#ServantLeader
👉Consultant & Manager - Hotels and Tourism,
👉D/Shadow Minister for Natural Resources and Tourism @ACTBarazakivuli,
👉World Peace Ambassador.
Hii ni kwasababu Wasanii mnakubali kutumiwa.
Uzalendo kwa Wanamuziki wengi haupo.
Bado mna nafasi ya kutumia sanaa kurejesha Taifa katika bomba la haki na uwajibikaji.
VIDEO:
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Adbul (Diamond Platnumz) ameilalamikia Serikali ya Tanzania kuwa imewekeza nguvu kubwa kwenye mchezo wa mpira wa miguu huku ikiudharau muziki na kuukumbuka kwenye kampeni pekee.
Ameeleza hayo leo Machi 31, 2026 kwenye mahojiano maalum na kituo cha Wasafi FM akieleza kuwa muziki unapuuzwa sana na hata ushauri wa ujenzi wa Arena kaa ajili ya matukio makubwa ya kimziki haufanyiwi kazi pamoja na kwamba ni muhimu sana.
"Wanaweka nguvu sana kwenye mpira ila kwenye mziki wana dharau sana mshikaji wangu sisi tunaonekana tu kwenye kampeni yani hapo tupo 'serious' ila baada ya hapo ila baada ya hapo miundombinu aaah" amesema Diamond Platnumz
Mwezi Mmoja nyuma Dudu Baya alisema kuwa kifaa Cha MRI tulicho nacho Tanzania ni kifaa ambacho huenda kilinunuliwa ambacho kimetumika (used).
Baada ya siku kadhaa wizara ya Afya walikuja kukanusha hicho kitu.
Lakini leo Mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali (CAG) katika ripoti yake amesema MSD waliagiza dawa na vifaa tiba ambavyo vina karibia kuisha muda wake (expire) na hivyo kugharimu serikali hasara ya Bilioni 20.
Kwa alicho kisema CAG hayuko mbali na alicho kisema Dudu Baya.
Kikao cha kwanza cha mkutano wa tatu wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kimeanza leo, Machi 31, 2026, jijini Dodoma, lakini kimechukua muda mfupi wa dakika 15 pekee kabla ya kuahirishwa hadi kesho, Aprili 1, 2026 saa 3:00 asubuhi.
Kuahirishwa kwa kikao hicho kumetokana na kutokuwepo kwa Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, ambaye alitarajiwa kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Badala yake, Waziri Mkuu yuko katika shughuli za maziko ya aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) pamoja na Mbunge wa Jimbo la Isimani, Marehemu William Lukuvi.
Bunge hilo linaendelea na majukumu muhimu ya kujadili na hatimaye kupitisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2026/2027, zoezi ambalo ni msingi wa kupanga matumizi na vipaumbele vya maendeleo ya taifa kwa mwaka ujao.
Kikao kinatarajiwa kuendelea kesho ambapo Waziri Mkuu atawasilisha rasmi bajeti hiyo muhimu mbele ya wabunge.
Umeshauri lililojema ila serikali yetu hii ya mbumbu leading itajifanya haioni.
Yenyewe inawaza kuwanyonya wananchi mpaka tone la mwisho.
Solution ni Moja tu @ccm_tanzania watoke kwenye hatamu.
Leo tumeamka na bei mpya ya mafuta. Bei tuliyoitegemea kufuatia mashambulizi yanayoendelea ya Marekani na Israel dhidi ya Iran. Kama ilivyo sehemu zote duniani bei imepanda sana na gharama za maisha zitakuwa kubwa sana. Serikali isaidiane na wananchi kubeba gharama hizi.
Serikali iondoe tozo, kodi na ushuru katika mjengeo wa bei ya mafuta ili kumwezesha mwananchi kupata nafuu.
Pope Leo XIV has released his prayer intention for April, inviting Catholics around the world to pray for priests facing moments of crisis in their vocation:
In the name of the Father, and of the Son, and of the Holy Spirit. Amén.
Lord Jesus,
Good Shepherd and companion on the journey,
today we place in your hands all priests,
especially those going through moments of crisis,
when loneliness weighs heavily,
when doubt clouds their hearts,
and when exhaustion seems stronger than hope.
You who know their struggles and wounds,
renew in them the certainty of your unconditional love.
Let them feel they are not mere functionaries or lonely heroes,
but beloved sons, humble and cherished disciples,
and pastors sustained by the prayer of their people.
Good Father,
teach us as a community to care for our priests:
to listen without judging,
to give thanks without demanding perfection,
to share with them the baptismal mission
of proclaiming the Kingdom in word and deed,
and to accompany them with closeness and sincere prayer.
May we support those who so often support us.
Holy Spirit,
rekindle in our priests the joy of the Gospel.
Grant them healthy friendships, networks of fraternal support,
a sense of humor when things don’t go as expected,
and the grace to always rediscover the beauty of their vocation.
May they never lose trust in You,
nor the joy of serving your Church with a humble and generous heart.
Amen.
Pope Leo released his prayer intention for the month of April, inviting Catholics to pray for priests who are facing a personal crisis in their vocation.
#TANZANIA: BWEGE AZIKWA NA MAELFU YA WANANCHI WA KILWA MKOANI LINDI
Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Kilwa Kusini, Selemeni Bungara maarufu Bwege leo Machi 31, 2026 unazikwa jioni hii huku ukisindikizwa na maelfu wa Wananchi wa Kilwa mkoani Lindi katika nyumba yake ya milele.
Itakumbukwa hadi umauti wake unamfika alikuwa Mwanachama wa CHADEMA na mara ya mwisho alionekana katika viunga vya Mahakama Kuu kwenye kesi ya Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu katika kesi inayomkabili ya uhaini.
Zaidi: https://t.co/vs6m7UugQP
"Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha ndugu Seleman Bungara (maarufu kwa jina la Bwege) aliyekuwa mwanachama wetu wa ACT Wazalendo kabla ya hivi karibuni kutangaza kuhama chama, taarifa zinasema ndugu Bungara amefariki ghafla mapema leo wakati akiwa Hospitali alipokwenda kwa ajili ya kupata huduma yake ya kawaida ya kusafisha figo (dialysis), kwa niaba ya Chama, natoa pole za dhati kwa mke wa marehemu Bi. Mwanawetu Said Zarafi ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Chama chetu, kwa msiba huu mzito wa kuondokewa na mmewe" -Semu
"Aidha, Chama kinatoa pole kwa familia, wanachama wa ACT Wazalendo, ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine, ndugu Bungara atakumbukwa kama mmoja wa wanasiasa wa upinzani waliojitolea na kusimama imara katika kupigania na kutetea haki na mfumo wa demokrasia ya vyama vingi katika nchi yetu wakati wote wa uhai wake, ACT Wazalendo itashiriki kwa hali na mali katika msiba huu ikiwemo kubeba gharama za mazishi ya ndugu Bungara, vilevile tunatoa wito kwa wanachama wote wa ACT Wazalendo jimbo la Kilwa Kusini na popote nchini kuungana na familia ya marehemu kuwafariji katika kipindi hiki kigumu, msiba wa ndugu Bungara ni msiba wa ACT Wazalendo, Mungu aipokee roho ya marehemu na kuilaza mahali pema peponi, Amina" -Semu
Ni sehemu ya kile kilichoelezwa kwenye taarifa ya Chama cha ACT Wazalendo iliyotolewa kwa umma kupitia Kiongozi wa Chama hicho Dorothy Semu kufuatia kifo cha Mbunge wa zamani wa Kilwa Kusini Seleman Bungara (Bwege) kilichotokea mchana wa leo, Jumatatu Machi 30.2026.
Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), Charles Kichere imebaini makadirio yasiyo sahihi ya gharama ya ujenzi wa Uwanja wa AFCON Arusha pamoja na pia udhaifu katika majadiliano ya zabuni ya ujenzi wa Uwanja huo.
“Mradi ulikadiriwa kugharimu Sh187 bilioni lakini ulisainiwa kwa Sh338.54 bilioni sawa na ongezeko la asilimia 81. Hali hii inaonyesha kuwa makadirio hayakuwa sahihi na yaliathiri maamuzi ya kibajeti pamoja na utekelezaji wa mradi,” amesema.
VIDEO:
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo @ACTwazalendo , Dorothy Semu amesema chama hicho kimesikitishwa na msiba wa bwege kwani ameondoka mtu hodari wa siasa ambaye alikuwa na mchango mkubwa kwao na kwa watu wa Kusini.
Semu ameeleza hayo akizungumza na Jambo TV leo Machi 31, baada ya kushiriki mazishi ya Bwege yaliyofanyika Kilwa Kivinje mkoani Lindi na kufafanua kuwa hata Bwege alipobadili msimamo kuachana na wa ACT Wazalendo na kuiunga mkono CHADEMA bado waliendelea kuwasiliana na kuwa karibu.
"Pamoja na baadae kuwa na msimamo tofauti hatukuchukizwa naye...tuliendelea kuwa na Bwege kama mwenzetu hatukuona alipopungua" amesema Semu
VIDEO:
Kiongozi Mstaafu wa chama cha @ACTwazalendo , Zitto Kabwe amemtaja Marehemu Selemani Bungara(Bwege) kama kiongozi ambaye alikuwa na uwezo mkubwa licha ya kutofanikiwa kuwa na elimu kubwa na aliweza kutetea watu wake.
"Bwege hakuwa mbunge wa kwanza wa Kilwa, wala hakuwa ndio msomi sana wa Kilwa pamoja na darasa la saba lake, alijua kuwatetea na aliwatetea na mna haki ya kumsindikiza namna mnavyomsindikiza leo" amesema Zitto
Zitto ameungana na mamia kwa mamia ya wananchi waliojitokeza leo Machi 31, Kilwa Kivinje mkoani Lindi kwa ajili ya kushiriki mazishi ya Bwege huku maneno 'msimamo' na 'haki' yakitawala vinywani mwa waliomfahamu Bwege.
Hali ya Maisha inakua ya Maumivu.
Mifumo ya wizi serikalini inaongezeka.
Hakuna ashirio la Mamlaka kuwajibisha na kurejesha pesa ziloibwa.
Tanzania Hatuna responsible Economic visionary leading leader.
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta zitakazoanza kutumika kuanzia leo Jumatano, Aprili 1, 2026 ambapo kumekuwa na ongezeko kubwa la bei ikibainishwa kuwa ni kutokana na athari za mzozo wa kivita kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran ulioibuka Februari 28, 2026.
Katika taarifa yake, EWURA imeeleza kuwa mashambulizi katika visima vya mafuta, maghala na viwanda vya kusafisha mafuta Mashariki ya Kati pamoja na kufungwa kwa Lango la Hormuz—linalopitisha takribani asilimia 20 ya mafuta duniani, vimesababisha kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia, hivyo kuathiri pia gharama za uagizaji nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa bei mpya:
Dar es Salaam: Petroli Sh 3,820, Dizeli Sh 3,806, Mafuta ya Taa Sh 3,684
Tanga: Petroli Sh 3,881, Dizeli Sh 3,867, Mafuta ya Taa Sh 3,745
Mtwara: Petroli Sh 3,912, Dizeli Sh 3,898, Mafuta ya Taa Sh 3,777 huku maeneo mengine Petroli ikiwa ni zaidi ya Sh. 4000
EWURA imesisitiza kuwa wafanyabiashara wote wa mafuta nchini wanapaswa kuuza kwa bei zinazoonyeshwa kwenye mabango ya vituo vya mafuta, na hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka.
Aidha, mamlaka hiyo imewataka wananchi kutumia mafuta kwa uangalifu na ufanisi kutokana na athari za kimataifa zinazoendelea, huku ikiendelea kuchukua hatua za kuhakikisha upatikanaji wa mafuta nchini hauathiriki.
Bei hizo zimepanda ikiwa ni tofauti na Bei zilizotangazwa tarehe 4 Machi 2026 ambayo maeneo mengi ilikuwa ni Sh 2864 hadi 2959.
Inna lillah waina ilaih waina ilaih raajiun.
Pole sana familia ya Mzee Suleiman Bungara Bwege kwa msiba huu mzito. Pole sana Mama Mwanawetu Zarafi, mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha ACT Wazalendo kwa kufiwa na mumeo.
Pole zangu kwa wana Kilwa na Lindi kwa mtihani huu. Mola ampumzishe Mzee wetu na tuendelee kumwombea dua.
Nawapongeza sana DRC kwa kufuzu kwenda Fainali ya Kombe la Dunia 2026. Nchi ya Kongo imekuwa Mwakilishi pekee kutoka EAC @jumuiya na mmoja wa wawakilishi 2 tu kutoka SADC @SADC_News katika @FIFAWorldCup 2026. Hongereni sana banaKongo! @SORAZIZ