Misa za kingereza zinanipiga sana KO!!
Wataniua hawa!!
Ile nasadiki ilivyo ndefu vile, kwa kiswahili tu inachosha…..ndo uichape kwa Yai!!
So ninachofanya wao wakisali kingereza mimi nasali kwa kiswahili kimoyomoyo!!
Shida kishwahili kirefu sana, wao wameshamaliza Ameen!!
Mimi ndio niko kwenye Nasadiki kwa roho mtakatifu……😌
Mwanzoni mapenzi yanavyo anza unaweza sema huyu ndiyo ametumwa na mungu, ila kadri siku zinapozidi kwenda ndiyo unagundua mungu hajui chochote kuhusu hayo mambo yenu 😅
Kwenye Sheria kuna somo linaitwa “CRIMINALOGY & PENALOGY”. Moja ya MISINGI ya somo hili ni kwamba; HUWEZI KUFANYA UHALIFU BILA KUACHA ALAMA. Sasa angalieni hapo 👇, “PETROL STATION” inahusiana vipi na UKATOLIKI?😂😂
Anaandika Askofu Bagonza (PhD)
"POLISI NA “WAKATOLIKI”
1. Nalazimika kuwapongeza Polisi wetu kwa ukomavu wao na ustaarabu wa kutozuia maandamano ya “Wakatoliki” walioenda kueleza hisia zao kwa Balozi wa Papa hapa nchini.
2. Nachukulia uvumilivu wao kama ishara ya kuacha kupambana na maoni ya watu na hisia zao. Basi wafute hata kesi za Mzee Mwandambo aliyekamatwa kwa kueleza hisia zake za kidini.
3. Kumbe, msimamo huu wa Polisi ulianza mapema pale walipomvumilia kiongozi aliyesema atakata vichwa vya watakaoandamana. Shikilia hapo hapo Polisi, jizuie kuingilia uhuru wa watu na maoni yao.
4. “Wakatoliki” hawa wasiojua kusoma vizuri walichokiandaa; walioamua kumwimba “Mwamba ni Yesu” badala ya Bikira Maria Mlinzi wa Taifa letu, na waliosahau kuwa Baba Mtakatifu wa sasa anaitwa Papa Leo wa 14; wametimiza haki yao ya kikatiba.
5. Watakapokuja Wakatoliki halisi wanaojua kusoma na kuvaa kwa heshima mbele ya Balozi wa Papa, wakasoma tamko lao kuwataka Polisi wamkamate aliyempiga Fr. Kitima, na wamlete aliyeteka mapadre na kuwadhalilisha, akawavisha wake za watu mavazi ya kitawa ili waonekane ni watawa walioshika bendera za vyama nk - hawa Wakatoliki wakiandamana, polisi kuweni wavumilivu kama mlivyokuwa wavumilivu kwa “Wakatoliki” hawa.
Sisi Wajaluo tunaamini kuwa chuki dhidi ya Ukatoliki inayoendeshwa kwa mikakati mibovu, ina nia mbaya dhidi ya serikali kuliko ilivyo na nia mbaya dhidi ya Ukatoliki.
Kupigana na Ukatoliki ni lazima uwe na dini nyingine ndani yako inayokusukuma kupigana vita hiyo. Wajaluo “tusiotahiriwa” tunajiuliza hiyo dini ni ipi"?