Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Suleiman Jafo ametangaza kuongeza SIKU 3 za kujiandikisha kwenye Orodha ya Mpiga Kura, hivyo zoezi la kujiandikisha litaisha tarehe 17/10/2019.. Mimi Nimejiandikisha, wewe Je!!!???*NENDA UKAJIANDIKISHE*
Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Arusha, anawakumbusha wananchi wote wenye umri wa kuanzia umri wa miaka 18 na kuendelea, kujiandikisha kwenye Orodha ya Wapiga Kura, Zoezi linaendekea mpaka tarehe 14/10/2019.
Tumia vizuri muda uliopangwa, haakikisha unajiandikisha!!!
"Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, imetumia kiasi cha shilingi milioni 150 kujenga Ofisi ya Uthibiti Ubora Shuleni, halmashauri ya Arusha, kwa lengo la kuendelea kuboresha miundombinu ya elimu, kuimarisha kiwango cha taaluma kwa wanafunzi".#TUNATEKELEZA
"Serikali imeamua kuboresha huduma za afya nchini, kwa kutumia kiasi cha Tsh. milioni 400 kujenga Kituo cha Afya Mbuyuni kata ya Oljoro ikiwa ni Jengo la Mama na Mtoto, Maabara, Jengo la Upasuaji na Nyumba ya Mganga". Dkt. Wilson Mahera Charles - Mkurugenzi Mtendaji Arusha DC.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Halmashauri ya Arusha, mwl Hosein Mghewa, ametangaza rasmi, majina ya Mipaka ya vijiji iliyoko katika eneo la halmashauri ya Arusha, kwenye mkutano wa hadhara wa wananchi wa Kijiji cha Marurani, kata ya Nduruma, Halmashauri ya Arusha.
DED Arusha DC, Dkt. Wilson Mahera, amewataka watumishi wa halmashauri hiyo, kufanya kazi kwa bidii na kwa kushirikiana kama timu, bila kujali nafasi walizonazo, ili kufikia malengo yaliyoaanishwa kwenye mpango mkakati wa halmashauri hiyo kufikia mwaka 2025.
Idara ya Maendeleo ya Jamii Arusha DC, imejipanga kutekeleza mradi wa 'TCI - Tupange Pamoja, kwa kutumia majukwaa ya vijana, wanawake na walemavu kuwapa elimu ya Afya ya Uzazi kwa Vijana, kupitia mpango wa 'Huduma Rafiki kwa Vijana', Mradi unaofadhiliwa na shirika la JPEIGHO.
Dr. Shevaline Minja, mmoja wa timu ya Uendeshaji Mradi wa TCI- TUPANGE PAMOJA, ARUSHA DC, akitoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana wa shule ya sekondari Mlangarini, baada ya kuwakuta Zahanati ya Mlangarini wakisubiri kutibiwa, hakika vijana wanahitaji elimu zaidi ya afya ya uzazi
Ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto (maternity ward), hospitali ya wilaya Olturumet, halmashauri ya Arusha umefikia asilimia 95, mpaka kukamilika utagharimu kiasi cha shilingi milioni 147, fedha zinazotokana na mapato ya ndani ya halmashauri.
Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Arusha, Dkt. Wilson Mahera, anawatangazia wananchi wote kuwa kesho 22.08.2019 kutafanyika MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI, kwenye Ukumbi wa Mikutano halmashauri ya Arusha kuanzia saa 03:00 asubuhi.
Wananchi wote mnakumbushwa kuhudhuria mkutano huo
Watalamu wa Kilimo na Mifugo, halmashauri ya Arusha, wamejipanga kutoa Elimu ya Kilimo na Mifugo kwa vitendo kupitia mashamba darasa kwenye Mabanda ya Halmashauri hiyo, wakati wote wa maonesho ya NANENANE yanayoendelea kwenye Viwanja vya Themi eneo la Njiro jijini Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Dkt. Wilson Mahera, anawatangazia wananchi wote, kutembelea Banda la Halmashauri yake katika viwanja vya maonesho Nanenane -Themi Jijini Arusha na kujionea shughuli za Kilimo na Ufugaji kwa vitendo. "Karibuni nyote"
KONGAMANO LA WAZEE WILAYA YA ARUMERU
Viongozi na Wazee Mashuhuri wa Wilaya ya Arumeru, watazungumza na Waandishi wa Habari leo Alhamisi tarehe 25.07.2019 kuanzia saa 04:00 asubuhi, kwenye Ukumbi wa Mikutano Halmashauri ya Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro amezindua rasmi kampeni ya Kitaifa ya 'JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA' yenye lengo la kutokomeza vifo vya mama na mtoto, vinavyotokana na Uzazi, katika halmashauri ya Arusha.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro amezindua amezindua rasmi Kampeni ya Kitaifa ya 'JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA' halmashauri ya Arusha yenye lengo la kutokomeza vifo vya mama na mtoto vinavyotokana na uzazi.
Uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, Jimbo la Arumeru Magharibi unaendelea vema kwenye vituo 238 vilivyopangwa huku vijana wakijitokeza kwa wingi.
Wananchi wote wenye sifa, wanahimizwa kwenda kujiandikisha ili kupata Kadi, za kupigia kura kwenye uchaguzi Mkuu 2020
Afisa Muandikashaji Jimbo la Arumeru Magharibi anawakumbusha wananchi wote kuwa Zoezi la Uandikishaji na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga Kura Jimbo la Arumeru Magharibi limeanza leo tarehe 18.07 na kumalizika tarehe 24.07.2019.