Nimeona video imesambaa mtandaoni, maiti ya mwanaume imeokotwa ikiwa imekatwa kichwa, inaelea katika bonde la mto Msimbazi eneo la Tabata. Baadae nakutana na chapisho la msanii, Mh. Temba anasema ni mjomba wake anaitwa James Temba. Nchi yangu imeharibika sana. Tumefikaje hapa?
Zamani haikuwa ishu lakini nowadays kuchinja kuku, ukiona anavyopigania roho, lazima uingie huruma.
Lakini kuna mtu ana ujasiri wa kumkata kichwa binadamu mwenzake na kutupa mwili wake mtoni.
Kichwa chake hatujui kiko wapi.
Tumefikaje hapa?
Ukatili wa daraja hili, Tanzania?
F1 is the footage that surfaced this weekend on social media portraying a headless corpse of a male human being.
The voice from the footage alleges the corpse to be found in Tabata area, the suburb of Dar Es Salaam
Today I have received credible information that the deceased has been positively identified by his family members as JAMES TEMBA, a second year student at the Institute of Finance Management
I’m closely following up the scene to understand the motive of his supposedly culprits
Nchi nyingi — kuanzia Australia hadi Denmark — sasa zinaweka mipaka ya matumizi ya mitandao ya kijamii kwa watoto walio chini ya miaka 16.
Kwa vijana wa Tanzania na Africa: lindeni akili zenu, muda wenu, na ndoto zenu.
Mitandao ya kijamii inapaswa kukutumikia wewe — si kukuteka wewe.
Viumbe waliohamia ACT na CHAUMMA kutafuta ubunge uchaguzi wa 2025, wanamsikiliza vizuri na kumuelewa, Mzee Selemani Saidi Ally Bungara (Bwege)?
Mzee Bwege ni mbunge mstaafu katika Jimbo la Kilwa Kusini katika kipindi cha miaka 10 - kuanzia 2010 hadi mwaka 2020, kupitia (CUF) kabla ya kuhamia ACT.
Ni mwanachama wa ACT; anasema wenzake wamekubali kufanya utapeli na CCM. Kwamba CHADEMA wapo sahihi kubeba agenda ya NO REFORMS, NO ELECTION
Kwamba, (chama chake) ACT - wazalendo wanasubiri huruma ya CCM kupata wabunge. Wanaomba wapewe wabunge. Wakati CHADEMA wameamua kudai haki.
Kwamba ACT wanakwenda kushiriki uchaguzi kwa huruma ya CCM na siyo kushindana katika uchaguzi. ACT wanaomba haki. Wakati CHADEMA wanadai haki.
Mzee Bwege anasema CHADEMA wasishiriki uchaguzi, na wavumilie miaka 5 bila ruzuku, ikifika 2030, CHADEMA itaungwa mkono na watu wenye akili timamu
Mzee Bwege anasema ACT na wenzao wanaoshiriki uchaguzi wanatumia maneno ya khanga na jikoni kuwalaghai wananchi ili kurahisisha biashara ya CCM,
Na kwamba, lengo la kushiriki uchaguzi ni kuhalalisha huo UCHAGUZI. Mzee Bwege anasema CHADEMA wamebadili upepo, hawaombi haki. Wanadai haki.
Watanzania wengine wengi wanaweza kuchelewa kuwaelewa CHADEMA kwa hatua walizochukua sasa, lakini watawaelewa baadae, nchi ikiwa salama.
Bwege anasema wao (ACT), hawajui kama CCM watawaonea huruma na kuwapa wabunge au CCM watawakazia msuli na wasiwape hata mmoja.