VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche leo Oktoba 13, 2026, amezindua rasmi ofisi ya chama hicho Kanda ya Kaskazini, iliyopo Kata ya Elerai mkoani Arusha.
Ofisi hiyo inalenga kuratibu shughuli za chama katika Kanda ya Kaskazini inayojumuisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga, pamoja na kurahisisha utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya kichama.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CHADEMA, akiwemo Godbless Lema, Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, pamoja na Amani Golugwa, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara.