. @JamesMbowe4
Wanaharakati hawajatufikisha hapa. Tumefika hapa kwa kuwa kikundi kidogo cha watu kiliamua kufanya siasa za UDALALI na kutumika na MaCCM – wakahamia CHAUMMA kwa kupewa ahadi za uongo za madiwani, wabunge na halmashauri. Hizo ni siasa za UDALALI.
Kama kweli ungelikuwa unampenda Tundu Lissu kuliko hao wanaharakati, usingemkimbia wakati anachagiza ‘No Reforms, No Election’ kwa wananchi ili waelewe somo. Ulikimbilia CHAUMMA, ukagombea ubunge na husemi ulipewa kura ngapi. AROBAINI?
Kama wewe na wenzako mngelikuwa mnampenda Tundu Lissu kuliko hao wanaharakati unaowaona maadui, ungejaribu kutenga muda wako hata mara moja, kwenda Mahakamani, kumsalimia na kumuunga mkono katika kesi zake. Hujawahi kufika hata kwa bahati mbaya
Wanaomshtaki Tundu Lissu ni Serikali ya CCM. Hawa ni mabosi zenu. Hao ndiyo ambao wananufaika na TAL kuendelea kuwepo gerezani kwa makosa ya uongo na ulaghai ya uhaini. Tundu Lissu anajitetea mwenyewe na ameeleza Mahakamani anashtakiwa na CCM
CHAUMMA mlishindwa kumtaja mgombea wa CCM katika utapeli wenu wa kampeni. Mmeshindwa kutoa pole baada ya mashosti zenu (CCM) kufanya mauaji ya kutisha, mkahudhuria uapisho kambi ya Jeshi – tunaelewa, huwezi kusema CCM wanamuonea TAL
Wanaharakati wanatengeneza vipi pesa kupitia Tundu Lissu kuwepo gerezani? Michango? Familia ya Tundu Lissu imetoka hadharani na kufafanua aliyefanya utapeli ni nani na wametoa taarifa polisi, amekamatwa na hadi sasa yupo mahabusu. Hakuna agenda hapo.
Katika uchaguzi ndani ya CHADEMA tulipoamua kumuunga mkono FAM, tuliamini wagombea wote ni CHADEMA na atakayeshindwa, ataponya maumivu haraka na kuendelea na harakati. Imekuwa kinyume chake. MADALALI mmekuwa zaidi ya KIBAJAJI na NAPE
Mnafanya kazi ambayo MaCCM wamekuwa wakiifanya wakati wote, kushambulia CHADEMA na viongozi wake. Hii inatia mashaka kama mlikuwa wapinzani kweli wa MaCCM au mlikuwa marafiki wa maCCM katika rangi za CHADEMA. Ni kushindwa uchaguzi tu?
Mzee Freeman Mbowe akiwa gerezani kwa makosa ya uongo ya ugaidi, tulitenga muda, tukahudhuria na kuripoti kesi kwa miezi nane mfululizo. Tuliamini FAM siyo GAIDI. Alipotoka, alikwenda moja kwa moja IKULU. Alitukwaza. Lakini tuliamua kumuelewa.
Unafikiri hayapo ambayo mzee FAM alitukwaza? Yapo, lakini tuliamua kumuelewa kama kiongozi. Mfano, maridhiano tuliyapinga. Hata kumleta Mwenyekiti wa CCM katika mkutano wa BAWACHA siku ya wanawake Duniani, haikuwa sawa. Lakini tulimuelewa.
Kama ambavyo tulisimama kidete na kulinda jina la CHADEMA na viongozi wake wakati Mzee Freeman Mbowe, akiwa kiongozi wetu, ndivyo tutasimama, kutetea taswira ya CHADEMA na kuwalinda viongozi. CHADEMA ni UHURU na MABADILIKO ya KWELI
Mnamchoresha sana Mzee MBOWE, sana. #TunduLissuSioMhaini #JusticeForTAL ✊
IDF wamewatafuta mateka na maiti zote tangu HAMAS walipowateka eneo la kibbutz 07.10.23 na wamefanikiwa kupata mwili wa mwisho wa raia wao 26.01.25. IDF wametumia siku 843. Hii ni miaka 2 na siku 113. Wakati IDF wanatafuta maiti (mifupa in-such), wakabidhi kwa familia zao, wazike kwa heshima katika ardhi yao, kwetu hapa maiti zinapotezwa kuficha ushahidi. Kuna familia zinalia hadi sasa hazijawahi kuona maiti za ndugu zao tangu 29.10.25 hadi leo. Hii inasikitisha sana. Wamezika picha na nguo za marehemu. Wengine wanatekwa wanatupwa porini ili waliwe na wanyama wakali. Ni kitu hatari sana kama Serikali isipojali na kuthamini haki za watu wake kuishi.
Rais wa nchi akishapoteza uhalali, mpaka birthday yake itatumiwa kama sherehe ya kitaifa.
Hiyo ndio gharama ya ushenzi!!
Nizam al-Mulk na Machiavelli hawakukosea waliposema mtawala yeyote yule anayenyanyasa watu wake kamwe hawezi kuishi kwa amani.
Rais wa nchi akishapoteza uhalali, mpaka birthday yake itatumiwa kama sherehe ya kitaifa.
Hiyo ndio gharama ya ushenzi!!
Nizam al-Mulk na Machiavelli hawakukosea waliposema mtawala yeyote yule anayenyanyasa watu wake kamwe hawezi kuishi kwa amani.
Hiki ni kikao cha tawi la Ilundo Kiwira, Rungwe Mkoani Mbeya.
Kikao hiki kimefanyika January 25. 2026 baada ya kifungo cha Mahakama kumalizika sasa ni mwendo wa vikao vya ndani na mikutano ya hadhara mpaka kieleweke.
Tuna Mungu, Tuna watu, Tutashinda.
Ameandika Askofu Bagonza
MZEE MTEI AMEZIKWA MWILI; FIKRA ZAKE ZIMEBAKI
Jana 24/1/2026, taifa limeuzika mwili wa Mzee Edwin Mtei (94). Ana historia inayogusa sekta nyingi hapa nchini. Watu wa namna hiyo huwa ni kama moto ambao hufa/kuzimika na kuacha majivu badala ya kuacha moto. Yeye ameacha fikra. Ebu tudadavue umbeya kidogo:
1. Amewakusanya na kuwaunganisha watanzania. Hata waliohujumu fikra zake wakashika vipaza sauti kumsifia. Duh! Hata shetani anatamani kama wangekuwa wanamaanisha walichokuwa wanaongea bila kupepesa macho! Misiba ni darasa la uongozi.
2. Kanda zote za Chadema zikatoa salamu. Nikajifunza. Kama hatuko tayari kubadilika, basi tupanue mahabusu na magereza. Hakuna hela inayotosha kuwanunua wote, na hakuna risasi za kutosha kuwaua wote. Tunahitaji uongozi, siyo utawala.
3. Freeman Mbowe; Mkwe, mmoja wa waasisi, Mhanga wa maridhiano-hila, M/Kiti Mstaafu na mfungwa wa zamani, “akaiba show” kama alivyoiiba Monduli Februari 2024. Aliongea vizuri. Tunasubiri vitendo. Tomaso ni wengi sana. Ajue: Mkandamizaji wake wa jana hawezi kuwa mkombozi wake wa kweli leo. Awe moto siyo vuguvugu.
4. Madaraka makubwa hayaachani na upofu na ukiziwi. Mwenye madaraka akiona na kusikia, madaraka hupungua na usalama wake kuongezeka. Wananchi huchukua madaraka na kuyatumia kumlinda kiongozi wao. Bunduki haiongezi madaraka bali ni “Kausha madaraka”. Watawala wetu zindukeni, bunduki zinakausha madaraka yenu.
5. Upofu na ukiziwi ukimpata mtawala, mahabusu na magereza hugeuka vyuo vikuu vya mabadiliko katika nchi. Uhuru wa Afrika Kusini uliandaliwa Roben Island. Uhuru wa Kenya uliandaliwa Lokitang Prison na Lodwar Prison. Hapajawahi kutokea mfungwa wa kisiasa aliyerudi toka gerezani akamnyenyekea mtawala aliyemuweka. Hata Mandela alisamehe lakini hakuabudu aliyotendewa gerezani. Nipe ushahidi wa mfungwa wa kisiasa mnyenyekevu?
6. Katika nchi huru “zisizo huru”, mabadiliko huandaliwa katika vyuo vinavyoitwa House Arrests, mazuio ya maandamano, sheria za uchochezi, doria mitandaoni, na Safe Houses. Mahabusu maalum (solitary confinement) huwa ni madhabahu ya kuyeyusha dhahabu iwe bora zaidi. Hakuna barua nyepesi itokayo gerezani. Tunajikaanga.
7. Uhuru ni panga likatalo kuwili. Ukimweka huru mfungwa, mnufaika wa kwanza ni Askari Jela. Alipo mfungwa, yupo Askari. Wote wananyeshewa na wote wanakesha. Mkandamizaji na mkandamizwaji, wote hunufaika na uhuru. Kuwafungulia wafungwa wa kisiasa, ni kuwaweka huru watawala wetu. Mnataka nani aseme ndipo mjue hili ni kwa faida yenu?
8. Nimetoka ibadani. Leo tumehitimisha Ufunuo. Tumekumbushwa kubadilika kwa Bwana Yesu mbele ya wanafunzi wake kule mlimani. Wakatamani kubaki huko utukufuni. Yesu akasisitiza washuke ili kuhudumia wahitaji. Tunaalikwa kushuka ili kuwahudumia watu. Hitaji kuu la watu wetu ni UHURU na THAMANI YA UTU wao. Miradi bila uhuru ni sawa na chakula kizuri kwa mfungwa.
Ngoja niende kula. Kuna Mjaluo hapa kaazima suruali la kwenda kuposea mke wa pili, anasunbua sana hapa mtaani.😅😅