Kwa hiyo kwa akili za Magereza wanaamini kabisa kwamba Ujumbe wa TL unatakiwa kukanushwa?! Ili iweje.
Tatizo hamsomi alama za nyakati nisha wahi kuwaambia Tundu Lissu ni LAW MANIA ..
Pia akiwa ndani anaendelea kuwa Imara ,akiwa nje anaendelea kuwa Imara ,mumejaribu kumuua Mungu akakataa...anaendelea kuwa Imara wakati haiba yenu inaporomoka hovyo mbele ya jamii.
Kama ilivyokuwa kwa Babu yao Farao ndiyo roho ya vijukuu vyake imezidi kuwa ngumu na kaidi mbele za Mungu.
Eti tunazungumzia maridhiano katikati ya kudhuluma Haki za watu na propaganda zisizojali Uhai wa maelfu ya watanganyika wa hanga wa ukatili wa Oktoba 29.
Mtaendelea hata kukanusha kwamba leo hajaenda chooni kujisaidia na haitasaidia...
HAKI ,UKWELI NA UWAJIBIKAJI VITALIPONYA TAIFA.
@Baradhuli2 Sioni jinsi gani mlemavu mwenye kampuni au biashara yenye uwezo ya kugombea nafasi ya zabuni za serikali akatengwa kwa misingi ya ulemavu wake. Kama kweli 30% yote iko allocated kwa makundi maalumu kama walemavu, basi hii sera haiko sawa inapaswa kupitiwa upya.
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) @ChademaTZ2 Bara, John Heche, John Heche @HecheJohn , amebainisha kuwa urithi mkubwa ulioachwa na muasisi wa chama hicho, Mzee Edwin Mtei, si jina la chama pekee bali ni mfululizo wa mapinduzi ya kisera ambayo yamebadilisha maisha ya Watanzania, ikiwemo kufutwa kwa kodi ya kichwa.
Akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 33 ya CHADEMA, Heche amesema Mzee Mtei aliyefariki dunia Januari 19, 2026, nyumbani kwake Tengeru mkoani Arusha, alichagua jina la "Chama cha Demokrasia na Maendeleo" kwa makusudi ili kuakisi mrengo wa Kati-Kulia (Center-Right), unaoamini katika soko huru, haki za binadamu, na mamlaka ya wananchi.
“Kwa hiyo chama chetu ni chama cha mrengo wa kati kulia ambacho kinaamini katika demokrasia, kinaamini katika soko huru la watu kufanya biashara, unafanya bila bugha na serikali inatimiza wajibu wake unalipa kodi, tunaamini katika misingi ambayo rasilimali za nchi yetu zitumike kwa ajili ya kuendeleza watu wetu sio kuendeleza wageni. Hicho ndicho alichokipigania mzee Mtei”, ameeleza.
TUTASHINDA. MSIOGOPE.
Nelson Mandela alisimama mahakamani mara nne katika maisha yake ya mapambano. Siyo kwa sababu alikuwa mhalifu, bali kwa sababu alisimama imara kupinga mfumo dhalimu uliowanyima watu utu, haki, na sauti.
Kabla ya kesi maarufu ya Rivonia ya mwaka 1963/64, Mandela alikuwa amefungwa gerezani mara mbili. Kila kifungo kilikuwa ujumbe: dola ilitaka kumvunja moyo, kumchosha, kumkatisha tamaa. Lakini haikufanikiwa.
Hukumu ya miaka 27 gerezani haikuwa tu adhabu kwa mtu mmoja, Mandela; ilikuwa jaribio la kuzika ndoto ya ukombozi wa Waafrika Kusini. Mandela alitengwa, akanyimwa uhuru, familia, na maisha ya kawaida.
Miaka mimgi ilipita taratibu, siku zikafanana, mateso yakawa sehemu ya ratiba. Lakini hata ndani ya kuta za gereza, wazo la uhuru halikufungwa. Ndoto ya uhuru haikuzima. Mawazo hayawezi kufungwa kwa minyororo.
Mapambano hayakulipuka mara moja baada ya hukumu hiyo. Ilichukua takribani miaka kumi kabla ya wafuasi wa ANC na jamii ya kimataifa kuamka kwa nguvu mpya, kwa uelewa mpana zaidi, na kwa mshikamano wa kweli.
Mabadiliko ya kweli mara zote huchelewa, lakini hayapotei. Mbegu inapandwa leo, lakini huota kwa wakati wake. Ndiyo maana hatupaswi kukata tamaa. Ikiwa leo tunaona giza, haimaanishi alfajiri haitafika.
Ikiwa juhudi zetu zinaonekana kama hazina matokeo, haimaanishi kuwa ni bure. Historia inaonyesha kuwa wale wanaodumu, wanaostahimili, na wanaokataa kukata tamaa, hatimaye hubadilisha mkondo wa mambo.
Maumivu tunayopitishwa si laana; ni somo. Ndiyo yanayotujenga, yanayotufundisha uvumilivu, na yanayotupa mizizi ya uimara. Bila maumivu, dhamira hubaki dhaifu. Bila mateso, ushindi hukosa maana.
Kama Mandela alivyosimama tena, nasi pia tunapaswa kusimama—si mara moja, bali kila tunapoangushwa. Bado hatujachelewa. Wakati bado upo. Kile tunachopitia leo kinaweza kuwa msingi wa ushindi wa kesho.
Kinachotakiwa si kukimbia maumivu, bali kuyavumilia kwa hekima na kuyageuza kuwa nguvu. Historia inawaandika kwa heshima wale wanaodumu, si wanaokata tamaa njiani na kukimbia mapambano.
Tundu Antiphas Mughwai Lissu anatimiza siku 284 gerezani, amevunja rekodi ya kuwa kiongozi wa kwanza wa juu wa chama cha upinzani Tanzania kuwekwa kizuizini kwa muda mrefu zaidi tangu mwaka 1992
Dola katili la CCM haliwezi kuzuia na kuzima ndoto za kuitafuta Tanzania inayoheshimu haki za watu, misingi ya utu, usawa na uwajibikaji. Tundu A.M Lissu sio mhaini. Tundu Lissu arejeshewe uhuru wake. #FreeTunduLissu
@Roma_Mkatoliki Propaganda. Ukishakuwa mpinzani kwenye nchi ambayo haijawahi kuona upinzani, unaitwa kibaraka wa mabeberu. Ilhali, vibaraka wenyewe ndio walioko madarakani
@HildaNewton21 Kwahyo Heche anaizuia mahakama isimalize kesi🤣🤣🤣 huyu toka akiwa chadema alikuwa na mapepe sana akiwa jukwaani. Sio mwanasiasa ambaye atakuja kuwahi kuwa na mvuto, ni dalali anaetafuta kipato kupitia siasa. Ipo siku atakuwa exposed kiasi cha kuwa hatarini
Hebu cheki chuma hiki, Clemence Mwandambo ameshikiliwa na Polisi wiki 3 bila kuonana na ndugu zake, ametoa anafuraha kuliko Samia, mateso yanaimarisha watu.
Nitafurahi sana kusikia jibu la hili swali la #Mwandambo ⬇️
KWA NINI WATOTO KWENYE SHULE ZA MSINGI ZA SERIKALI WANASOMA KWA KISWAHILI HUKU WALE WA SHULE BINAFSI WAKISOMA KWA KIINGEREZA LAKINI WOTE WAKIKUTANA KIDATO CHA KWANZA WANALAZIMIKA KUSOMA KWA LUGHA MOJA YA KIINGEREZA?