PR kama Yanga, these lads know there job very well.
Jambo lao hata liwe dogo vipi watahakikisha linazungumzwa kwa ukubwa mno.
"Kwenye siku ya Wananchi hamjawahi kuniona kwenye kipaza wala eneo lolote nikifanya vurugu zangu. Mwaka huu nimo, mimi ni kisima cha ubunifu na wote mnanijua
Nikishaingia, hakuna binadamu yeyote atakayejadili entrance ya mtu mwingine zaidi yangu, nitaishtua dunia"
๐๏ธ Ally Kamwe
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo September 10, 2025
Part 1
Kesi imeanza
Kasimama Wakili Nassoro Katuga anatambulisha Jopo la Mawakili wa Serikali kama kawaida yao.
Wapo mawakili sita wanaiwakilisha Jamhuri.
Katuga anasema mshitakiwa yupo.
Anaulizwa Mhe. Lissu nae anasema yupo tayari.
Majaji kama kawaida wapo wote watatu.
Katibu Mkuu wa Chama pia yupo hapa ameingia.
Kumbukeni leo tuna kesi mbili na ile ya mgawanyo wa mali za CHADEMA
Baadhi ya Mawakili wameanzia huko.
Sasa anasimama Job Mrema Wakili wa serikali.
Job Mrema: Naomba nianze kusema naunga mkono yote aliyosema Nassoro Katuga na naomba niongeze baadhi ya vitu.
Kuhusiana na Presidential Affairs Act kifungu cha 9 kinaelezea utaratibu ambao upande wowote unataka kuwaita mashahidi kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Lakini kifungu cha 9 tulichosema jana kilikuwa cha zamani lakini kwa mabadiliko ya sheria ya sasa sio kifungu cha 9 bali ni cha 10. Kwahiyo tunaomba ieleweke kuwa ni kifungu cha 10 pale kwenye tisa sio.
Kifungu cha 2 cha Sheria hii kinamtaja Rais, Makamu na Waziri Mkuu.
Hivyo kwa utaratibu ulioainishwa kwenye kifungu cha 10 unawazungumzia hawa vipngozi watatu wote.
Mashahidi hao wakihitajika utaratibu wa kufuatwa ni huo hapo.
Naomba nikisome tafadhali.
Anaanza kukisoma hicho kifungu cha 10.
Kingereza fulani cha Uyole ๐คฃ๐คฃhuyu sijui kama ni mchaga kweli.
Kwahiyo tumesema haya ili utaratibu ueleweke.
Compliance ya hiki kifungu haikufanyika. Na mshitakiwa alishauriwa kama anataka hao wawe mashahidi wake atakuja kuomba jambo hilo hapa mahakama kuu.
Mahakama hiyo ndio hii tuliyopo sasa anapaswa kuomba sasa kwasababu ndio inauwezo wa kusikiliza shauri.
Na kimsingi naomba kusisitiza hajaathirika na chchote kwasababu ndio kwanza mahakama inaanza.
Waheshimiwa majaji jambo kubwa tunalofahamu kwamba mahakama hii itajiuliza.
Je pingamizi lililoletwa na mtuhumiwa liko sawasawa mbele ya mahakama hii.
Lakini pia naomba kufanya marejeo ya kesi kama tatu.
1. George Aldon Kilinga and another vs Anna Joseph Riwa and another Civil appeal no. 6 2023 TZ HC 19093.
2. Joseph Mkenda vs Ladislaus PC Civil Appeal No. 132, 2023 [2024] HC 56
3. Commissioner General Tz Revenue Authority and AG vs Milambo Limited Civil appeal No. 62/2022
Anasimama Mh. Lissu anaomba wampe Nakala ya kesi wanazotaja.
Jaji anasema mpatieni sasa.
Katuga anasimama anasema jaji zipo kwenye mtandao hizi kesi.
Mh. Lissu anasema sasa niko gerezani nazipataje huko mtandaoni? Watu wanacheka๐คฃ๐คฃ
Jaji anasema sasa mawakili wa serikali mpo wengi sana chaguaneni mmoja akazilete hizo printed case.
Anaondoka Wakili mmoja.
Anasimama Katuga anasema naona mahakamani yupo mtoto ni kinyume na sheria kifungu cha 193 cha CPA.
Jaji anasema haya muondoeni huyo mtoto.
Ni kama watu wamesikitika fulani. ๐คฃ ika ndio sheria sasa.
Dogo alikuwepo ana umri kama wa miaka 13 hivi amekula suti amependeza sana na alikuwa anasikiliza kwa hisia sana.
Anaonekana ana ndoto ya kuwa Wakili pia huyu na alivyo alivyo huyu dogo ni kama anamkubali Mh. Lissu.
Ipo siku tutapata story yake bila shaka hata kama ni baada ya miaka 15. Kuna siku anaweza kuja kulielezea Taifa kuhusu kisa hiki akiwa tayari amekuwa Wakili labda enzi hizo wahenga wanasema muda ni mwalimu mzuri.
Haya anaendelea Mrema sasa.
Mleta pingamizi hakuieleza mahakama anaposema mahakama hii haina jurisdiction kwa mfano pecuniary jurisdiction au nyingine.
Alivyotaja hiyo pecuniary mawakili wamecheka.
Watakuwa wameelewa jambo ambalo sisi ma layman hatuelewi.
Mawakili wamecheka kwa dharau nahisi kutakuwa na kaujinga hapo.๐๐๐
Nitawauliza niwape mchapo baadae.
Je mahakama hii ina mamlaka au laa ndio hoja kubwa sasa mwenzetu hajasema hayo mamlaka ni yapi katika zile aina za mamlaka zinazojulikana kisheria.
Part 2 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 6
Amemaliza Wakili wa Serikali Mrema
Naona Majaji wanajadili jambo kidogo hapa
Jaji Nduguru anasema kila upande una wajibu wa kuiambia mahakama sio useme navumilia.
Kama kuna jambo lilionekana mapema kuna lina shida ulipaswa kusema na sio kusema nilikuwa navumilia.
Naomba tuwe guided na sheria maana sheria iko hapo.
Wote tunajua kuwa tunabanwa na pleadings na pleading ni ile PO yenyewe.
Msemaji unakuwa kwenye jicho la unasema mambo mengi ambayo yako on face of records.
Anaendelea Mhe. Lissu sasa.
Waheshimiwa majaji nimezungumza sana kuhusu records.
Sasa naomba nirudi kwenye sheria ya ukabidhi.
S. 262 of CPA Nilisema pia kuhsuu kesi ya Dodoli Kapufi kuwa lazima mwenendo wa committal lazima ufuate sheria.
Maombi yaliyopelekwa kwa Jaji mtembwa inasema yaliambatana na viapo viwili.
S. 266[3] ya CPA ndio hoja yangu.
Inazungumzia nini kinapaswa kuwepo kwenye record of proceedings.
Sheria inasema kila records inayopelekwa kwa mshitakiwa inapaswa kujumuisha nyaraka zote ikiwemo zilizotumika kwenye jambo lolote mahakama kuu au mahakama zingine. Hawajaniambatanishia hayo manyaraka yote.
Waheshimiwa majaji hizo nyaraka kupewa mtuhumiwa iko sababu.
Sababu yenyewe iko kanuni ya 5(1) na 5(2) ya kanuni za ulinzi wa mashahidi.
Zinasema mahakama itatoa amri endapo itaridhika kuwa mtu ambae amelindwa kuna hatari atakuwa kwenye tishio la usalama.
S. 263(4) of CPA (CRIMINAL PROCEDURE ACT yaani sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai)
Inamtaka mahakama kumuelezea mtuhumiwa atakapotoa taarifa yake asiwe na hofu na wala asitegemee upendeleo wowote.
Whatsoever he says may be given in evidence at the trial. Lolote atakalosema chochote alachosema kinaweza kutumika kama ushahidi katika trial yaani kesi ya msingi huko mahakama kuu.
S. 265(5) inasema yote ambayo mtuhumiwa atakachosema kirekodiwe na asomewe.
Sasa Waheshimiwa Majaji naomba niwapeleke kwenye records kuhusu chochote nilichosema je kiliruhusiwa? Je kilirekodiwa? Je nilisomewa? Twende sasa.
Kwenye rekodi ya Ukonga, kuna maneno ukurasa wa 5 kuna maneno ambayo yamesemwa na mahakama.
Ukisoma sheria hayo maneno yanapswa kuonekana kwneye rekodi na hayapo.
.sheria inasema aambiwe na asome.
Rekodi haioneshi kama aliambiwa. S. 263(5) of CPA nilipaswa kurekodiwa kwenye kila nitakachosema.
Sasa kwneye rekodi hii hakuna mahali kokote mtuhumiwa aliambiwa maelezo yako ni haya na ulichosema ni hiki unachochote cha kuongeza? Sijawahi ambiwa hivyo na hayapo kwenye records.
Na wala sijawahi kuulizwa una chochote cha kuongeza. Mimi sio vyakuongeza hata vyakwangu sikumaliza.
Sasa tuje rekodi ya mahakama hii kuanzia ukurasa wa 93 niliyosema yalipaswa kuwepo hayapo pia hata hayo.
Sijawahi kuambiwa kwamba haya ni maelezo yako. Nakusomea na kuulizwa una nyongeza sijawahi kuulizwa.
Maelezo haya ni ushahidi sio urembo kabisa.
S. 263(6) of CPA maelezo ya mtuhumiwa ni lazima mtuhumiwa aseme ni kweli au sio kweli? Ni maelezo yake na anayakubali.
Hakimu wa ukabidhi ni lazima athibitishe hiyo rekodi. Ukurasa wa 13 wa rekodi ya Ukonga. Pia Ukurasa wa 98 wa rekodi ya mahakama hii angalieni.
Ni lazima nyaraka hizo ziwe certified. Hakimu anasema maelezo hapo juu nathibitisha kuwa ni ya mtuhumiwa na amekiri ni yakwake. Kifungu ameweka 263(3) wakati kiuhalisia kifungu halisi ni 263(6). Anapothibitisha kuwa nilisema mimi na kukiri kuwa ni yangu. Ni wapi nilisema hayo?
Haya yaliyopo yaliandikwa wapi na lipi na lini na nani aliandika?
Sheria iansema mtuhumiwa anapaswa kusign or attest baada ya yale niliyoyasema.
Sahihi yangu wala dole gumba halipo wakati sheria inasema iwe hivyo.
Part 7 itaendelea post inayofuata.
Naomba Repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 3
Anaendele Mhe. Lissu
Kesi iliahirishwa 15/07 na siku hiyo kulikuwa na ugomvi kuhusu kuahirisha kuanzia page 53 to 60.
Hii siku pia aliandika a reasoned ruling kwneye page 68 to 73 na hiyo ikawa mara ya tatu kwa Hakimu kutoa sababu za msingi za kuahirisha kesi.
Waheshimiwa majaji tar. 30/07 kesi ilikuja na ugomvi wa kuahirisha ukawepo tena mkubwa.
Mtaiona hiyo kwenye page 74-79.
Maneno ya Hakimu kwenye page 79 yanasema "uamuzi kwamba hii kesi ifutwe au vipi tutaitoa tar. 13 August" je hiyo ndio reasonable cause ya kuahirisha kesi?
Hapa napo hakukuwa na sababu za kuahirisha kesi.
Ilipofika hiyo Tar. 13 August wakasema tuahirishe tena na hakimu aliwakubalia bila kutoa sababu.
Hayo yapo ukurasa wa 80 na 85. Kulikuwa na rival submission pale mahakama ya Kisutu.
Kwamba mashauri haya yataoneshwa mtandaoni au la yataamuliwa tarehe nyingine.
Sasa hii nayo ni sababu kweli ya kuahirisha kesi?
Suala la adjournment akaliacha hakulisemea.
Hizo adjournment ambazo zilikuwa granted unlawful, in blantant controversial of sec. 265.
Kila walipoahirisha I paid the price ya kurudishwa gerezani ya kwenda kufungwa na watu waliohukumiwa kifo.
Mtaona kwenye rekodi kuwa niliilalamikia sana inakuwaje mahabusu anachanganywa na condemned prisoner.
So kila walipoahirishwa nilirudishwa kwenda kuchanganywa na wanaosubiri kifo kule magerezani.
Mh. Lissu anaendelea.
Leo amepiga Kombati ya Chama mikono mifupi.
Leo anafuraha jana ni kama alikuwa amekasirika sana.๐คฃ๐คฃ๐คฃ
Maaskari wa Magereza nao wameacha kujifunga usoni.
Leo nawaona wawili tu waliojificha sura. ๐คฃ
Wengine wote tunawaona uso kwa macho.
Sasa tuendelee.
Siku 131 nilikaa hadi siku niliyosomewa commitall ndio maana nilimwanbia asije akawa kama Jaji aliyemuhukumu Jomo Kenyata. Asije akafanana nae.
Jambo lingine dogo linachekesha.
Kwenye rekodi mliyonipa hapa Hakimu Franco Kiswaga page 74 kunaonekana kulikuwa na mashauri tar. 31/07 sasa hiyo tarehe hakukuwa na mashauri yoyote.
Nenda kwenye ukurasa wa 81 hadi 85 kuna submissions. Zilipoanzia ni Tar. 13/August lakini ukweli ni kwamba zilifanyika tarehe 18 August.
Mambo ya Tarehe 18/08 yeye ameandika kuwa yalifanyika tarehe 13/08 sasa natamani kusema kuwa haya yalikuwa ni makosa ya kibinadamu lakini kwa namna yalivyoenda pale kisutu nasema huu nao ulikuwa ni mwendelezo wa uhuni uliofanyika pale Kisutu.
It is not accidentall it is deliberate fabrication.
Part 4 itaendele post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Septemba 9, 2025
Part 1
Kesi imeanza Mhe. Lissu ameingia. Katuga amesimama na kutambulisha jopo lake na mshitakiwa amesema yuko tayari.
Jaji amesema naomba nitoe mrejesho wa tulianzia wapi jana na tuliishia wapi? Ametoa huo mrejesho kuwa sasa tuendelee na lile pingamizi la endapo mahakama hii ina mamlaka ya kuendelea.
LISSU: Mh. Jaji nashukuru, jana nilipewa nafasi nikasome. Sasa hiyo kazi nimeifanya usiku kucha kwahiyo naomba kwa kuanzia nieleze tofauti zilizopo kati ya hizi nyaraka mbili na ili nisiwachanganye ninaposema rekodi ya Ukonga maana yake ni ile niliyoletewa na hakimu wa mahakama ya Kisutu na hakimu FRANCO KISWAGA ndio alimpa Kamishina mSaidizi wa Polisi Rabi Stima.
Rekodi ya Ukonga nina maana ni hiyo nyaraka niliyoletewa na Hakimu Kiswaga.
Kwahiyo nikisema rekodi ya Mahakama hii nitakuwa namaanisha ile niliyopewa jana.
Sasa naomba nianze.
1. Utofauti wa rekodi ya Ukonga ina kurasa 16 tu. Rekodi ya Mahakama hii ina kurasa 101. Sasa hizo kurasa zingine zilikuwa wapi? Nyaraka za mahakama zinawezaje kuwa na utofauti wa namna hii? Katuga hawakumpa hii niliyonayo mimi.
2. Rekodi ya Ukonga haina ile scanned berg (kibox pembeni kulia) inamaanisha ni original. Sasa ya ukonga haina lakini niliyopewa jana inazo hizo scanned berg. Sasa ililetwa na mahakama lakini sio original.
3. Rekodi ya ukonga inaanza tarehe 18/08 na inaishia Tar. 18/08. Kwa kifupi ilianza siku hiyo hiyo na kuishia siku hiyohiyo. Kesi ilianza na kumalizika siku hiyohiyo. Rekodi ya Mahakama hii imeanzia April 10, 2025 na kuishia Agosti 18, 2025. Mliyonipa hapa ilikuwa imekamilika kwa kila kitu.
4. Ukurasa wa 1 wa rekodi ya Ukonga na Ukurasa wa 86 wa rekodi ya Mahakama hii. Ukiangalia ile ya Ukonga page 1 ni kwamba commitall proceedings ilianza immediately. Yani mwanzo pale committal proceedings open, evident on itself lakini kwenye rekodi ya mahakama hii ukurasa wa 86 kulikuwa na ubishani mkubwa sana ambao umerekodiwa. Utaona baada ya corum kuna heading inaitwa Proveedings Mr. Katuga alielezea mambo kadhaaa.... ilianza hivyo. Kinachofuata kuanzia page 86 hadi 89 ni submissions kati ya prosecution na mimi mwenyewe. Rekodi ya ukonga mabishano hayo hayapo kabisa. Lakini hii niliyopewa hapa kila kitu kipo.
Utaona kwa mfano ukurasa wa 87 rekodi ya mahakama hii Hakimu alisema nimezingatia mawasilisho ya pande zote. Na akatambua uamuzi wa mahakama kuu. Mambo hayo kwenye document nikiyoletewa hayakuwepo na hakuambatanisha.
6. Kwenye ukurasa wa 15 wa rekodi ya Ukonga kuna orodha ya mashahidi halafu kuna maneno kuwa na mimi mshitakiwa I WILL CALL THE FOLLOWING WITNESSSES
Lakini kwenye ukurasa wa 100 wa rekodi ya Mahakama hii inasema I will call my witnesses and I will have my Advocates.
Kwenye rekodi ya ukonga na kwenye orodha ya mahakama hii hawajaandikwa mashahidi wangu.
Sio kwamba hawakuwepo, niliwataja lakini nyaraka hizi hazina majina hayo.
1. Samia Suluhu Hassan
2. Isdory Mpango
3. Kassim Majaliwa
Hao wote niliwataja lakini hawakuandika kabisa.
Nitarudi kwenye hilo la majina baadae.
Lakini ieleweke kuwa majina hayo nilitaja mchana kweupe kila mtu alisikia na ilikuwa kwenye Open Court. Aliamua kwa matakwa yake mwenyewe kutokuyaandika.
Hizi nyaraka zote zimetoka Kisutu na zinadai kuwa ni committal proceedings.
Which one is forgery and which one is original.
Mahakama hii inapaswa kujibu why this differences?
Jana niligusia kidogo kwamba kulikuwa na maahirisho mengi sana.
Nilisema yalikuwa zaidi ya 10 hayo maahirisho. Niliposoma usiku nimegundua iliahirishwa mara 13.
Kesi inapoahirishwa kwenye commitall proceedings s. 265(1) the court must record the reason of adjournment and for reasonable cause that adjournment can be granted.
Na hiyo sababu ya msingi lazima iandikwe katika mwenendo.
Sasa nataka nioneshe namna mahakama ya Mh. Franco Kiswaga ilivyoheshimu huo utaratibu wa kisheria.
Part 2 inaendelea post inayofuata.
Naomba Repost yako kwenye tweet hii.
Oyaaa hii kesi ishakuwa ngumu
Mahakama ya Kisutu na yenyewe inatuhumiwa kwa kughushi nyaraka kwenye kesi dhidi ya Mhe. Lissu
Kumbe ndo maana yule Hakimu Kiswaga alikuwa mkali sana + kumkandamiza Mhe. Lissu pale Kisutu kumbe behind the scene alikuwa na mambo yake na Mawakili wa Serikali leo wamepata aibu ya mwaka.
Wakili Katuga kanywea kama sio yeye.๐
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 9
Anaendelea Mhe. Lissu
Kwenye ukurasa wa 61 wa hii niliyopewa leo kuna taarifa kwamba kunashauri yamefunguliwa mahakama kuu kuhusu kuficha mashahidi na mkiangalia.
Pia font ya nyaraka niliyoletewa awali na font niliyoletewa leo. Ombi langu hatuwezi kuendelea leo naomba tuahirishe mnipe muda. Usiku wa leo utanitosha kesho turudi nije kuwaonyesha uchafu uliofanyika hapa.
Documents zimekuwa falsefied naomba tuahirishe turudi kesho ili nije kuendelea.
Kwa kifupi ni kwamba wahuni walitengeneza nyaraka mbili tofauti wakampelekea nyaraka tofauti.
Anasimama Katuga hapa, anaomba azungumzie hiyo criminality.
Jaji anasema ukitaka ku respond kwenye hilo utatuvuruga subiri basi akimaliza na wewe utapata muda wa kujibia huko mbele.
Lissu anasema Wakili atakuwa na hoja asitupotezee muda hapa.
Wananchi wanacheka. ๐๐๐
Majaji wanaandika hapo tusubiri maelekezo yao. Wameanza kuteta kidogo.
Jaji anasema tunaomba utunze maoni yako. Utapata muda wa kujibu maana hajamaliza na linaweza kuibuka lingine utapata muda wa kujibu uwe na utulivu tu Wakili.
Mheshimiwa Lissu amesema yeye usiku wa leo unamtosha ataenda kusoma kila kitu. Tukutane kesho asubuhi.
Tunawasubiri majaji sijui wanasema nini?
Maana ilitakiwa Mtuhumiwa apewe proceedings zote zimekamilika ametokea muhuni mmoja huko ameandika summary tena nyingine kwa mkono vi page kama 20 hivi halafu wakagonga mihuri ya mahakama.
Jaji anasema tukutane kesho saa nne asubuhi.
Mahakama imeahirishwa.
So kutane hapa kesho saa 4 asubuhi.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 8
Tumerudi Majaji wameingia.
Kama kawaida wako watatu.
Kumbukumbu ni kwamba tuliahirisha ili Mh. Lissu akasome nyaraka za proceedings alizopewa leo mara baada ya zile za kwanza alipewa nusu ambazo zimeanzia Tar. 18/08 na sio kuanzia Tar. 10/04.
Ngoja tusubiri mrejesho.
Je tutaendelea na shauri au hatutaendelea nalo? Je Mhe Lissu amesema amekuta mambo gani huko kwenye nyaraka alizopewa leo na je zina utofauti gani na zile alizokuwa amepewa mwanzo. Tutajua muda sio mrefu.
Majaji waaandika kidogo hapa.
Jaji anasema naomba tuendeleee.
Anasimama Katuga anasema Corum iko vilevile na mshitakiwa yupo.
Jaji anasema ongeza sauti.
Katuga anarudia hapa alichokuwa anazungumza.
Mshitakiwa yupo na shauri linakuja kuendelea na kusikiliza mapingamizi au wasilisho wa mshitakiwa kwenye suala la mamlaka ya mahakama hii.
Lakini pia tulikuwa na concern kwamba wenzetu wa Magereza wanasema barabara haziko vizuri tunaomba tusifike usiku sana.
Ni hayo tu mheshimiwa Jaji.
Kwa maneno mengine KATUGA anatuambia barabara za nchi hii ni tatizo sana.
Anapewa nafasi Mh. Lissu.
Mh. Lissu anasema sitawaweka sana kwa leo asiwe na hofu.
Nimepata hii record saa 10 kasoro dakika mbili na mlisema tukutane saa 10 na dakika kumi. Kwahiyo nimepata dakika 12 pekee za kupitia hiyo nyaraka.
Sasa sijaenda mbali sana kwenye kuisoma hii record. Hivyo naomba niseme lifuatalo.
Ukizisoma hizi nyaraka mbili ambazo zote nimeletewa.
Ukisoma zote kuna jambo limefanyika nafikiri litakuwa ni kosa la jinai.
Kuna criminality involved.
Record mliyoagiza nipewe na nimepewa. Precedings za Tar. 18/08 nilizopewa mwanzo.
Kwenye hii mpya niliyopewa Proceedings za Tar. 18/08 zinaanzia ukurasa wa 80.
Kwahiyo kwa kuhesabu idadi ya kurasa hizi nyaraka nilizopewa zinatofautiana.
Jambo lingine from page 86 kwenye hii niliyopewa leo kuna kitu kimeandikwa proceeding halafu kuna COURT ORDER iko page 86 hadi 89 lakini kwenye hii niliyoletewa mwanzo. Hiyo ORDER haipo kabisa.
Niliyoletewa gerezani haina hizo page kabisa za hiyo Court ORDER.
From page 94 to 98 kwenye niliyoletewa mahakamani ziko page 6 to 14 kwenye niliyopewa mahakamani.
Sasa hizi nyaraka zote nimepewa zikionekana ni nyaraka za mahakama?
Kwanini zitofautiane? Kwanini niletewe nyaraka gerezani ambayo sio yenyewe na ambayo nilipaswa kupewa.
Wako watu wamegushi kuna doctoring hapa. Zimeghushiwa. Zimefanyiwa mchezo mchafu.
Part 9 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii