China ina Takribani wanafunzi 300,000 wanaosoma USA.
China ina Takribani wanafunzi 90,000 wanaosoma UK.
LAKINI ndani ya China Mwaka Huu 2026 Wanafunzi Takribani Million 13 Wamefanya Mtihani wa Gaokao.
Mtihani wa Gaokao ndio Mtihani Mgumu zaidi duniani, Tanzania Idadi ya Watahiniwa inapanda, China Inazidi Kupungua.
Sababu ni Kuwa wanafunzi wengi wameanza Kukimbia mtihani Huo ambao wakati unafanyika hata Safari za Ndege ndani ya China Hupunguzwa, Magari hayaruhusiwi kupita Jirani na vyumba vya mtihani, Watoto wengi Hujiua kabla na baa da ya Matokeo.
Unaweza Soma zaidi Hapa:
https://t.co/tOOpzYqHfw
"Mwingine anaamka asubuhi anasema kesho tutaandamana na kwasababu ya kilichotokea Oktoba 29 taifa linalazimika kuwa na wasiwasi, Mamlaka lazima ziwe na wasiwasi kwasababu wasiwasi ni akili, Vyombo vya dola kama Polisi, Majeshi watakuwa huku na huku hata kama mtu alizungumza kijuhajuha tu na ni kwasababu kilichosababisha watu kufikiria kuandamana bado hakijashughulikiwa."
"Tutatumia nguvu ndio kuzuia lakini tatizo bado halijatatuliwa kwahiyo kumbe kuzuia haya maandamano ni kutumia nguvu kwa kutumia rasilimali za Nchi lakini kukomesha hili ni jambo dogo tu kukubaliana ili jambo husika litekelezwe mambo mengine yaende. Yaani ni simple tu."
"Mwingine anasema ana kikosi lakini kuandamana ni haki ya kikatiba ila kwasababu tatizo halijatatuliwa tunakaribisha kila aina ya takataka, kila tatizo. Wasiotutakia mema wanaweza pia kutumia nafasi hii hii." -Seleman Msindi maarufu kama Afande Sele.
🚨𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄
Ujumbe wa aliyekuwa Mbunge wa Arusha mjini @godblessjlema1 kuhusu suala la ndoa baada ya @pastor_roseshaboka kusema ana Degree 4 hivyo hawezi kuishia kupika na kufua.
“Tatizo la zama hizi ni kwamba tunawasilisha ndoa kana kwamba ni gereza la ndoto, wakati ukweli ni kwamba ndoa bora ni mahali ambapo ndoto za pande zote mbili hukua. Lakini juu ya ndoto zote kuna ndoto moja kuu zaidi, kuishi kwa furaha, upendo, heshima na unyenyekevu”
“Kufua boxer au kupika ukiwa na degree nne si udhaifu, kama ambavyo elimu si kipimo cha ubora wa ndoa wala thamani ya mtu. Mambo haya yanaweza kuishi pamoja bila mgongano”
“Elimu haimfanyi mtu kuwa mkubwa kuliko huduma, na huduma haipunguzi hadhi ya mtu. Mtu anaweza kuwa na shahada nyingi, akaongoza na kubadilisha jamii, na bado akachagua vitendo vya upendo ndani ya ndoa. Hilo si kushushwa hadhi, ni uchaguzi wa upendo”
“Tatizo huanza pale majukumu ya kifamilia yanapoonekana kama adhabu badala ya kujitoa. Ndoa si mashindano ya vyeo au vyeti, bali ni safari ya kuulizana, Leo nitakufanyia nini ili maisha yetu yawe bora zaidi”
“Ndoto za mtu mmoja mmoja zina thamani, lakini ndoa yenye afya hujengwa pale ambapo “sisi” inakuwa kubwa kuliko “mimi”. Wakati mwingine mmoja huweza kuahirisha au kubadilisha ndoto yake kwa ajili ya familia, huo si udhaifu, ni ukomavu”
“Mwisho wa yote, ndoa haijengwi na degree wala cheo, bali na upendo, heshima, unyenyekevu na kujitoa. Hapo ndipo ndoto mbili zinapogeuka kuwa maisha bora ya pamoja. Mwanamke hapaswi kuzuiwa kukua katika elimu na maarifa, lakini pia anapaswa kuelewa kuwa ukuaji wake wa kweli huonekana zaidi pale anapolinda ndoa kwa unyenyekevu, busara na hekima kama ilivyo kwa mwanaume pia”
“Ndoto za mtu mmoja zinakuwa muhimu, lakini katika ndoa yenye hekima, ‘mimi’ hufa ili ‘sisi’ iishi kwa upendo, heshima na unyenyekevu.”
NB: Pengine My beloved Sisy Rose alikuwa na msingi mzuri kwenye hoja yake lakini pengine uwasilishaji wake tu ulipaswa kwenda mbele zaidi kwa unyenyekevu na maarifa. Maana ikieleweka juu juu ni hatari sana.
#MeaMswahiliUPDATES