Leo nimeshiriki maadhimisho ya siku ya wafugaji na wakulima (Nane nane) yaliyofanyika Mkoani Mbeya, ambapo Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr @SuluhuSamia alikuwa mgeni rasmi wa shughuli hiyo
Namshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutuwezesha kukutana mapema leo Jijini Mbeya, katika kilele cha Maonesho ya Thelathini ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi (Nane Nane).
Nawapongeza mamilioni ya wakulima, wavuvi na wafugaji katika kila kona ya nchi yetu kwa juhudi zenu katika uzalishaji, na kuendelea kulilisha Taifa letu. Kazi zenu za kila siku zinaipa nchi yetu si tu uhakika wa chakula lakini pia ajira (zaidi ya asilimia 65), malighafi kwa viwanda vyetu (zaidi ya asilimia 60), na zinachangia zaidi ya robo ya Pato la Taifa letu.
Tumeongeza Bajeti katika Kilimo lakini pia katika Mifugo na Uvuvi ili tutekeleze mipango tuliyojiwekea katika sekta hizi muhimu kwa uchumi na maisha ya kila Mtanzania.
Nazipongeza Wizara zote mbili kwa programu nyingi bora na mahususi zinazoendelea kutekelezwa. Programu mojawapo ni Jenga Kesho Iliyo Bora, inayowapa vijana na wanawake mafunzo ya kilimo, umiliki wa ardhi kwa zaidi ya miaka 66 na nafasi ya masoko ya mazao yao.
Kwa namna ya kipekee, Serikali itaendelea kutoa ruzuku katika mbolea na pembejeo. Nimeagiza Wizara ya Kilimo kukaa na Wizara ya Fedha ili kuondoa gharama za kusambaza mbolea kwa ngazi ya kata ambazo zinafanya bei ya mboleo kwa mkulima kuwa juu.
SACP David Misime – Msemaji wa Jeshi La Polisi, akitoa mhadhara kuhusu “Nafasi ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika Kujenga na Kukuza Umoja wa Kitaifa” kwa Washiriki wa Kozi Fupi ya kumi na Tano ya Wahariri wa Vyombo vya Habari tarehe 03 Agosti, 2023.
Leo nchi yetu inaadhimisha siku adhimu kuwakumbuka mashujaa wetu. Hii ni miamba na majabali ya kihistoria ambayo kwa kujitoa kwao kwa hali na mali kumetufanya sisi kuwa huru, kuishi huru, kuwa na Taifa letu, nyumbani kwetu, na kuwa hapa tulipo kama nchi.
Tunajenga mnara mrefu zaidi barani Afrika katika Jiji la Dodoma kama sehemu ya kuendelea kuwaenzi mashujaa wetu. Mnara huu ni alama nyingine ya uhuru wetu, shukrani yetu na kujitambua kwetu wapi tumetoka, wapi tupo na wapi tunakwenda. Nawaelekeza Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Fedha na wote wanaohusika na ujenzi huu wa kihistoria kuhakikisha unakamilika kwa wakati na kwa viwango.
Siku hii pia ni siku ya tafakari. Tafakari ya kuendelea kuyaishi waliyoyaamini na kuyasimamia mashujaa wetu kwa kutunza amani, umoja, utulivu, mshikamano na kufanya kazi kwa bidii kwa Taifa letu.
Katika siku hii muhimu, tuendelee pia kukumbuka na kuzingatia kuwa Tanzania ni moja, itabaki kuwa moja na kamwe haitagawanyika. Tusikubali na hatutaruhusu mtu yeyote au kikundi chochote kutugawa kwa kisingizio chochote kile.
Mwenyezi Mungu Ibariki Afrika.
Mwenyezi Mungu Ibariki Tanzania.
Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha mzee Hemedi Bakari Mkali, Mwenyekiti wa Wazee wa Dar es Salaam. Pole kwa wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam, familia, ndugu, jamaa na marafiki. Tangu harakati za kudai uhuru na hata sasa, kujitoa kwa hali na mali, na busara za wazee wa Dar es Salaam na kwingine kote nchini kumekuwa sehemu muhimu ya ushauri na mwanga katika mambo yenye kuleta tija kwa nchi yetu. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Samia Suluhu Hassan, ameongoza Kikao Cha Halmashauri kuu ya CCM Taifa kilichotanguliwa na Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Leo, Julai 09,2023 katika Ukumbi Wa (White House) Jijini Dodoma .
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg. Samia Suluhu Hassan, ameongoza Kikao Cha Halmashauri kuu ya CCM Taifa kilichotanguliwa na Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Leo, Julai 09,2023 katika Ukumbi Wa (White House) Jijini Dodoma.