"Vijana wa vyuo vikuu wanakimbia mijadala ya kisiasa. Mazingira sio rafiki. Wameshuhudia mhadhiri akipewa kesi ya ugaidi kisa tu mafunzo anayotoa darasani. Siasa imegeuzwa jinai. Hofu nyingi, kuliko matumaini."
Makamu Mwenyekiti wa @ACTwazalendo Bara
@MchinjitaIR#AmkaPodcast
"Mwaka 2025 mauaji makubwa yamefanywa nchini. Kuna watu ndugu zao waliko. Wengine wanasema kuna maiti zimepelekwa viwandani kuchomwa moto. Yote haya yanahitaji Tume Huru ya Uchunguzi."
Makamu Mwenyekiti Bara wa @ACTwazalendo@MchinjitaIR#AmkaPodcast
Katika kuwakabili wapigania haki, dola linaweza kuwatisha. Wapambanaji dhaifu hutishika ila wapambanaji imara, vitisho huwa ndio chachu ya mapambano. Hivi ndivyo anavyoeleza Ndg Anthony Severine wakati akichambua filamu ya Makala iitwayo Everything Must Fall.
#DarasaLaWiki
"Serikali imeshindwa kusimamia haki za wafanyakazi wa sekta binafsi."
Majula Kafumu
Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva wa Mabasi Tanzania
#AmkaPodcast Ep 12
"Dereva akipata ajali hapati msaada wa manufaa kutoka kwa tajiri wake. Madereva hatuna bima ya afya. Mshahara tunapewa mkononi au kwenye simu. Haupitii benki, kwa hivyo tunakosa sifa ya kukopesheka."
Majula Kafumu
Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva wa Mabasi Tanzania
#AmkaPodcast
"Serikali inasema kuwa inatoa mikopo ya asilimia kwa wanawake na vijana, lakini haiwafikii. Kuna mchakato mrefu unaohitaji gharama ya fedha, hata hivyo mwishowe vikundi vinavyopata vichache mno."
Katibu wa Ushirika Wanawake Wavuja Jasho
Faria Shomari
#AmkaPodcast| Episode 13
"Ni kumwangusha machinga endapo ukimwondoa maeneo ya katikati ya mji, hifadhi ya barabara na kwenye maeneo ya karibu na huduma za kijamii."
Katibu Mkuu Kiongozi wa @ACTBarazaKivuli@idrisa_kweweta
AMKA. HOJI. KOMBOA
#AMKAPodcast.
Kwenye darasa la wiki lilopita tulitazama na kujadili filamu ya makala ya "Decolonize Law! Part 3: Fighting for Transformation.
Tumeona jinsi unyonyaji wanyonge ulivyohalalishwa kisheria kipindi cha ukoloni na ukaendelea kubaki hata baada ya uhuru.
#DarasaLaWiki#AmkaPodcast
"Huduma ya maji inatakiwa Serikali itoe na si mtu binafsi. Kila raia ana haki ya kupata maji haijalishi ana kipato gani."
Waziri Kivuli wa Maji wa ACT Wazalendo
@CornelyYasinta#AmkaPodcast#Ep09
Leo Juni 19, 2026 Darasa la Wiki linaendelea katika Ukumbi wa Juma Duni Haji, Makao Makuu ya @ACTwazalendo (DSM.)
Darasa letu la leo linaangazia MTAJI kwa mtazamo wa Karl Marx katika Kitabu chake cha DAS KAPITAL
πβπ½
Hili darasa linafanyika kila Ijumaa.
β#DarasaLaWiki
"Mwaka 1992 Wanafunzi UDSM waliingia barabarani kupinga Serikali, iliposema kuwa haina rasilimali za kutosha kuendesha elimu bure."
Mwenyekiti wa Wanafunzi wanaosoma Sayansi ya siasa UDSM
Anthony Severine
Je! Wanafunzi wa sasa wanashiriki katika mapambano ya kudai haki?
"Badala ya miaka saba ya shule ya msingi, sasa wameweka miaka sita. Je! Kwa kuweka miaka sita walimu wameongozeka? Je! Miundombinu imeboreshwa? Wamejibu changamoto?"
Waziri Kivuli wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa @ACTwazalendo@rizikishahari@Amkapodcast Ep 07
#AmkaPodcast
"Serikali inajenga matabaka. Pale Shule ya Msingi Mzimuni, sasa pana kuna ya Kiingereza na Kiswahili. Wa Kiingereza mazingira yao bora na wanalipa laki 4 kwa mwaka."
Waziri Kivuli wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa @ACTwazalendo@rizikishahari
Amka Podcast Ep 07
#AmkaPodcast
"Mwalimu na mwanafunzi lazima watumie lugha wanayoifahamu. Kwa sababu unapofikiri, lazima ufikiri kwa lugha yako."
Waziri Kivuli wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa @ACTwazalendo@rizikishahari
Amka Podcast Ep 07
#AmkaPodcast
"Bunge dhaifu. Kama kungekuwa na bunge ambalo linajali maslahi ya Taifa, wangepitisha maadhimio ya kuwachukulia hatua wabadhirifu waliotajwa kwenye Ripoti ya CAG."
Mwanadarasa
@jksemkuya03#RipotiyaCAG#AmkaPodcast
Amka Podcast ep 06 inaangazia hali ya afya nchini Tanzania, gharama za matibabu, mfumo wa ugharamiaji na hatua za Serikali.
Kutazama zaidi, bofya link hiiππΏ
https://t.co/LhEhF2zDFM
Amka Podcast Episode 05
"Kila mwaka vijana wanaoingia katika soko la ajira ni zaidi ya milioni moja, lakini wanaoajiriwa huwa chini ya laki mbili. Kwa hivyo vijana wasiopungua laki nane wanakuwa wako mtaani tu. Matokeo yake ndio tunapata GZ wasiokuwa na mwelekeo."-Kassela Mdachi