VIDEO:
Askofu wa Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe, Dkt. Benson Bagonza, amesema vijana wengi hubaguliwa katika michakato ya kisiasa kwa kulazimishwa kuwa wanachama wa vyama vya siasa huku akisema kundi la vijana wasio na vyama vya siasa ni kubwa zaidi kuliko wenye vyama vya siasa.
Amebainisha hayo Julai 9, 2026 alipokuwa akichangia kwenye Kongamano la Demokrasia lililofanyika Zanzibar.
Amehoji kuwa ikiwa kushiriki siasa ni lazima kuwa ndani ya vyama vya siasa ni ipi nafasi ya vijana walio nje ya vyama hivyo.
Ameongeza kuwa kwa kutokuwa wanachama wa chama chochote, vijana hao wanapoteza uhalali wa kuchaguliwa kuwa viongozi huku wakibaki na haki ya kuchagua pekee.
Amesema katika mazingira ambayo hakuna uhakika wa Kura zao kuheshimiwa inapelekea pia kupoteza haki ya wao kuchagua akisema katika mazingira hayo kunauwezekano wa rushwa kila eneo.
Aidha amesema kutokana na mazingira hayo vijana wengi huamua kutopiga kura huku wale walio ndani ya vyama vya siasa wakipoteza uhakika wa kura zao kuhesabiwa hata baada ya kuchaguliwa.
CHADEMA imehitimisha salama vikao vyake vya Kamati Kuu vilivyofanyika mjini Kigoma.
Maazimio yaliyopitishwa katika vikao hivyo yatatangazwa rasmi na viongozi wakuu wa chama kwa wakati utakaotolewa.
Kwa sasa, msimamo na kipaumbele chetu ni mambo mawili tu: Uhuru wa Mwenyekiti Tundu Lissu na Katiba Mpya.
Hii ndiyo dira yetu, ndiyo ajenda yetu kuu, na ndiyo mwelekeo tunaopaswa kuusimamia kwa umoja na uthabiti.
Vijana wajibu wetu ni ule ule kulinda Chama hiki na viongozi wake kwa wivu mkubwa. Ajenda za Chama zitapiganiwa kwa nguvu zote.
#KatibaMpyaFreeTunduLissu
Maazimio ya kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika Kigoma yatatangazwa hivi karibuni na viongozi wakuu wa chama. Nina matumaini kwamba yatatoa majibu kwa kelele na mijadala mingi iliyoibuka hivi karibuni. Hata hivyo, iwapo italazimu kutetea heshima yangu binafsi dhidi ya kauli mbalimbali za dharau na upotoshaji, nitafanya hivyo kwa ufasaha. Nasikitika kwamba naweza kujikuta katika jaribu hilo, lakini heshima ya mtu si jambo la kupuuzwa.
Bila kuathiri maazimio ya Kamati Kuu yatakayotolewa na Viongozi Wakuu wa Chama napenda kuwahakikishia Watanzania wote kuwa CHADEMA ni imara sana leo. Ni chama kilichojitoa kuikomboa Tanzania kutoka mikononi mwa Mamumiani wa CCM.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Kaskazini kimewasimamisha viongozi wake wawili Abubakari Mashambo, aliyekuwa Katibu wa Jimbo la Bumbuli na Joseph Mwakidasi, aliyekuwa Katibu wa Wilaya ya Muheza, zote za Mkoani Tanga kwa tuhuma za kukiuka Kanuni za Maadili ya Viongozi wa chama kwa kutoa matamko kupitia vyombo vya habari dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa Taifa (Bara) John Heche bila ya kufuata taratibu za chama.
Kwa mujibu wa taarifa mbili zilizotolewa na Katibu wa Kanda ya Kaskazini Yohana Kaunya, viongozi hao wanatuhumiwa kukiuka Kanuni 10.1(viii), 10.1(ix) na 10.1(x) za Katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006, Toleo la 2019, kwa kutoa tuhuma zisizo na uthibitisho na kuzisambaza kupitia vyombo vya habari badala ya kutumia vikao halali vya chama.
Taarifa hizo zinaeleza kuwa Mashambo na Mwakidasi wametakiwa kuwasilisha uthibitisho wa tuhuma zao ndani ya siku 14 tangu walipopokea taarifa rasmi, kwa mujibu wa Ibara ya 6.3.6(c) ya Katiba ya CHADEMA, huku wakisubiri mchakato wa kinidhamu kukamilika.
Aidha, kusimamishwa kwao kutadumu hadi Kamati Tendaji ya Kanda itakapokamilisha uchunguzi na kutoa uamuzi wa mwisho kwa mujibu wa Ibara ya 6.3.6(v) ya Katiba ya chama. Katika kipindi hicho, hawataruhusiwa kutekeleza majukumu ya nafasi walizokuwa wakizishikilia wala kuzungumza au kutenda kwa niaba ya ofisi hizo.
Hatua hiyo inakuja wakati CHADEMA ikiendelea kukabiliwa na migogoro ya ndani inayohusisha baadhi ya viongozi wake, huku uongozi wa Kanda ya Kaskazini ukisisitiza kuwa masuala yote ya kinidhamu yataendelea kushughulikiwa kwa kuzingatia Katiba, kanuni na taratibu za chama.
UKIZOEA VYA KUNYONGA HAYA NDO MADHARA YAKE.
Naambiwa NDUGU BASHITE huko kwenye Uchaguzi wa Kamati ya OLYMPIC Tanzania kapindua Matokeo ya URAIS hadharani.
Katuma watu wake kuhakikisha Mshindi hatangazwi.
Uchaguzi wenye wapiga kura 36 umezingirwa na Maaskari zaidi ya 10 wenye mitutu ya Bunduki.
Imagine kati ya wagombea watatu aliyepewa ushindi ni yule aliyepata kura Moja.
Naambiwa mwangalizi wa kimataifa ambaye ametokea UGANDA alibaki ametoa macho, anashangaa kila kitu, mwisho akawaambia "aibu kabisa hii" akaondoka.
Sasa jifikirie kama wanaweza uhuni huu mbele ya macho ya wageni, wakiwa peke yao si ndo hatari zaidi?
Tukiwaambia nchi imeoza na inahitaji overwhole mnaona kama ni chuki za wapinzani. Hebu ona nchi inavyofedheheshwa kwa mambo madogo kama haya.
Tuliwaambia mkishamalizana na upinzani mtaanza kulana wenyewe kwa wenyewe.
Haya, sie ya kwetu macho, tunajiandaa na 77 ya kesho.
Matokeo halisi ni haya hapa.
1. ANTHONY MTAKA KURA 29
2. HENRI TANDAU KURA 6
3. LEONARD THADEO KURA 1
MSHINDI WETU KWA MUJIBU WA VIBARAKA WA BASHITE NI NDUGU LEONARD THADEO.
Ukitaka kufahamu kiwango ambacho nchi yetu imeharibika ni pale unamsikiliza ‘Luteni Kanali’ wa JWTZ ambaye amepewa wadhifa wa kuwa Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano anatumia kauli mbiu ya kampeni za MaCCM, ‘Kazi na Utu’. Hii nchi imeharibika kiwango cha kutorekebishika kirahisi.
Ikumbukwe hii HOTUBA Baba ASKKFU aliitoa mwezi wa 8 kabla ya #OCTOBER29. in short chezea watumishi wenu wote mnao wamudu ila suala likifika kwa JASUSI huyu bana ni kuumbe kingine kabisa akiamua kunyooka ni BADMAN kweli kweli�
Makamu Mwenyekiti wa Bara, Mhe. @HecheJohn, pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Bara, Mhe. @amanigolugwa, wakisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Suez Dani Maradufu, Tarime Mjini.