Kila kitu mahakamani ukikosea unaadhibiwa. Mfano kesi ya mahakama ya mwanzo ukifungua ya wilaya unakutana na pingamizi la kisheria, ukikosea taratibu vilevile, unaweza tozwa gharama za kesi( Bill of Costs) ndio maana unahitaji muongozo wa wakili anayejua sio kila jambo utalijua.
Kujitetea bila wakili ni kama kuingia vitani bila silaha. Sheria ni ngumu, na taratibu za mahakama ni changamato kuzijua zote. Kumuajiri wakili ni hatua ya bora kuhakikisha unalindwa kisheria, unapata haki yako, na kila hatua inafanyika kwa njia inayofaa.
Unaweza ukawa unatoa maelezo ya kujitetea mahakamani,ukijua yanakufanya kutokuwa na hatia kumbe ndio unajifunga mwenyewe na maelezo yako, kujua kitu gani cha kusema na wakati gani na kitu gani hutakiwi kuzungumzia kabisa ni fundi wa kisheria muhimu sana. Tumia wakili itakusaidia
Written Statement of Defence(hati ya utetezi wa madai) ni hati rasmi ya mdaiwa inayojibu madai ya mdai, ikieleza ukweli, hoja za kisheria, na ushahidi wa kupinga madai, ikiwa ni sehemu ya utetezi mahakamani. Hii ni kwa Mujibu Civil Procedure Code Cap 33.
Mediation ni mchakato wa kutatua migogoro kwa njia ya amani kupitia msuluhishi. Inafanyika mahakamani, na pande zisipohudhuria, uamuzi wa upande mmoja unaweza kutolewa. Makubaliano yanapotokea, hutumika kama hukumu . Mediation ni mchakato wa lazima Civil Procedure Code Cap 33
"Shaka(Hisia) pekee, hata ikiwa kubwa kiasi gani, haiwezi kutosha kuthibitisha hatia ya mshtakiwa. Sheria inahitaji ushahidi thabiti ili kumtia mtu hatiani kwa kosa lolote." Joseph Ngonyani vs Republic (Criminal Appeal No. 35482 of 2024) [2025]
Kukazia hukumu ni mchakato wa kisheria unaofanywa ili kuhakikisha utekelezaji wa hukumu iliyotolewa na mahakama. Mara baada ya hukumu kutolewa, pande zote katika shauri zinatarajiwa kutekeleza hukumu hiyo kwa hiari.
Ukishindwa kesi ya madai unalipa gharama za kesi (Bill of Costs) ni nyaraka rasmi inayowasilishwa mahakamani au kwa mamlaka husika ikionyesha gharama zote ambazo upande mmoja (aliyeshinda kesi) katika shauri la kisheria anadai kulipwa na upande mwingine(aliyeshindwa kesi).
Ulimwengu hautakuhukumu kwa sura yako ilivyo(mbaya au nzuri) rangi yako (mweupe au mweusi), wala kimo( yaani mfupi au mrefu) bali kwa matendo na matokeo ya shughuli zako. Yaani unazalisha nini na unawatendea watu nini? Ni mabaya au mema.
Wanafunzi wa kiume wa form 2 wawili walikutwa na wanafunzi wa kike wawili form one wote wakishiriki ngono. Wote chini ya miaka 18. Je hao wa kiume wanakosa gani, adhabu yao ni nini? Nasoma comments na nitazijibu
Mkataba wa million 100 unataka kumpa wakili 100,000 wengine hawakatai lakini atatengeneza mkataba wa page moja, ukitokea mgogoro yeye ndio material witness ( anaanza kukupiga chenga haji kutoa ushahidi) unaanza kutukana mawakili kuwa sio waaminifu.
Unaenda kwa wakili wa kwanza kwa issue yako anakuambia million 3, unaenda kwa wakili wa pili anakuambia million 2, unaenda kwa wakili wa tatu jambo hilohilo unaambiwa 500,000. Unampa wa 500,000 anachukua then mahakamani hafiki, wakati wa kufile nyaraka haandai.Unaanza kulalamika
Baada ya kumuwekea mtu dhamana, huyo mtu akatoroka mfano, na wewe huna mali ya kuuza kulipia kiwango cha pesa ya dhamana kilichowekwa basi kwa mujibu wa Sheria wewe ndio utatakiwa kufungwa. Nyongeza ya III Sheria ya Mahakama za mahakimu
Mtu unamdai 300,000 bado unataka na kuweka wakili😀😃😃😃😃. Angalia kesi ya kuku usiuze ng'ombe,
Kesi zingine simamieni wenyewe. Wakili atakuongoza na kukushauri jinsi gani ya kufanya.
Kama ni mkataba wakili ameushuhudia bhasi ikitokea mgogoro mahakamani, huyo wakili aliyeshuhudia ni muhimu kumleta kama shahidi muhimu(material witness) ukishindwa kumuita unaweza ukapoteza kesi kwa sababu unakuwa umeshindwa kuthibitisha kesi yako/madai yako.
Offa ya mwisho wa mwaka Usajili kampuni, jina la biashara kwa nusu bei usichelewe. Haitatokea tena hii ni kwa watu 10 wa mwanzo. Utapata ushauri pamoja na kuandaliwa nyaraka zote za usajili. Wale wanataka kuandaliwa nyaraka wasajili wenyewe tunawaandalia.
Baada ya kumuwekea mtu dhamana, huyo mtu akatoroka mfano, na wewe huna mali ya kuuza kulipia kiwango cha pesa ya dhamana kilichowekwa basi kwa mujibu wa Sheria wewe ndio utatakiwa kufungwa. Nyongeza ya III Sheria ya Mahakama za mahakimu