Wakajawa na uchungu, wakashauriana wao kwa wao wamtendeje Yesu.
Luka 6:11
Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu.
Luka 6:12
Viwango vya maombi🔥💪🏿
YESU AKAOMBA USIKU KUCHA MASAA 12 ILI ACHAGUE MITUME😅
NUKUU YA LEO: “Kwanza tafuta nafasi, ukipata nafasi onesha uwezo, ukionesha uwezo utajenga jina na kuaminika, ukiaminika utaanza kupata hela. Katika kupitia hatua hizi ni lazima ukubali maumivu ya mchakato wa lazima.” - Ruge Mutahaba
Kuna watu kwenye maisha hupaswi kuwabakiza kwenye maisha yako yani wasamehe halafu waweke mbali na wewe sio kwa ubaya bali kukuepushia matatizo yasio ya lazima✍️
Mnatuita mabahili sababu mnatufahamu kwa majina tu, Ila hamfahamu tulipotokea, Mungu endelea kuwalinda wote wanaopambana kubadilisha Historia ya walipotokea.
Nipo sehemu mbaya utanisamehe kwa uandishi. Lugha ya malaika zipo chache kwenye Biblia, kitabu cha Daniel, MENE MENE TEKEL na PERESI. Mfano mwingine upo kwenye kitabu cha ufunuo, inaitwa sign languages. Mungu pia ana lugha anaweza kuongea kwa Light, or water, I heard voice
Ambapo sehemu kubwa ya makala hiyo ilielezea maajabu ya ujenzi wa ukuta wa Benin, na kwamba ukuta wa Benin ni miongoni mwa ukuta mkubwa kuwahi kujengwa hapa ulimwenguni.
.
.
🙌🏾👊🏾✌🏾
.
.
Asili ya lugha ni nini?
Katika unabii wa Isaya, kauli za Yesu na mafundisho ya Paulo kulikuwa na vivumishi vilivyotumika kwa lugha. Hebu tuzichunguze.
Isaya 28:11 Maana kwa midomo ya kigugumizi na kwa lugha nyingine atasema na watu hawa.
👇👇
Maswali & Majibu (MM)
Majibu kutoka kwenye somo: Maombi ya kunena Kwa lugha
Niona nije na Majibu Kwa mfumo wa somo kbs ili yaweze kuwajenga na wale wasio fahamu pia kuondoa ubishi usio Jenga!
Hili ni moja ya swali nililolipokea!👇
“Tumeizunguka Gaza na hatutaruhusu Chakula, Maji, Mafuta wala Umeme uingie Gaza. Tunapigana na binadamu Wanyama sana na sisi lazima tuwatendee hivyo hivyo” Yoav Gallant, Waziri wa Ulinzi wa Israel
Meli ya kubeba ndege za Kivita ya Marekani inayoitwa “The USS Gerald R. Ford” ikiambata na meli nyingine za kivita zimefika kwenye bahari ya Israel, zikiwa tayari kutoa Msaada kwa Israel Muda wowote ule zitakapo hitajika.
Kundi la wadukuzi la Urusi la Killnet laonyesha kuunga mkono Hamas na kusema kuhusu Israel:
"Serikali ya Israel, unahusika na umwagaji damu huu. Huko nyuma mwaka wa 2022, uliunga mkono utawala wa kigaidi nchini Ukraine. Ulisaliti Urusi. Leo, Killnet inakujulisha hili rasmi! Mifumo yote ya serikali ya Israeli itakabiliwa na mashambulizi yetu!"
MGOGORO WA ISRAEL NA PALESTINA.
NINI CHANZO CHAKE, NINI KINAENDELEA NA NI IPI SULUHU YA KUDUMU?
#UZI 🧵
Uzi huu utaangazia uhalisia wa mgogoro kwa uwazi bila upendeleo. Hivyo kama una mihemko ya itikadi za kidini na kiushabiki nakushauri USISOME.
Like, Repost kisha tuendelee.
Hakikisha una chuja Taarifa na Habari Unazozipata Kutoka Katika Vyanzo Mbali mbali hasa zinazokuhusu wewe na maisha yako watu wengi wanapenda kugombanisha ili kuvunja uhusiano wenu na ndoto zenu zisitimie✍️
1.MABIBO
Ukiwa Dar es Salaam itakuwa si neno geni kwako kulisikia "MABIBO" inatamkwa hivyo hivyo kwa lugha ya Kiswahili.
Ukiwa barabarani ni kawaida Kukutana na magari (Daladala) za Mabibo kwenda Makumbusho,Mabibo Mwananyamala,Mabibo Kariakoo,Mabibo kwenda Mnazi mmoja,Mabibo kwenda Temeke,Mabibo kwenda Mbagala na sehemu nyingine lukuki.
Mabibo ipo Wilaya ya Ubungo,Jimbo la Ubungo, ni kata ndiyo inaitwa Mabibo yenye mitaa Sita
1.Matokeo 2.Mabibo farasi 3.Mabibo 5.Azimio 6.Kanuni
Umashuhuri wa Mabibo ulizagaa kwa kuwepo na Bar na Kumbi ya Starehe ya MULEBA BAR,Uwepo wa Shule ya Sekondari ya ROYOLA ,Mabwawa ya majitaka (maarufu kama Mabwawa Saba).
Kama Jina linavyosadifu MABIBO imetokana na Miaka ile ya 1960 hadi 85 kuwepo kwa shamba kubwa la Mikorosho
Shamba lilikuwa la Wanakijiji mbalimbali ambao walikuwa wenyeji wanao miliki mashamba hayo ya mikorosho,katika eneo la MABIBO.
Wenyeji wengi wa Mabibo wakati ule walikuwa ni wayao,Wangindo,wamakonde na Wamakua.
Watoto wengi tulikuwa tunaenda kufuata Korosho miaka ya mwanzoni lakini Wenyeji walikuwa wakali sana ukigusa korosho zao.
Walikuwa wanaruhusu watoto wale MABIBo Ila korosho unaacha hapo hapo ulipo tungua BIBO
Ikawa siyo Jambo baya bado makundi ya watoto kutoka sehemu mbalimbali tulikuwa tunaenda kusaka Sungura na kanga kwa kutumia Mbwa.
Mkikutwa na maroba na mifuko mmebena mikononi lazima mtaulizwa mmebeba nini..?
Sasa Kama ulibeba Korosho ni bakora tuh zinakuhusu,Salama yako useme umebeba "MABIBO" na ukisachiwa usikutwe na "KOROSHO" Utakula Viboko mpaka uone cha mtema kuni.
Mle mashambani neno MABIBO ni "FORMULAR", Neno MABIBO ni "PASS WORD" ya wewe kuingia na kutoka Salama
Hawakuwa na Uchoyo wa Kuzuia Mtu asile Mabibo kwa sababu yakioza watakula Popo tuh,Ila usiguse korosho zao.
Taratibu umaarufu wa tunda la BIBO ambapo wingi wake ni MABIBO ukawa mkubwa kwa simulizi la Watoto tunaotoka mbali kwenda kwenye Mikoroshi ya watu
MABIBO likashika kwa kasi sana.
NINI CHANZO CHA MGOGORO WA ISRAEL NA PALESTINA???
Historia ya mzozo kati ya Israel na Palestina ni ndefu na yenye migogoro mingi. Inaanzia enzi za zamani, na inahusisha masuala ya ardhi, dini, utaifa, na siasa. Hapa kuna muhutasari wa historia hiyo:
ZAMA ZA BIBLIA:
Historia ya Ibrahim ni muhimu katika maandiko matakatifu ya dini ya Kiyahudi, Ukristo, na Uislamu. Ili kuelewa uhusiano wake na mgogoro wa Israel na Palestina, ni muhimu kuanza na maisha yake na jinsi alivyoleta athari kubwa katika historia ya imani hizi tatu.
👉Ibrahim (Abraham) na Sara:
Ibrahim, aliyeitwa pia Abraham, alikuwa mwanzilishi wa imani ya Kiyahudi. Katika Biblia, anaelezewa kama mtu aliyeteuliwa na Mungu kuwa baba wa taifa lake. Mungu alimwita aondoke kutoka mji wa Uru wa Wakaldayo (katika eneo la Mesopotamia) na kuelekea Kanaani. Pamoja na mkewe Sara, Ibrahim alihamia Kanaani na baadaye, wakati walipokuwa wazee sana, Mungu aliwapa mwana wao wa pekee, Isaka. Lakini Ibrahim alikuwa tyari na mtoto na kijakazi wake Hagar.
👉Ismaeli na Waarabu:
Ibrahim pia alikuwa na mwana wa kwanza, Ismaeli, kupitia surrogacy na mjakazi wake Hagar. Ambaye walifukuzwa baada ya Sara kujifungua mtoto wa kwanza. Waarabu wanajiona kama wana wa Ismaeli na wanamheshimu kama mwanzilishi wa taifa lao. Hii inaunganisha Ibrahim na Waarabu na ina athari kubwa katika mgogoro wa Israel na Palestina, kwani Wayahudi na Wapalestina wanapigania ardhi ya baba yao, na historia ya Ibrahim inaunganisha pande zote mbili.
👉Yakobo na Wana wa Kumi na Mbili:
Mwana wa Isaka na mjukuu wa Ibrahim, Yakobo (Israel), alipewa jina la Israeli na Mungu. Yakobo alikuwa na wana kumi na wawili, ambao walikuwa waanzilishi wa makabila kumi na mawili ya Kiyahudi. Hii ndyo ilianzisha msingi wa taifa la Israeli.
👉Mgogoro wa Israel na Palestina:
Mgogoro wa Israel na Palestina unahusisha madai ya ardhi yanayotokana na historia ya eneo hilo. Waisraeli wanadai haki ya kuishi katika ardhi ya Kanaani ya baba yao Ibrahim (Palestina ya leo) kulingana na ahadi ya Mungu kwa Ibrahim. Wapalestina, kwa upande mwingine, wanadai haki ya kuwa na nchi yao katika ardhi hiyo hiyo ambayo ni ya babu yao Ibrahim.
Kwa hiyo, uhusiano wa Ibrahim na wana wake (Ismaeli na Isaka) na historia ya uhamiaji wao katika ardhi ya Kanaani inachangia kwa kiasi kikubwa mgogoro wa Israel na Palestina.
Mimi naweza sema Ibrahim asingechepuka basi haya yasingetokea leo hii. Hawa ni ndugu wa baba mmoja wanagombania mirathi.
ENEO KUKALIWA NA MAKABILA MENGI
Kupitia historia, eneo hili lilikaliwa na makabila ya Kiarabu na Wayahudi kwa nyakati tofauti. Lakini utawala wa kigeni, kama wa Waarabu, Warumi, Waturuki, na Waingereza ulibadilisha umiliki wa ardhi hiyo.
UKOLONI WA WAINGEREZA
Baada ya Vita Vikuu vya Kwanza na vya Pili vya Dunia, utawala wa Kiingereza uliendelea huko Palestina, na ndio waliendeleza mgawanyo wa ardhi kati ya Wayahudi na Waarabu huku waki chochea mgogoro wa Wayahudi na waarabu. Hii ilisababisha ongezeko la makazi ya Wayahudi katika eneo hilo.
AZIMIO LA UMOJA WA MATAIFA
Umoja wa Mataifa ulipitisha Azimio la Umoja wa Mataifa namba 181 mwaka 1947, lililopendekeza ugawaji wa Palestina kuwa mataifa mawili: moja kwa Wayahudi na nyingine kwa Waarabu. Hata hivyo, mgogoro uliibuka kati ya makundi haya na kusababisha vita na kuanzishwa kwa nchi ya Israel mwaka 1948.
Tangu wakati huo, kumekuwa na migogoro mingi, ikiwa ni pamoja na Vita vya Arab-Israeli (1948, 1956, 1967, 1973) na migogoro ya ardhi. Matokeo ya vita hivyo yalisababisha Israel kupanua eneo lake na kuongeza makazi ya Wayahudi katika Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza.
MICHAKATO YA AMANI
Kupitia miongo kadhaa, kumekuwa na jitihada za kuleta amani kati ya Israel na Palestina, ikiwa ni pamoja na Mkataba wa Oslo wa mwaka 1993 na mikataba mingine. Hata hivyo, mpaka sasa, suluhisho la kudumu halijapatikana, na mzozo unaendelea kuathiri eneo hilo.
ITAENDELEA 👇
#UPDATES Jumla ya Wapalestina 256 wakiwemo watoto 20 wameuawa na watu wengine 1,864 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Israel katika muda wa saa 24 zilizopita hii ni kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina huko Gaza.
Jeshi la anga la Israel lilitoa picha za mashambulizi yake kwenye majengo mengi katika ukanda wa Gaza ambako maeneo ya wanajeshi wa Hamas yanasemekana kuwepo.
#EastAfricaTV
Israeli Prime Minister Netanyahu urges Gaza residents to leave to other countries: "Gazans’ should flee", as time to start ground operation approaches.
Vita vya Israeli na Palestina (hali ya asubuhi ya 08.10.23) .
✍IDF haijaweza kutimiza ahadi zake za kusafisha maeneo yote yaliyotekwa na adui usiku. Ufagiaji unaendelea.
✍ Mapigano makali yameanza upande wa mpaka wa israel na lebanon.
✍Ndege zisizojulikana zimeingia kwenye anga ya israel.
✍Inadaiwa mpaka sasa zaidi ya wanajesh+ rais wa israel 200 wameuwawa huku majeruhi kuwa zaidi ya 1500.
✍ Israel imedai kushambulia malengo 10 katika ukanda wa Gaza waliodai na maeneo ya vikundi vya Hamas.
Lakini jambo muhimu zaidi ni kwamba tangu jana, raia wa Israeli wameacha kujihisi salama na wameacha kuamini kwamba jeshi lao litawalinda kwa njia yoyote. Na huu ni ukweli mwingine ambao nchi italazimika kuishi nao sasa.
Haijalishi ni jinsi gani Israeli italipa kisasi sasa, haijalishi inafanya nini, haijalishi inapiga kikatili kiasi gani kujibu, jambo baya zaidi kwa serikali ya Israeli tayari limetokea. Ile taswira ya kutoshindwa kwa IDF na kuwepo kila mahali kwa huduma za kijasusi za Israeli imetikiswa siku ya Jana.