Kuna tofauti kati ya marafiki na watu sahihi.
1. Rafiki anaweza kuwa mtu yoyote
2. Mtu Sahihi ni Mtu Ambaye Anaendana na mwelekeo wa maisha unayotaka kujenga.
Si kila rafiki ni mtu sahihi kwako.
Na si kila mtu sahihi lazima awe Rafiki yako wa karibu.
USICHANGANYE
FOCUS in yourself
1. Jiheshimu kabla ya kutaka kuheshimiwa.
2. Jipende kabla ya kutaka kupendwa.
3.Jithibitishe kabla ya uthibitisho kwa wengine.
4.Timiza ahadi zako kama unavyotimiza ahadi za boss wako.
Kila kitu kinaanza kwako.
LOCK IN.
Anko
"Nilishawahi kuona Funza Kwenye Embe, Nikamwona kwenye Papai.
Lakini Sijawahi kumwona kwenye Limao.
Wakati Mwingine Kuwa Mtamu Sana Ndiko Kunakokufanya Uliwe.
Shule ilitudai Akili
Mitaa inatudai Mafanikio
Usitambie Elimu,Mitaa inataka Pesa
Mtaa haujali unajua kias gani;Mtaa unataka kuona nin unafanya kwa kile unachojua
Elimu na Pesa si Maadui.Elimu ni Chombo,Pesa ni Matokeo.Tatizo Si Elimu;Tatizo ni Elimu isioweza kutengeneza Thamani
Mungu huanza kuwapima watu kwa mambo madogo sana kabla hajakupa vikubwa. Ukiomba milion 10 ataanza kukupa lakini 100,000 akupime. Kama ilivyo kanuni yake
Luka 16:10
[10]"Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia..."
Kadri unavozidi kuishi,unagundua kua si kila jambo linaweza kutatuliwa kwa Nguvu,Pesa,au Ujanja wa kibinadamu.Kuna Watu waliumizwa kimyakimya lakn Haki yao ikasimama.Kuna waliodhulumu wakidhani hawatawahi kulipwa,lakn Maisha yakawajibu.
Sababu
MUNGU YUPO—na ndie Muamuzi wa mwisho
Kutaka Kuonekana Tajiri Kumewafilisi Watu Wengi Zaidi Kuliko Umaskini Wenyewe. Kuishi kwa Ajili ya Macho ya Watu ni Biashara ya Hasara. Ila Hakikisha Unaishi Ndoto Zako bila Drama wala kufakefake, Be you👊…!!
Kila mtu anapitia changamoto ambazo wengine hawazijui.
Sote tunajaribu kutengeneza maisha yetu kwa matumaini & hofu.
Kuoneana huruma na kusaidiana sio jambo la hiari, ni jambo la muhimu kwa maisha yetu ya kila siku kama binadamu, Akikisha Unasaidia hiyo ni hazina na utalipwa👊.
Maamuzi Yatakayo Badilisha Maisha Yako:
1. Kuamka mapema
2. Kujifunza kila siku
3. Kuheshimu muda
4. Kufuatilia mambo yako
5. Kutoogopa kufeli na kuanza upya
6. Kuchagua marafiki mnaofanana maono
7. Kuweka akiba na kuwekeza kwa nidhamu
8. Kulinda afya yako ya akili na mwili
Haya endelea kumwendekeza kila akikukosea wewe ndo unaomba msamaha kama ndo ulikosea.
Sometimes mahusiano yanahitaji roho ngumu acha kujishusha ovyo ovyo inatakiwa uchukue uamzi mgumu huku ukitambua huyo hakufai katika maisha yako.
Pangusa mikono na uende zako, utanishukuru.
Ukiona kila ukimshirikisha rafiki ako AU rafiki zako jambo lako halifanikiwi🙌sasa wewe jaribu jambo lingine bila kumshirikisha Kama likifanikiwa PIGIA MSTARI😶Sijakwambia uachane nae URAFİKİ ila jiulize je! Anafaa kuendelea kuwa Karibu yako ?
Wakati mwingine Mungu hukuvua kila kitu ili kukuonyesha kwamba bila watu, pesa, au sifa — bado unaweza kusimama. Usikate tamaa unapovuliwa, kuna nguo mpya inashonwa. ✍️
Kwenye Dunia ya Mahusiano na Ndoa. Wanawake Wanaenda Kwenye Kesho yao, Wakiwa Hawajamalizana na Jana yao.
Ogopa sana anko,Ishi na Mwanamke kwa Akili Mno