AV MEDIA Co LTD an Event & AudioVisual Production Company. Radio&TVC Production, Events Planning, Graphics, Billboards, Posters Enquiries: [email protected]
Msanii wa Hip Hop Bongo, Country Boy ametangaza kukamilika kwa kolabo yake na Rapa Emtee wa Afrika Kusini.
Ngoma hiyo, 'Alright' ni miongoni mwa ngoma tatu ambazo zipo kwenye mipango ya kutoka hivi karibuni.
#Tanzania#zanzibar@countrywizzy_tz@emteerecords#SouthAfrica
African acts that have won the BET Best International Act award #BETAWARDS
• Davido (2018) 🇳🇬
• Burna Boy (2019, 2020, 2021) 🇳🇬
• Tems (2022) 🇳🇬
• Burna Boy (2023) 🇳🇬
• Tyla (2024) 🇿🇦
Ni taarifa ambayo nilikuwa naifahamu, lakini moyo tu ulikuwa unagoma kukubaliana na ukweli, ni kitu ambacho nilijidanganya kuwa hiyo siku wakimpost sitoumia ila sio kweli, nimeumia sana na huu usajili, niliamini nimeshazoea ndani ya mwezi mzima niliishi nikifahamu ila nilipoona post leo nilishika ganzi.
Hutokea pale Mchezaji bora kuwahi kutokea kwenye historia ya huu mpira wa Tanzania, Rafiki yako na umeishi kuyaona matukio yake bora uwanjani anaondoka klabuni, iliwahi kunitokea hii kwa Eden Hazard, Emmanuel Okwi na leo imejirudia, ndio football ni sehemu ya furaha na maumivu makali sana.
Suala wala sio kwenda Yanga bali hii picha inajirudia kichwani mwangu kuwa wana CHAMA Technician, wana AZIZ Technician, wana PACOME Ball Dancer, wana Maxi Nzengeli Engine ya Scania na Wana AUCHO The Tank kwenye kiduara, halafu mbele una DUBE The Baby Face Assasin, hii ni simulizi ya kutisha sana.
Hii imeuma sana hii, BORN RED MAESTRO Ndio umezaliwa kuwa Mwekundu, BORN READY, yes umezaliwa kuwa tayari, na upo tayari kwa hii changamoto mpya, all the best Baller🫡! BORN RED, BORN READY ila asibadilike Mtu kwenye ule msimamo wa huyu ndie GOAT wa Ligi Kuu hii, kila Mtu abaki na upande wake ule.
HII IMENIUMA VIBAYA MNO.
VISIT MOROGORO🇹🇿
Msanii wa Hip Hop Bongo, Dizasta Vina ametangaza ujio wa albamu yake mpya ambayo inatarajiwa kutoka Januari 6, 2024.
Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa yake kwa umma, kabla ya albamu hiyo, zitatoka ngoma kadhaa za utangulizi.
cc @dizastavina
Wasanii wa Bongofleva, AY, Alikiba na Joh Makini wanaandaa wimbo wa pamoja.
"Usiku wa jana jikoni na wabobezi AY x Alikiba x Me, produced by Taz Goemi who's ready?" ameandika Joh Makini.
cc @AyTanzania@OfficialAliKiba@JohMakini
Staa wa Bongofleva, Madee amesema anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kwa kila anachoomba anampa ila bado kimoja tu!.
"Kila nachokiomba ananipa, kasoro kimoja tu mpaka leo kinachelewa ila ipo siku naamini atanipa." Madee Insta Story.
#madee#Tanzania#SANA#yanga#Zanzibar
Diamond Platnumz na Harmonize wanataja nyimbo zao, 'Shu!' na 'Single Again' kama zenye mafanikio zaidi Bongo upande wa Amapiano.
Je, tunaweza kutumia vigezo gani vya kiufundi zaidi kujiridhisha ni kweli nyimbo hizo zimefanya vizuri kimataifa kama wanavyosema?.
Kwa nchi kama Marekani, wimbo kuingia Top 10 ya Billboard Hot 100 na hata kushika nafasi ya kwanza, unahesabika kama wimbo wenye mafanikio.
Albamu kuingia Top 10 ya Billboard 200 na hata kushika namba moja, inahesabika kama albamu yenye mafanikio.
Na ikitokea wimbo au albamu husika kuchaguliwa na hata kushinda tuzo za Grammy, kazi husika inatambulika kuwa na mafanikio zaidi!.
Je, kwa Tanzania ili wimbo tuseme una mafanikio tunapaswa kutazama vigezo gani?.
Kutoka kushoto ni Binti wa kwanza wa Beyonce na Jay Z, Blue Ivy Carter ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 11, huku akiwa ameshinda tuzo ya Grammy na BET.
Ni mtoto maarufu zaidi duniani baada ya Prince George na North West, mtoto wa Kim Kardashian na Kanye West.
Rapa na Mkurugenzi wa Bad Boys Records (1994), P. Diddy katika picha ya pamoja na Nelly mwaka 2004.
Utakumbuka kwa sasa Diddy ana utajiri wa Dola1 Bilioni, hiyo ni kwa mujibu wa Forbes.
Je, wakati huo ulikuwa wapi?.