Anayeona missed calls zako mara kwa mara alafu hakupigiii kwa namna flani anakuona huna umuhimu katika maisha yake punguza kujipa umhimu kwenye maisha ya mtu wa namna hioโ๏ธ
Watu hawataki kuingia kwenye madawa, watu hawataki kulewa kupindukia, hakuna anayependa kujidunga dunga tuu. Watu wana maumivu, watu wana msongo wa mawazo, watu wanataka tu kupata amani ya moyo na furaha, watu wanaomba njia wasaidiwe kuwa na maisha bora kila siku wanaomba huo msaada. Hawana shida na mtu, wao wana shida na wao wenyewe.
Watu wanaona bora wafanye vilivyokithiri ili tu waweze kuingia kwenye kidunia chao ambacho chenyewe kina amani, furaha na kila kitu good good. Watu wasaidiwe. Tusaidiane.
Watu wamepoteza pesa, nyumba, biashara, kazi, mke, mtoto, mama, baba, watu wamepoteza watu wanaowapenda na kila walichokiona kwao ndio dunia, watu wanaiona dunia yao ikifa huku wao wakiwa hai. Watu wasaidiwe. Tusaidiane. Hata kwa kumsikiliza tu mtu, unaweza mbadilishia maisha.