"Kujibu kunaweza kuamsha hasira zilizolala, kunaweza onyesha ujinga wako, kunaweza toa taarifa za ziada, kunaweza kukunasisha kwenye mtego, na kunaweza kuhitimisha dhana fulani watu walizonazo juu yako. Kutokujibu hakumaanishi huna majibu, bali kwaweza kuwa kipimo cha busara."
"Mtoto mjenge kabla ya kumjengea. Ukihangaika sana kumjengea bila kumjenga yeye mwenyewe, hatakuwa na uwezo wa kuviendeleza ulivyomjengea. Ukimjenga yeye, hata usipomjengea, atajenga vyake." ~Togolani Mavura.
"Sote katika nyakati fulani fulani katika maisha yetu hata tuwe imara kiasi gani tunaweza kuyumbishwa na majaribu na mitihani. Hakikisha una mtu anayejua kulirejesha dishi lako katika masafa yake ama sivyo utachanganya chaneli. Maisha haya kila mtu na 'mrekebisha dishi' wake!"
"Katika uongozi ni muhimu sana sana kutambua ni wakati gani una cheo tu, wakati gani una mamlaka tu, na wakati gani una vyote viwili, yaani cheo na mamlaka. Muhimu zaidi, kutambua nafasi yako na ukomo wa unachoweza kufanya katika mazingira yote hayo matatu!" ~Togolani Mavura.
Kinachoniumiza zaidi ni kwamba hukuondoka wakati nilipokuwa naogopa kukupoteza, wala hukuondoka wakati ambao nilikuwa nakutazama kwa jicho la hofu.
Badala yake umeondoka wakati ambao tayari niliishinda hofu yangu, na kwa mara ya kwanza niliamini kwamba wewe ni wangu wa milele.
"Kuna watu ni daraja la kuivusha riziki kwa wengine na kuna watu ni tuta la kukinga riziki isiwafikie kirahisi wengine. Ukiwa na nafasi ya kumsaidia au kumuinua mtu mmoja tu, msaidie na muinue yule ambaye kwa kuinuka kwake atakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuinua wengine."
��عض الأبواب لا تُفتح بالقوة، بل بالصبر. وما كتب لك سيصل إليك في الوقت الذي يكون فيه خير لك
Baadhi ya milango haifunguliwi kwa nguvu, bali kwa subira. Na kile kilichoandikwa kuwa chako kitakufikia wakati ambao utakuwa ni bora zaidi kwako.
"Kuna watu wamebebwa na jina la ukoo, kuna wale ambao wao ndio wamelibeba jina la ukoo wao. Wale wa kwanza wana ukoo wa kuuangukia na kuwaokota wakianguka, hawa wa pili wakianguka wanauangusha na ukoo mzima. Ukiwa kundi la pili wajibu mabegani mwako ni mkubwa zaidi. Usijisahau!"
"Bila kuwasaidia wao kufika hapo ulipo, wewe hutatoka kufika kule unapopatamani kwenda. Inabidi apatikane wa kujaza nafasi yako ya sasa ili nafasi yako ya mbele ifunguke." ~Togolani Mavura.
#NgojaNikwambie
Furaha ya kweli hupatikana ndani ya NAFSI yako bila kujali kitu kingine chochote. Hakuna kitu kinachoweza kuinunua furaha hiyo, hata ukiwa na pesa zote za DUNIA hii.
Kimsingi, kile tunachokitafuta huwa kiko ndani yetu, si NJE YETU. Unaishi ndani, kabla ya NJE!
"Sote ama ni wahanga au wahanga watarajiwa wa magonjwa ya afya ya akili. Maisha yetu yamezungukwa na sababu nyingi za kutukatisha tamaa na kutupa msongo wa mawazo. Daima jitahidi kutopoteza mambo mawili, kwanza, tumaini, na pili, watu sahihi katika mduara wako (support system)."