‼️🚨MTOTO AMEPOTEA‼️
Mtoto anaitwa Athumani Masudi, umri wa Miaka 14, anasoma Mvumoni secondary school - Kidato cha Kwanza. Amepotea toka Jana asubuhi alivyokuwa anaenda shule hakurudi.
Mwenye taarifa piga namba 0678098076
Mama yake kijana ni mjane anamlea mwenyewe huyu mtoto - please tupambane tumpate mtoto!
Leo #MariaSpaces tunajadili: Kesi za mchongo, utekaji mauaji - kuna maridhiano gani ya kitaifa?
Kila kukicha tunaendelea kuona dhulma kubwa na mauaji huku watawala wakiongelea maridhiano - kama Taifa tunaridhiana vipi? Tunatokaje
Leo saa 2 uck
#MariaSpaces : Kesi za mchongo, utekaji mauaji - kuna maridhiano gani ya kitaifa?
Kila kukicha tunaendelea kuona dhulma kubwa na mauaji huku watawala wakiongelea maridhiano - kama Taifa tunaridhiana vipi? Tunatokaje
Leo saa 2 usiku
Huyu ni Mwenyekiti wa BAVICHA Wilaya ya Kilosa, Kamanda Yohana Kibasa ambae pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Nyavisi kilichopo Kata ya Ruaha na Jimbo la Mikumi.
Hapa ni Msibani kwa Kamanda na Mwanachama wetu Joseph Mlasu aliyefariki baada ya kupata ajari.
Niliwaambia hawa DPP na serikali wamekimbilia kwa Jaji Mkuu 😁 - Lissu kawabana kila kona kweli! Wameishiwa legal arguments!
Yaani ni vituko 🙄
Na niwaambie @ccm_tanzania the only solution ili Taifa itulie ni #FreeTunduLissu na #SamiaMustGo
Mnachelewesha the inevitable! Na mtatekeleza tu haya!
Nasema #TutaelewanaTu
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 221
Jaji Ndunguru ameteta sana na wenzake kama dakika 10 hivi.
Sasa anawasha kipaza sauti.
Anasema yafuatayo: tumesikiliza hoja zote hivyo vijembe vyenu msivilete.
Sasa mshitakiwa alisema anapingamizi na tukasema upande wa mashitaka walete open statement ili Mahakama iamue.
Mambo mengine ya kwamba imeambatana na nini na nini kipo wapi hayo sio mambo ya msingi.
Mshitakiwa endelea sasa, hawa upande wa mashitaka mmemaliza hapo, presentation ya notice na justification ya notice.
Watu wanacheka hapa 😂😂😂😂
Nafikiri mpaka sasa Katuga ameelewa nani ni Bingwa wa Sheria.
Mhe. Lissu amasimam, sasa Waheshimiwa Majaji kwa kuanzia niseme hivi waliyosema wenzetu.
1. Upande wa mashitaka unasema notice yao haileti shahidi mpya bali inaongezea ushahidi wa shahidi ambae ushahidi wake ulishatolewa kwenye committal.
2. Wamemtaja huyo shahidi kwa jina kabisa.
3. Wamesema wameleta viambatanisho vinavyotakiwa kwa mujibu wa kifungu cha 308(2) cha CPA.
Sasa baada ya kusema twende kifungu kinavyosema cha 308
A witness whose statement or evidence was not read during committal......
Kifungu kinasema shahidi mpya.
Kinachotakiwa kuletwa ni jina la shahidi wa ziada, huyu ndio anaweza kutolewa notice.
Wamesema wenyewe hawaleti shahidi mpya bali wanaongezea ushahidi wa shahidi aliyepo.
Sasa huyu shahidi ambae tayari yupo na wamemtaja huyo Shahidi ACP Amin Mahamba.
Sasa waheshimiwa Majaji naomba niwaalike kwenye ukurasa wa 90 na 91 na 99 na 100 wa record ya committal proceedings na ukurasa wa 134 wa record ya Mahakama hii ambapo upande wa mashitaka ulitaja majina ya mashahidi wao.
Huyo Amin Mahamba yupo na mimi maelezo yake ninayo hapa sasa Waheshimiwa majaji hiyo notice inaingiaje mahakamani.
Ushahidi wake tayari upo mahakamani na notice inatakiwa iwe ya shahidi ambae maelezo yake hayakusomwa mahakamani.
Hii sio notice ya additional witness ni notice ya additional evidence ambayo haipo kisheria nimetafuta CPA yote hicho wanachosema hakipo.
Jambo lingine ni kwamba wanaleta ushahidi wa mtu aliyefanya upelelezi wa matukio ya uchaguzi mkuu 2025 sasa Majaji matukio ya tukio ya tarehe 29/10 mimi tayari niko mahabusu
Anasimama Katuga anasema tunapinga anaanza kujadili ushahidi wetu kama mtakubali ni sawa tu.
Lissu: Si ndio kayaleta haya mwenyewe wanakatazaje nisiyazungumzie?
Jaji Ndunguru: Mshitakiwa endelea.
Lissu: amesema mwenyewe kwa mdomo wake hapa Mahakamani. Nilimwambia asibwabwaje sana. Akang'ang'ania kuanza kusema mambo ya tarehe 29/10 ndio maana na mimi nasema hayo ya tarehe 29 mimi nilikuwa jela.
Wanafikiri hayo yatawasaidia maana wanataka kugeuza mashitaka kwa kuleta mambo ya tarehe 29/10/2026. They can not amend the information through the back door. Kama mnataka ku amend information nendeni kwenye kifungu cha 294 ch CPA.
Hiyo wanayoiita notice haipo kisheria. Haitambuliki. Hiyo notice muifutilie mbali. Yaani notice na yaliyomo.
Na mwisho, Wahe. Majaji hiyo notice ikiachwa ikawa sehemu ya record ya Mahakama itafungua sanduku la pandora ambalo lina kila aina ya mambo mabaya ambayo sidhani kama itaweza kushughulika mambo hayo.
Wanataka tuzungumze mambo ya October 29 mtakuwa mmefungulia balaa na isije ikawa shida. Mkifungua huo mlango tutaenda huko. Tutazungumzia mauaji ya kimbali na tutaulizana nani aliyeua watanzania. Hii kitu haina mashiko. Are they ready? Mimi niko tayari. Isiruhusiwe ikiruhusiwa niko tayari?
Jaji tafadhali naomba tusiende huko.
Katuga aliambiwa na Lissu kuwa huwezi kunifundisha Sheria akakataaa. Baada ya Lissu kumaliza hapa. Katuga amekuwa mdogo sana yani. Ni kama anataka kulia.
Katuga anasimama anasema napaswa kufanya nini reply au rejoinder
Mhe. Lissu anasema fanyeni reply halafu mimi ndio nitakuja kumaliza.
Wanakubaliana hivyo.
Part 222 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
Kama ulipitwa na kesi ya LISSU jana basi @iswahilinews wamekuwekea simulizi yote kwa njia ya SAUTI.
Hii nzuri sana kwa ambao wanakuwa bize hawana muda wa kusoma, tenga dakika zako 45 sikiliza mwanzo mpaka mwisho ilivyokuwa jana.
REPOST 200