Harakati za kulipwa haziwajibiki kwa ukweli.
Kipaumbele chao ni umaarufu, michango na ufadhili. Ukweli unapopingana na ajenda yao, hubadilishwa au kufichwa ili simulizi lao liendelee.#WanaharakatiMamluki
Exposing Paid Activists
JAMBO JIPYA LA KUJIFUNZA KWA SISI TULIONDAMANA
Wale tuliofiwa, tuliojeruhiwa, tuliokamatwa, ambao tuko sero na tumefikishwa mahakamani juzi tujiulize:
Mosi: Je tumewaona kina Mange Kimambi misibani, mahakamani, hospital au gerezani kutufariji? Kuna nini wametusaidia zaidi ya kudai watashitaki ICC na EU?
Pili:Unadhani wanatuonaje kutuambia tuandamane tena wakati tumeshakufa, hatujui kama tutakuwa tumepona majeraha au mkono wa dola utakuwa umeshatuachia? Si wanatuona hamnazo na mbumbumbu Mzungu wa reli?
Tatu:Je mimi niliyesalimika juzi unadhani ananionaje kuniambia tarehe 9 Desemba niandamane tena wakati niliponea chupuchupu kwenye kifo juzi? Si kama tu wanatulinganisha na mbuzi wa kafara? Si unajua sasa kuwa wao hawataandamana? Je si sasa pia unajua askari hawatumii fimbo kutuzuia kuchoma mali za umma na mali za masikini wenzetu?
Nne:Je unajua tuliyemchomea gari, tukapora duka lake ana hasira kiasi gani na sisi? Unadhani hiyo tarehe 9 Desemba atakuwa mikono tupu? Hatakaa na bastola au rifle au mkuki wa sumu?
Tano:Je unajua safari ijayo serikali haitakubali tena tuchome miundo mbinu iliyoijenga kwa gharama kubwa ya kodi zetu? Kama juzi iliweza kutuua sisi majambazi, wahalifu na vibaka unadhani hiyo 9 Desemba itatuacha? Mnategemea raia wenzetu wasikitike tukiuawa wakati tunachoma huduma ya usafiri?
Sita: Unadhani kuchoma miundombinu,na kuiba ndio njia sahihi za sisi kudai haki zetu?
Tusisubiri tukanywe na mama zetu kwa ule wimbo wa asiyesikia la mkuu . Tujikanye wenyewe kabla hatujapata balaa.
Watu wameshasema hawataomboleza tena tukiuwawa mara ya pili kwa uhalifu na vurugu maana wanaamini hatuandamani bali sisi ni waporaji na vibaka kama vibaka wengine tu.
Kwa kifupi taifa haliwezi kuvumilia uhalifu, uasi na uvunjifu wa amani na uhalibifu wa mali za umma na binafsi kwa kisingizio cha kudai haki kupitia mgongo wa demokrasia.
Alamsiki
Tawasifu ya Rais wa pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Ali Hassan Mwinyi, iitwayo 'Mzee Rukhsa: Safari ya Maisha Yangu' itazinduliwa tarehe 8 Mei 2021. Kitabu hiki kimebeba simulizi za maisha yake binafsi na safari yake ya uongozi #MzeeRukhsa#TawasifuZaUONGOZI
Kwa masikitiko makubwa tarehe 17th March 2021, saa 12 jioni tumempoteza Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli ambaye amefariki kwa maradhi ya moyo katika hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.
@DrHmwinyi Mungu akupe subra kiongozi wetu mwema ndani ya mwezi mmoja umeondokewa na mashujaa wawili wakubwa mungu akuongoze vyema katika hili na jingine@DrHmwinyi
@TolbertVitalic2 Mtu hana mabaya matupu na mema atakua nayo japo machache huenda hayakua mema kwa upande wako lkn kwa upande wa mwngn yamekua mema kwa mujibu ulivomgusa wema ule