Fainali ya Michuano ya kuwania taji la Cheraa Unity Cup kati ya Sibanga FC na Kapsara FC itachezwa Jumamosi hii ya Mei 16, 2026 kwenye Uwanja wa Zion Transend, ulioko Cherangany Kaunti ya Trans Nzoia, nchini Kenya. Bingwa atazawidiwa Ksh. 1,000,000. Mechi itaanza saa sita mchana.
John Kamaisi, wa Nakuru Golf Club, alituzwa Ksh. 92, 500 baada ya kushinda Ubingwa wa Mashindano ya NCBA Kiambu Open 2026 huku matokeo hayo, yakimfanya Kamaisi kupande hadi nafasi ya pili kwenye orodha ya Kenya Amateur Golf Circuit Order of Merit, akiwa na jumla ya alama 344.
Kocha Mkuu wa timu ya mpira wa magongo ya Kisumu Youngstars Hockey Club John Shivisi alishinda Tuzo ya Betika/SJAK ya Kocha Bora wa mwezi Februari 2026 nchini Kenya baada ya kuiongoza timu hiyo kupanda Daraja kucheza kwenye Ligi Kuu ya mpira wa magongo, msimu ujao 2026/27
Droo ya mechi za Robo Fainali kwa Mashindano yote mawili ya Shirikisho la Soka Afrika CAF, zitafanywa mchana wa Jumanne hii ya Februari 17, 2026 katika makao makuu ya chama cha Soka nchini Misri, yaliyoko Jijini Cairo.
Timu ya taifa ya Kenya, maarufu kama Jasiri, ilitwaa Ubingwa wa Mashindano ya Kimataifa ya Mchezo wa Tong IL-Moo-Do ya makala ya 12 ya Mombasa Open na kulihifadhi taji hilo kwa mara ya 12 mfululizo. Jasiri ilijishindia jumla ya medali 234 – dhahabu 67, fedha 67 na shaba 100.
Huu mpira unaitwa ITRI utakaotumika wakati wa AFCON 2025, nchini Morocco ambapo jina la mpira huo unatokana na jina la saa ya kale ya Morocco, zellij, na pia ITR inaelezea nyota iliyopo katika bendera ya taifa la Morocco. Mpira huo unauzwa kwa Sh.22,360 kwa fedha za Kenya.
Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya soka ya Kenya ya wanawake ya Harambee Starlets Beldine Odemba, mwenye umri wa miaka 41, ameshinda Tuzo ya Betika/SJAK ya Kocha Bora wa mwezi Oktoba mwaka 2025 nchini Kenya na kuzawidiwa kitita cha Ksh.100,000 pamoja na kikombe.
Rais wa Madagascar Andry Rajoelina leo Jumatatu ya Oktoba 13, 2025 ameitoroka nchi hiyo kukimbilia Ufaransa kufuatia mfululizo wa maandamano ya wananchi wake yaliyongozwa na vijana wa kizazi cha Gen Z wakilalamikia ufisadi, umasikini na huduma duni za kijamii.
Kampuni ya Dola Group ya Mombasa kudhamini Michuano ya Sisi Ni Dola Cup 2025 kwa muda wa mwezi mmoja ikishirikisha timu 20 baadhi ya timu hizo zikitoka Kaunti ya Kilifi, Kwale na Mombasa huku bingwa wa makala hayo ya kwanzakabisa, akituzwa kitita cha Ksh.500,000.
Shirikisho la Mchezo wa Tong Il-Moo-Do nchini Kenya(KTMF) likishirikiana na Shirika la Kijamii la Brilliant Feminine wameungana kupiga vita dhidi ya Unyanyasaji wa Kijinsia(GBV) na kuendeleza kampeni za wanawake kuwezeshwa ili kujinasua kiuchumi.
Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain PSG Ousmane Dembélé ameshinda Tuzo ya Mwanasoka Bora barani Ulaya ya Ballon D’Or ya mwaka huu 2025 akiwashinda Lamine Yamal wa Barcelona na Vitinha wa PSG. Kocha wa PSG Luis Enrique alishinda Tuzo ya Kocha Bora wa mwaka.
Wanariadha Peter Mwangi na Fridah Ndida walishinda mbio za maandalizi za Kilomita 21 za Standard Chartered Nairobi Marathon zilizofanyika, Jijini Nairobi, nchini Kenya. Fridah alitumia dakika 77 kushinda kitengo cha wanawake naye Mwangi alitumia dakika 65 kushinda mbio za wanaume
Kocha Mkuu wa Harambee Stars Benni McCarthy, raia wa Afrika Kusini, ndiye mshindi wa Tuzo ya Betika/SJAK ya Kocha Bora wa mwezi Agosti mwaka 2025 nchini Kenya na kuzawidiwa kitita cha Ksh.100,000 pamoja na kikombe. Sikiliza Radio Mabingwa Link: https:https://t.co/mej6yUw3XX
Michuano ya makala ya nane ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ligi za Nyumbani, yaani Kombe la CHAN 2024 inakamilika rasmi Jumamosi hii ya Agosti 30, 2025. Madagascar na Morocco zinacheza fainali kuanzia saa kumi na mbili jioni Uwanjani Kasarani Jijini Naironi.
Jumla ya mechi 12 za Ligi ya Taifa Daraja la Pili Kanda ya Kaskazini ya Kundi A ya Shirikisho la soka nchini Kenya (FKF) zitachezwa wikendi hii kwenye viwanja tofauti. Mechi nne zinapigwa Jumamosi hii ya Julai 26 na mechi nyingine nane zinasakatwa Jumapili ya Julai 27, 2025.
Timu itakayoshinda Ubingwa wa Michuano ya Kombe la Dunia la Klabu la FIFA 2025 kati ya The Blues Chelsea ya England na Mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ‘Les Parisiens’ (yaani Wana Paris) Paris Saint-Germain PSG ya Ufaransa atapata kitita cha Doła za Kimarekani 40 milioni.
Rais wa Kenya Dkt. William Ruto akizungumzia ‘umuhimu wa umoja’ katika timu wakati alipotembelewa na mabingwa wa Mozzart Cup timu ya Nairobi United FC katika Ikulu ya Nairobi siku ya Alhamisi ya Julai 10, 2025.