⚔️;
Tanzania Communication Regulation Authority (TCRA) has suspended Wasafi Television from broadcasting for a period of 6 months, Starting today, January 5.
MAHAKAMA yamwondolea Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya Mama Lucy Emma Mutio, Dk Regina Musembi madai ya ulanguzi wa watoto baada ya mwendesha mashtaka ya umma kusema uchunguzi haujawahusisha na uhalifu huo.
FIFA:Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF),Ahmad Ahmad amefungiwa kujihusisha na soka kwa miaka 5 na kutozwa faini TZS milioni 463.8 na FIFA kwa kukiuka kanuni za maadili. Ahmad amekutwa na hatia kutoa na kupokea zawadi kinyume na taratibu na matumizi mabaya ya fedha.
MTU mmoja alipigwa risasi za moto na kujeruhiwa wakati wa wizi katika Mlima Mall kando ya barabara ya Thika.
>Kiasi kisichojulikana cha pesa zilizoibiwa, DCIO wa Kasarani Jack Owino anasema.
#UGANDA.
TAKRIBAN watu 16 waliuawa katika siku mbili za ghasia zilizozuka kati ya vikosi vya usalama na wafuasi wa mbunge aliyezuiliwa Bobi Wine, polisi ya Uganda inasema.
#EACC:YAANZA uchunguzi juu ya madai ya mwenendo mbaya wa Waziri Magoha.
👉🏾Yamuita mkurugenzi wa Elimu Kaunti ya Uasin Gishu Gitonga Mbaka kurekodi taarifa hiyo kesho.
HARAMBEE STARS WAWASILI NCHINI:
👉🏾Matumaini yao kufuzu michuano kuwania kombe la Afrika mwakani yadidimia.
👉🏾Hii ni Baada yao kupata kichapo mkononi mwa Wakomoro hiyo jana jijini Moroni.
LILONGWE:
👉🏾Serikali ya Malawi imeishutumu Afrika Kusini kwa kuzuilia ndege yake ya urais kwa masaa kadhaa bila sababu yoyote.
👉🏾Rais Lazarus Chakwera alikuwa ziarani Ijumaa, lakini kuondoka kwake kulicheleweshwa kwa sababu za usalama.
Wafuasi wa Mwanamuziki Bobi Wine anaegombea kiti cha Urais nchini Uganda mapema leo asubuhi walilazimika kuvuka bwawa huko West Nile baada ya JESHI LA POLISI kuzuia njia yao ya kuelekea mkutano wa mgombea huyo.
(📸@DailyMonitor)
MZOZO WA TIGRAY:
>ETHIOPIA YAKANA madai ya mazungumzo kuwezekana na TPLF yatakayo ongozwa na Uganda.
>Kikosi Kazi cha Dharura juu ya Tigray kinasema ripoti sio sahihi.
SIJALAGHAI!
>Mwanamuziki Mejja wa Kansoul akana madai kwamba alimlaghai mwanablogu.
>Aonya mashabiki wake kuwa ana akaunti moja tu ya mtandao wa kijamii na ni kwenye Instagram.
MZOZO WA #TIGRAY:
>Karibia Watu 25,000 wanaokimbia mzozo katika eneo la Tigray nchini ETHIOPIA wamevuka na kuingia nchi jirani ya Sudan, shirika la habari la Jimbo SUNA limeripoti.
>UN yasema inafanya kazi ya kuwapatia makazi.
#HABARI:
‘‘Waasi walikata vichwa vya watu katika mkoa wa Cabo Delgado wa Msumbiji katika msururu wa mashambulio ambayo yalianza Oktoba 31 na yalidumu kwa siku kadhaa’’, shahidi aiambia shirika la CNN, akithibitisha ripoti za mapema za vyombo vya habari vya serikali.