Hivi maendeleo ni dhuluma? Maendeleo ni kutofuata sheria za manunuzi? Maendeleo ni ukamataji na utumbuaji wa kiholela unaofanywa bila kufuata utaratibu na sheria na watawala? Maendeleo ni kupigwa kwa wananchi? Basi kama haya ni maendeleo acha niyapinge tu 😊
#ChangeTanzania
Neno “sense of security” naweza kutafsiri kama kuhisi kama una usalama. Tutambue hiyo haiji na mali uliojilimbikizia, nguvu ya kiutawala uliyo nayo bali itaimarishwa na vitendo vyako vya kiungwana kwa watu wengi hususan kama kiongozi. Hakuna ulinzi dhidi ya hii #ChangeTanzania
Changamoto kubwa ya ulimwengu kwa sasa ni kwamba wenye akili hawataki kujihusisha na siasa, na hivyo wajinga wamepewa mamlaka ya kuwatawala wenye akili na wasio na akili @NabilTanzania1@MariaSTsehai@JamiiForums
Huyu ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Eng. Mussa Iyombe
Mzee mwenye uzoefu na msimamo - mtumishi wa umma anayejitambua akiwafunda maDC - wasimamie sheria na haki ie Rule of Law anayosema @fatma_karume
Hatakosa wale ndugu zetu kuja kumpinga
Lakini tutafika #ChangeTanzania
Baada ya kuhitimisha Operation yetu ya siku sita ndani ya hifadhi ya Ruvu Chini iliyoisha Jumamosi iliyopita salama na kufungwa na Mhe DC wa Kibaha. Jana Kisarawe tulipata heshima ya kupokea ugeni mkubwa wa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Ndg. Japhet Hasunga (mb).
Don't let other people's drama be your reality 🤗
Jikitie kuelewa tatizo ila tambua kuwa wapo watu ni mahiri wa kuunda matukio mpk ktk maisha binafsi, wakwepe utajikuta umepoteza muda wako
Kwa sasa kila mtanzania ahangaike kuhakikisha tuna utawala wa kisheria
#ChangeTanzania
Hakuna "milele" hapa duniani. Yenye uhakika duniani ni mabadiliko! Hata ukibisha, ukigoma, ukipambana huwezi kusimamisha mabadiliko. Hebu jaribu kubisha na kugomea uzee 😂😂, au bisha na gomea jua kutua, mvua kunyesha. Gomea mtoto kukua. Maisha ni mabadiliko #ChangeTanzania
Enyi watanzania wenzangu! Kulinda demokrasia; kukemea dhuluma; kupambana na uonevu si jukumu pekee la vyama vya kisiasa, vyama vya wafanyakazi, taasisi zisizo za kiserikali bali jukumu ni la kimoja wetu kama raia. Hakuna atakayekuja kukukomboa #ChangeTanzania
Kama umekaa kimya kuhusu uonevu, dhuluma, unyanyasaji eti unadai inahatarisha maisha yako, ajira nk. Ila unatarajia mwingine akusemee, apigwe, anyimwe fursa za kazi kwa ajili ya haki utakayofurahia wewe pia - basi usimlaumu siku huyo mwenzako akifuata mfano wako #ChangeTanzania
@DaudiMitimingi@MariaSTsehai KATIBA ipi inayolindwa kipindi Cha Sasa?! Nadhani kinachotekelezwa kwenye katiba kwa kipindi hiki ni uwepo public holiday tu.
Kwenye zama hizi kupata mtu mwaminifu ni nadra sana, inasikitisha unapoteza marafiki kwa sababu ya kuwakopesha ubaya zaidi umemsamehe ndani ya moyo wako lakini hawapokei simu wala kujibu message, roho inauma ukipoteza rafiki kwa ajili ya hela. Urafiki > Pesa.
Sio lazima ufanye kila kitu ambacho wengine wanafanya ili 'utoshe' kwenye jamii, mara zingine kuepukana na matarajio ya watu ndio inakua chachu ya furaha katika maisha yako.
@SKubenea@MariaSTsehai Dhana ya ubaguzi, chuki, ubinafsi, kutojali kusikiliza HOJA za wengine kunaharibu Taasisi. Ukiwa mroho usiwe mchoyo. Hamahama yote hii je ni kesi ngapi zilizothibitisha mtu kanunuliwa kweli?! (Hakuna),kutoridhika na kile apatacho sehemu moja kunamuhamisha. (Huyu ni maskini.)
(Wataulizwa waliouhukumiwa adhabu) "kwani hawakuwajia Mitume miongoni mwenu wakiwasomea Aya za Mola Wenu na kuwaonya kukutana na siku yenu hii"? (siku ya malipo).
Quran 39:71