Edwin Sifuna is a true son of Baba Raila Odinga and a real Kenyan patriot, who stood with him in good and bad times.
On this special day, we honor your courage, your consistency, and your unwavering dedication to the mwananchi.
Happy Birthday !
“History whispers before it screams.”
Historia ya dunia ina mifano mingi ya serikali au tawala zilizohusika katika mauaji ya halaiki dhidi ya raia wao au makundi fulani ya watu. Mara nyingi matokeo yake yalikuwa:
• kuporomoka kwa tawala,
• majeraha ya kizazi kwa kizazi,
• migawanyiko ya kitaifa,
• hukumu za kimataifa,
• au viongozi kuishi maisha ya hofu, uhamisho, au aibu ya kihistoria.
Baadhi ya mifano mikubwa ni hii:
1. The Holocaust — Ujerumani ya Nazi
Chini ya Adolf Hitler, serikali ya Nazi iliua takribani Wayahudi milioni 6 pamoja na:
• Waroma (Gypsies),
• walemavu,
• wapinzani wa kisiasa,
• na makundi mengine
2. Rwandan Genocide
Rwanda (1994)
Ndani ya siku karibu 100 tu, zaidi ya watu 800,000 waliuawa — hasa Watutsi na Wahutu.
Vyombo vya serikali, wanamgambo, na propaganda za redio vilitumika kuchochea mauaji.
Majirani waliuana.
Marafiki waliuana.
Jamii ilipasuka vibaya sana.
3. Cambodian genocide Cambodia 1975- 1979
Utawala wa Pol Pot uliua takribani watu milioni 1.5–2.
Wasomi, walimu, watu waliovaa miwani, viongozi wa dini, na yeyote aliyedhaniwa kuwa “adui wa mapinduzi” waliuawa.
Katika Cambodian genocide chini ya Pol Pot, utawala wa Khmer Rouge ulikuwa na mtazamo mkali sana dhidi ya “wasomi” na kile walichokiita ushawishi wa dunia ya kisasa au elimu ya Magharibi.
Ndiyo maana hata kitu kidogo kama kuvaa miwani wakati mwingine kilitafsiriwa kama “dalili ya usomi.”
Mantiki yao ilikuwa ya kikatili na ya kipumbavu:
* mtu anayesoma sana anaweza kuvaa miwani,
* mtu anayesoma anaweza kuuliza maswali,
* mtu anayefikiri kwa uhuru anaweza kuipinga serikali.
Kwa hiyo katika paranoia ya mapinduzi yao, hata:
• walimu,
• madaktari,
• maprofesa,
• watu wanaozungumza lugha za kigeni,
• watu waliokuwa na elimu,
• au waliokuwa wanaonekana “wa mjini”
walionekana kama maadui wa mfumo mpya.
Katika baadhi ya maeneo, watu waliuawa kwa sababu tu:
* walikuwa na vitabu,
* walijua lugha ya kigeni,
* walikuwa na taaluma,
* au walionekana “wenye akili nyingi.”
Miwani ikawa kama “alama ya kushukiwa.”
Hii inaonyesha hatari kubwa sana ya:
• siasa inayochukia elimu,
• mapinduzi yasiyo na mipaka ya sheria,
• propaganda inayogeuza kundi fulani kuwa “adui wa wananchi,”
• na mfumo unaoona kufikiri tofauti kama tishio.
Ni moja ya mifano ya kihistoria inayoonyesha jinsi hofu, chuki, na itikadi kali zinavyoweza kuondoa kabisa ubinadamu wa kawaida.
Cha kusikitisha ni kwamba wengi waliouawa hawakuwa wanajeshi wala wahalifu.
Walikuwa raia wa kawaida tu waliokuwa wamewekewa “label” ya kuwa hatari kwa mfumo.
Na baada ya miaka mingi, Cambodia iliendelea kubeba majeraha makubwa:
• upungufu wa wasomi,
• trauma ya kizazi,
• hofu ya kisiasa,
• na kumbukumbu nzito ya taifa lililowahi kugeuza wananchi wake wenyewe kuwa maadui.
4. Bosnian genocide
Katika vita vya Balkan miaka ya 1990, maelfu waliuawa kwa misingi ya ukabila na dini.
Mauaji ya Srebrenica massacre yalikuwa moja ya matukio mabaya zaidi Ulaya baada ya Vita Kuu ya Pili.
5. Stalinist purges
Soviet Union
Chini ya Joseph Stalin:
• mamilioni walifungwa,
• kuuawa,
• au kutoweka kwenye kambi za mateso (Gulag).
Watu waliishi kwa hofu kubwa.
Kukosoa serikali kulikuwa hatari.
Hoja kubwa ya kihistoria
Karibu kila mahali ambapo serikali au tawala zilifanya mauaji makubwa dhidi ya wananchi:
• ukweli ulijaribu kufichwa mwanzoni,
• propaganda ilitumiwa,
• watu waliogopa kusema,
• taasisi zilinyamaza,
• baadhi ya wananchi walitetea ukatili huo kwa sababu ya siasa au hofu.
Lakini baadaye:
• ushahidi ulitoka,
• historia ilizungumza,
• dunia ilihukumu,
• na majina ya viongozi wengi yakabeba doa la kihistoria milele.
Ndiyo maana mataifa yenye hekima hujenga:
• taasisi huru,
• mahakama imara,
• vyombo vya habari huru,
• na uwezo wa serikali kukosolewa bila kuiona jamii kama adui.
Kwa sababu damu ya wananchi inapomwagika bila haki,
athari zake zinaweza kulitesa taifa kwa vizazi.
Kwa nini kila mara.tunaongelea Oktoba 29 tu kana kwamba mauaji yalifanyika siku moja tu wakati wa maandamano? Mauaji hayakuendelea.katika siku zilizofuata bila hata harufu ya maandamano?
Wakatoliki na VIJORA wapi na wapi?! Yaani hakuna hata shati moja la UWAKA wala kitenge cha WAWATA?!
Sasa ngoja WAKATOLIKI wenyewe watoke wakiongozwa na MAPADRI na MAASKOFU kama walivyoandamana DRC mpaka Kabila akachemka.
NB: Hawa wote MALOFA pamoja na waliowatuma,matako yenu😎
Tarehe 3 Nov 2025, rais Samia Suluhu Hassan ameapishwa rasmi kuwa rais wa Tanzania baada ya ushindi wa kishindo wa 97.6% dhidi ya wapinzani wake kwenye uchaguzi mkuu uliotawaliwa na vurugu zilizosababisha maafa makubwa.
Lakini nini kilikuwa nyuma ya yote haya?
Nisome
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 125
Kwahiyo kwa kumalizia hoja hiyo ni kwamba shahidi huyu hana Competence ya kutoa hii nyaraka hapa Mahakamani.
Sababu ya nne ni Chain of custody.
Msingi wa hoja hii ni kesi maarufu ya Paulo Maduka na Wenzake 4 vs R Criminal Appeal No. 110 of 2007.
Ushahidi wa aina hii unahitaji uoneshwe kwamba kutoka mahali ulikoanzia mpaka unaletwa Mahakamani.
Kukiwa na break of chain of custody ushahidi haupokelewi.
Shahidi anasema kwenye ushahidi wake aliletewa hizo video na Michael gyumi.
Michael Gyumi alizitoa wapi??
Nakumbuka shahidi wa kwanza alisema ile memory card ilitokea Dodoma kwa mtu anaitwa P akaletewa Andrew churu na alisema kulikuwa na hati ya makabidhiano.
Hiyo hati ya makabidhiano mlileta mahakamani?
Andrew churu alimkabidhi peter Malugala
PW2 John kaaya akasema alimkabidhi Peter Malugala na alijaza PF 45 there is no documentation maana mashahidi hawajaleta hata moja.
Sasa Waheshimiwa kutokana na kesi tajwa hapo juu.
Chain of custody must always be maintained hawa Mapolisi wamemaintain kitu gani? Hakuna lolote.
Hiyo kesi niliyosema ya Paul Maduka
Maana yake ni kwamba Ushahidi wa aina hii unahitaji uonyeshwe kutoka mahali ulipoanzia paka kuletwa mahakamani unahitaji uthibitisho wa kinyaraka umepitia kwenye mikono gani.
Kesi hiyo ya Paul Maduka page 18 to 19 Mr Justice Edwin Rutakangwa anasema kapiga kiingereza hapa kuwa huo mlolongo inabidi usivunjike.
Kwahiyo Waheshimiwa Mahakama ya rufani baada ya Paul Maduka chain of custody should always be maintained it should not be broken.
Waheshimiwa Majaji hata PGO zimesisitiza hilo, Waheshimiwa majaji PGO 229 paragraph 8 inazungumzia Chain of Custody.
Na waheshimiwa Majaji nitawasomea inasema anaanza kusoma hapa anajaribu kuelezea umuhimu wa chain of custody hapa kwamba lazima ionyeshwe kuwa mlolongo wa kupokea kielelzo haujavunjwa au kielelezo kubadilishwa hapa.
Mhe. Lissu anasema kama hakuna chain of custody hakuna Ushahidi wa kuingizwa mahakamani kama hawajaestablish chain of custody hivyo ni rai yangu kuwa msikubali hizi video ziingie kama vielelezo katika mahakama yenu.
Mhe. Lissu amemaliza hivyo ni zamu ya Jamhuri kujibu sasa.
Ni kama wamechanganyikiwa hawaeleweki nani ajibu au wanataka kufanya nini? 😂
Wakili wa Serikali Mkuu Renatus Mkude anasimama na kujibu kuwa wako tayari kujibu hoja za Mh. Lissu lakini watatumia two hours. Majaji wanauliza hiyo two hours unamaanisha nini? 😂😂
Anajibu Wakili Mkude kuwa ni kutokana na hoja za Mshtakiwa alizosema lakini pia shahidi huyo ndo wa muhimu katika mzizi wa kesi hii.
Hivyo tunaomba two hours ili tusilipue katika kuisaidia Mahakama.
Kama itawapendeza tukaahirisha mpaka Jumatatu ni sawa pia Waheshimiwa Majaji.
Mhe. Jaji Ndunguru anasema,
Sasa sikiliza Wakili wa Serikali kimsingi tumeelewa uliposema tu habari ya masaa mawili ulimaanisha unaomba ahirisho hadi Jumatatu.
Mahakama kichekooo 😂😂😂😂
Kumbe hata Majaji wanajua janja janja za Mawakili wa Serikali.
Shauri linaahirishwa hadi Jumatatu saa tatu kamili asubuhi ambayo itakuwa ni Tarehe 20/10/2025.
Tukutane Jumatatu wapendwa,
Sasa ngoja nikanywe wine kidogo nikiwa nakusanya hizo nguvu za Jumatatu.
Mungu awabariki sana.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Oktoba 15, 2025.
Last time tuliishia part 101 so leo tunaendelea na
Part 102
Leo Tarehe 15/10/2025.
Mheshimiwa Tundu Lissu ameingia Mahakamani.
Amesimama Kizimbani anauliza Polepole amepatikana na Mama anasemaje si Balozi wake?
Majaji wameingia na Shahidi nae kama kawaida ameingia yupo hapa. Inspector wa Polisi John Kaaya.
Karani anasimama Criminal Session No. 19605 Jamhuri dhidi ya Tundu Lissu.
Iwapendeze naitwa Renatus Mkude Wakili wa Serikali niko na Job Mrema, Ignas Mwinuka, Harrison Lukosi, Winiwa Kasawa tunaiwakilisha Jamhuri. Na Mshitakiwa yupo. Lakini pia tuna jambo tunaomba kuiambia Mahakama.
Mhe. Lissu anasema na mimi niko tayari na pia nitakuwa na jambo la kuieleza Mahakama.
Renatus Mkude, tulipokea taarifa ya Msiba wa Msajili wa Mahakama Kuu kanda ya Shinyanga.
Tumekuwa na utaratibu wa kwenda kushiriki matukio kama haya na tulipanga kuhudhuria kwenye msiba huo kwa vile ni jambo la kibinadamu ilikuwa na rai yetu itakapofika saa tano twende tukamuage huyu ndugu yetu ili tuendelee kesho tena. Ni hayo tu.
Mhe. Lissu anasimama kwenye hilo mimi sina pingamizi lolote na ikiwapendeza wakienda kwenye huo msiba wanipelekee salamu zangu za rambirambi kwa wafiwa.
Lakini pia niwaeleze kuhusu watu waliokuwa wanazuiwa kuingia Mahakaman, nimesema sana jambo hili.
Kasoro juzi Jumatatu sikulizungumzia kwasababu niliambiwa wangeruhusiwa siku hiyo lakini walikuja wakazuiliwa hapo getini.
Kwa taarifa nilizonazo walichukuliwa na maafisa wa uhamiaji na baadae wakafukuzwa nchini ili wasiweze kuingia Mahakamani kushuhudia kesi hii.
Sasa waheshimiwa majaji hii ni mara ya tatu kwa watu wanaotaka kuja kuhudhuria mahakama hii kufukuzwa nchini.
Walianza na Ujumbe uliotoka Kenya ukiongozwa na Jaji Mkuu mstaafu wa Kenya, Willy Munyoki Mutunga.
Wakafuata Boniface Mwangi na Agatha Atuhire walikamatwa na kuteswa na kupelekwa mipakani na kutupwa.
Na sasa hili limetokea kwa raia wa Ujerumani na Marekani walioingia nchini kihalali kuja kutaka kuona kinaendelea nini.
Hii ni kesi kubwa kuliko zote ndivyo inasema Katiba yetu ni kesi inayo draw Regional and International attention.
Haya yaliyofanyika Kisutu tayari yapo kwenye Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa yapo katika mahakama za haki za binadamu na watu Afrika.
Kwahiyo haya sio mambo madogo kabisa. Mahakama inapoingiliwa inasababisha sintofahamu kwenye mfumo wetu wote wa haki jinai ndani ya Taifa letu.
Mwaka 1958 kulikuwa na kesi kubwa sana katika Mahakama ya Wilaya Dar es salaam Kivukoni ambayo ni Regina Vs Julius Nyerere na wenzake wawili mmoja wapo Robert na mwingine Rashid baldell.
Wakoloni wa kingereza did not dare kuzuia watu kwenda kushuhudia kesi ya kiongozi wao na wanaofahamu historia ya nchi hii Mwalimu alitetewa na Wakili kutoka Wingereza.
Wakoloni hawakukataza pia hawakupiga watu wasiingie Mahakamani.
Kesi ya Jommo Kenyata pia ilikuwa kubwa sana ambayo ilifanyika katikati ya Vita vya Maumau, Waingereza did not dare kuzuia watu kwenda kusikiliza the trial of Jomo Kenyata ilifuatiliwa.
Mwaka 1956 mpaka 1961 tulikuwa na kesi ya Uhaini Afrika Kusini imeelezwa kwenye Long Walk to Freedom, Kesi ya Nelson Mandela hakuna mtu aliyepigwa wala kuzuiwa kwenda Mahakamani, hakuna watu walioteswa ili wasiingie Mahakamani.
Sasa nchi hii baada ya miaka 64 ya Uhuru Serikali yetu na vyombo vya Ulinzi na Usalama inazuia watu wasiingie Mahakamani kwenye nchi ambayo sheria zinasema mahakama ni ya wazi.
Tunafanya mambo ya hovyo kuliko wazungu waliotutawala sisi hapa Tanganyika, walioitawala Kenya na wale wa Afrika Kusini sasa mimi niko Gerezani na Mahakama imeshindwa kufanya lolote.
Sasa ili isije kuja kusemwa baada ya mimi na nyie majaji kutoweka hapa Duniani kuwa nilikuwa kwenye dhambi ya watu ambao walinyamaza kimya mambo haya kutokea. Nimesema kutimiza wajibu wangu na sitaki dhambi ya kunyamazia uovu au maovu, naomba kumalizia hapo.
Part 103 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.