Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Sita kutoka Tabora hadi Kigoma kwenye hafla iliyofanyika Katosho mkoani Kigoma tarehe 20 Julai, 2026.
Ni wakati muafaka sasa kufufua utekelezaji wa mradi wa kuifanya Kigoma kuwa special economic zone na Bandari ya Kigoma kuwa duty-free inland Port. Waheshimia Kafulila, Zitto, Simbakalia, nk watakuwa na kumbukumbu ya hilo suala.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anaendelea kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR Tabora-Kigoma, ambapo zaidi ya shilingi trilioni 6 zimeelekezwa katika mradi huo muhimu wa kimkakati.
Leo, 20 Julai, 2026, Mhe. Rais ataongoza uzinduzi na uwekaji wa jiwe la msingi wa mradi huo katika eneo la Katosho, Kigoma.
Kazi na Utu, Tunasonga Mbele.
Tembelea: https://t.co/XFsl2QgHBH
__________
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#CCMIpoKazini
#TanzaniaKwanza
My comments here siyo kuhusu taarifa hii. Naangalia akaunti zote hizo za Ikulu kwenye mitandao ya Kijamii. Halafu sipati jawabu ya juhudi za serikali kutishia kufunga mitandao hiyo wakati inapo tumika kuikosoa Serikali. Kutangaza taarifa zao ni poa lakini siyo kuzikosoa.
Fuatilia matangazo ya moja kwa moja kupitia akaunti zetu za Instagram: ikulu_mawasiliano, Facebook: Ikulu Tanzania Facebook fanpage: Ikulu Mawasiliano, Twitter: ikulu_Tanzania Youtube Channel:
Ikulu Tanzania na Tovuti: https://t.co/Ma2oVK5f15
#TanzaniaYetuSote#NchiYetuKwanza
#MaendeleoEndelevu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuzindua meli nne mpya za mizigo zenye uwezo wa kubeba tani 2,000 kila moja katika hafla ya kitaifa itakayofanyika Julai 20, 2026 mkoani Kigoma, hatua inayolenga kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa mizigo na kuimarisha biashara katika ukanda wa Ziwa Tanganyika.
Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa leo Jumapili Julai 19, 2026 , amesema meli hizo zimetengenezwa na kampuni ya Gold Voyage Logistics Limited kutoka China na zitatoa mchango mkubwa katika kusafirisha mizigo kati ya Tanzania na nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Burundi na Zambia kupitia Ziwa Tanganyika.
Amesema uzinduzi huo unaenda sambamba na mkakati wa Serikali wa kuifanya Kigoma kuwa lango kuu la biashara kuelekea masoko ya Afrika ya Kati kwa kuimarisha usafiri fungamanishi unaojumuisha reli, bandari na usafiri wa majini kwa mujibu wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Prof. Mbarawa amesema ongezeko la biashara katika ukanda huo linaonekana kupitia takwimu za Bandari za Ziwa Tanganyika zilizohudumia tani 815,285 za shehena katika mwaka wa fedha 2025/26, ikilinganishwa na tani 397,897 mwaka 2024/25, hali inayoonesha mahitaji makubwa ya miundombinu ya kisasa ya usafirishaji.
Ameeleza kuwa Serikali pia imejipanga kuboresha Bandari ya Kigoma kwa kujenga gati la kisasa la abiria na mizigo ili kuhudumia meli mpya pamoja na zilizopo, hatua itakayoongeza uwezo wa bandari hiyo kuhudumia biashara za ndani na za kimataifa.
Prof. Mbarawa amewaalika wananchi wa Kigoma na Watanzania kwa ujumla kushiriki hafla hiyo muhimu, akieleza kuwa miradi hiyo itaongeza fursa za biashara, uwekezaji na ukuaji wa uchumi wa Taifa huku ikiimarisha nafasi ya Tanzania kama kitovu cha usafirishaji katika ukanda wa Maziwa Makuu.
Ndio utapeli unaofanywa na wanasiasa wa Tanzania, kila kitu ujanja ujanja. Elimu ya juu imegeuzwa kuwa tissue paper, inapangusa upumbavu wa watawala tu.
Chukulia mfano Mwigulu Nchemba. Wakati anafanya PhD pale UDSM 2012 - 2017, alikuwa pia Mbunge anayehudhuria vikao vya Bunge Dodoma, Mjumbe wa Kamati za Bunge za Bajeti, Katibu wa NEC wa Uchumi na Fedha, Mhazini wa CCM, Naibu Waziri wa Fedha, Waziri wa Kilimo, na Waziri wa Mambo ya Ndani.
Chuo Kikuu cha Daresalaam @UDSTOFFICIAL kinatuaminisha kwamba wakati Mwigulu Nchemba anatekeleza majukumu yote haya aliweza pia kupata muda wa kujiandikisha kama mwanafunzi wa PhD full time.
Yani wakati anatekeleza majukumu yote haya, aliweza pia kuhudhuria vipindi vyote na kukamilisha coursework, akapata muda wa kufanya tafiti, kuchapisha makala, kuandika dissertation, halafu kama haitoshi, akamaliza yote haya ndani ya miaka mitano na kutunukiwa PhD.
Unless haufahamu what it takes kufanya PhD, huu ni muujiza wa hali ya juu.
Hata hivyo haishangazi kwa sababu ni UDSM hii hii ailiyompa Samia PhD ya heshima mara baada tu ya kuingia madarakani.
Kiongozi wa zamani wa ACT- Wazalendo na Mbunge Mstaafu wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, amesema uzinduzi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Tabora hadi Kigoma unaotarajiwa kufanywa na Rais Samia Suluhu Hassan wiki hii ni hatua muhimu kwa maendeleo ya mkoa huo, lakini amesisitiza kuwa manufaa kamili ya reli hiyo hayatapatikana iwapo Serikali haitakamilisha mradi wa chelezo cha meli na kiwanda cha ujenzi wa meli cha Katabe.
Katika uchambuzi wake, Zitto amesema wananchi wa Kigoma walipigania ujio wa reli ya kisasa si kwa ajili ya usafiri wa abiria pekee, bali kama sehemu ya mfumo mkubwa wa usafirishaji wa mizigo unaounganisha Bandari ya Kigoma, Ziwa Tanganyika na mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), eneo lenye utajiri mkubwa wa madini.
Amesema mradi wa chelezo cha Katabe wenye thamani ya zaidi ya Sh600 bilioni, uliozinduliwa mwaka 2023 kwa kushirikiana na kampuni ya Dearsan kutoka Uturuki, umekwama kutokana na ukosefu wa fedha.
Kwa mujibu wake, mradi huo ulilenga kujenga na kuhudumia meli kubwa za mizigo ambazo zingebeba mabehewa ya reli moja kwa moja kutoka Kigoma kwenda Kalemie nchini DRC na kurejesha madini kupitia Bandari ya Dar es Salaam.
Zitto ameeleza kuwa kusimama kwa mradi huo kunaiathiri Tanzania kushindwa kutumia kikamilifu fursa ya kijiografia na biashara inayotokana na uzalishaji wa madini, ikiwemo lithiamu kutoka mgodi wa Manono nchini DRC.
Amesema DRC ina uwezo wa kupitisha zaidi ya tani milioni 20 za mizigo kwa mwaka kupitia Kigoma, jambo ambalo lingeongeza kwa kiasi kikubwa shughuli za Bandari ya Dar es Salaam na kukuza uchumi wa taifa.
Aidha, amehoji ukosefu wa uratibu kati ya taasisi za Serikali akieleza kuwa Shirika la Reli Tanzania (TRC) linaendelea na ujenzi wa SGR wakati Shirika la Meli Tanzania (MSCL) limeshindwa kuendelea na mradi wa chelezo, licha ya miradi hiyo kubuniwa kutekelezwa kwa wakati mmoja kama miradi pacha inayokamilishana.
Zitto amemtaka Rais Samia kutumia ziara yake Kigoma kutembelea eneo la Katabe na kuwataka wasaidizi wake kutoa majibu kuhusu hatima ya mradi huo.
Amesisitiza kuwa bila chelezo na kiwanda cha meli cha Katabe, Reli ya Kisasa ya Tabora–Kigoma itapoteza sehemu kubwa ya manufaa yake ya kiuchumi yaliyokusudiwa, huku akieleza kuwa kukamilika kwa mradi huo kungefungua maelfu ya ajira na kuifanya Tanzania kuwa kitovu kikuu cha usafirishaji katika ukanda wa Afrika Mashariki, Maziwa Makuu na Afrika ya Kati.
Mhe @zittokabwe ilishauri awali kuwa SGR ianzie DAR KGM halafu TBR MZA, tukapuuza. Akashauri tuchimbe mkaa wa mawe na chuma kabla ya SGR, tukapuuza. Sasa tunaona sdhari za kukataa ushauri wake. Safari hii bora tumsikilize na kutathmini kwa kina ushauri wake.
Kiongozi wa zamani wa ACT- Wazalendo na Mbunge Mstaafu wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, amesema uzinduzi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Tabora hadi Kigoma unaotarajiwa kufanywa na Rais Samia Suluhu Hassan wiki hii ni hatua muhimu kwa maendeleo ya mkoa huo, lakini amesisitiza kuwa manufaa kamili ya reli hiyo hayatapatikana iwapo Serikali haitakamilisha mradi wa chelezo cha meli na kiwanda cha ujenzi wa meli cha Katabe.
Katika uchambuzi wake, Zitto amesema wananchi wa Kigoma walipigania ujio wa reli ya kisasa si kwa ajili ya usafiri wa abiria pekee, bali kama sehemu ya mfumo mkubwa wa usafirishaji wa mizigo unaounganisha Bandari ya Kigoma, Ziwa Tanganyika na mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), eneo lenye utajiri mkubwa wa madini.
Amesema mradi wa chelezo cha Katabe wenye thamani ya zaidi ya Sh600 bilioni, uliozinduliwa mwaka 2023 kwa kushirikiana na kampuni ya Dearsan kutoka Uturuki, umekwama kutokana na ukosefu wa fedha.
Kwa mujibu wake, mradi huo ulilenga kujenga na kuhudumia meli kubwa za mizigo ambazo zingebeba mabehewa ya reli moja kwa moja kutoka Kigoma kwenda Kalemie nchini DRC na kurejesha madini kupitia Bandari ya Dar es Salaam.
Zitto ameeleza kuwa kusimama kwa mradi huo kunaiathiri Tanzania kushindwa kutumia kikamilifu fursa ya kijiografia na biashara inayotokana na uzalishaji wa madini, ikiwemo lithiamu kutoka mgodi wa Manono nchini DRC.
Amesema DRC ina uwezo wa kupitisha zaidi ya tani milioni 20 za mizigo kwa mwaka kupitia Kigoma, jambo ambalo lingeongeza kwa kiasi kikubwa shughuli za Bandari ya Dar es Salaam na kukuza uchumi wa taifa.
Aidha, amehoji ukosefu wa uratibu kati ya taasisi za Serikali akieleza kuwa Shirika la Reli Tanzania (TRC) linaendelea na ujenzi wa SGR wakati Shirika la Meli Tanzania (MSCL) limeshindwa kuendelea na mradi wa chelezo, licha ya miradi hiyo kubuniwa kutekelezwa kwa wakati mmoja kama miradi pacha inayokamilishana.
Zitto amemtaka Rais Samia kutumia ziara yake Kigoma kutembelea eneo la Katabe na kuwataka wasaidizi wake kutoa majibu kuhusu hatima ya mradi huo.
Amesisitiza kuwa bila chelezo na kiwanda cha meli cha Katabe, Reli ya Kisasa ya Tabora–Kigoma itapoteza sehemu kubwa ya manufaa yake ya kiuchumi yaliyokusudiwa, huku akieleza kuwa kukamilika kwa mradi huo kungefungua maelfu ya ajira na kuifanya Tanzania kuwa kitovu kikuu cha usafirishaji katika ukanda wa Afrika Mashariki, Maziwa Makuu na Afrika ya Kati.
Kiwango kimoja cha kumtegemea Mwenyezi Mungu ni kumuomba Yeye pekee kwa kila hitaji letu. Kiwango cha juu zaidi ni kumwachia kila jambo, ukiwa na yakini kwamba kwa hekima Yake isiyo na mipaka, Atakupa kilicho bora zaidi, kwa wakati na namna Anayoiona kuwa sahihi. 🤲
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi, ambaye ni Waziri wa Ushirikiano wa Kikanda Mhe. Floribert Anzuluni Isiloketshi, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 19 Julai, 2026.
Vyombo kadhaa vya habari Tanganyika hupotosha mambo muhimu katika taarifa zao. Nahisi kwa kujua au kutojua vinakuwa kama kasuku kwa kunukuu taarifa zisizo sahihi. Ni kweli kuna Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Mwungano wa Tanzania? Ni Bandari za Tanzania au za Tanganyika na za Zanzibar.
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, ameishutumu Serikali kwa kile alichodai kuwa ni usimamizi usio na uwazi wa ununuzi wa mafuta nchini, akidai wananchi wanaendelea kubeba mzigo wa kupanda kwa bei za mafuta wakati tatizo halitokani tu na hali ya soko la dunia bali pia na namna mikataba ya ununuzi inavyosimamiwa.
Akizungumza mbele ya wazee wa Tarime mkoani Mara, Heche amesema hoja ya Serikali kwamba kupanda kwa bei ya mafuta kunasababishwa na vita vya Mashariki ya Kati haiwezi kueleza tofauti kubwa ya bei ambazo Tanzania inanunua mafuta ikilinganishwa na baadhi ya nchi jirani.
Amesema Tanzania ina mfumo wa Bulk Procurement System (BPS) unaoratibiwa na Serikali kwaajili ya kununua mafuta kwa pamoja, pamoja na kuwa na miundombinu ya kuhifadhi mafuta iliyoanzishwa tangu mwaka 1978.
Heche amedai kuwa tangu Februari mwaka huu, TPDC ilimpa kampuni ya Vitol jukumu la kusambaza mafuta bila ushindani wa wazi wa zabuni ambapo kwa mujibu wa madai yake, kampuni hiyo huiuzia Tanzania tani moja ya mafuta kwa kati ya dola za Marekani 200 hadi 260, huku ikiuza mafuta hayo kwa Uganda kwa takribani dola 80 na Msumbiji kwa dola 90 kwa tani.
"Hakuna biashara ya namna hii duniani. Mafuta yakipanda bei kila kitu kinapanda bei. Huu wizi unaisimamiwa na serikali, wanaibia wananchi maskini." amesema Heche.
Kiongozi huyo wa upinzani amehoji pia umiliki wa kampuni inayosambaza mafuta, akisema ni muhimu Serikali kuweka wazi taarifa za wanahisa na wamiliki wake ili kuondoa mashaka yanayotolewa na wananchi.
Aidha, amedai kuwa hata katika sekta ya gesi, mgawo wa mali za Songosongo kwa kampuni ya Amber Energy umeibua maswali mengi yanayohitaji majibu ya wazi kutoka kwa Serikali.
Heche amesisitiza kuwa hoja zake hazilengi kupinga uwekezaji, bali kutaka uwajibikaji na uwazi katika usimamizi wa rasilimali za taifa, akitoa wito kwa Serikali kuweka hadharani mikataba ya ununuzi wa mafuta na maelezo ya kina kuhusu namna bei zinavyopangwa ili wananchi waelewe sababu halisi za gharama wanazobeba.
Utasikia, “Mheshimiwa, tuko pamoja” Kama maneno haya yangekuwa vitendo, CHADEMA ingekusanya Bilioni 1 ndani ya masaa 12.
Bilioni 1 ni watu 500,000 wakitoa Sh 2,000 kila mmoja; watu 100,000 wakitoa Sh 10,000 kila mmoja; au watu 100 tu wakitoa Sh Milioni 1 kila mmoja. Tusiruhusu maadui zetu watucheke. Tusimame kwa vitendo, si kwa maneno pekee.
Tukiamua, tunaweza kukusanya hata Bilioni 10 ndani ya wiki moja. Impossible is Nothing.
M-PESA: CHADEMA HQ – 0744 446 969
CHADEMA NMB: 22606600140
Vijana ndiyo nguvu ya taifa. Tusisubiri wengine wajenge harakati tunazoziamini. Tuchangie kwa hiari, kwa uwazi na kwa uwezo wa kila mmoja. Kila shilingi ni hatua ya kujenga chama imara kinachowajibika kwa wanachama na wananchi. #ChamaChetuWajibuWetu#NguvuYaWananchi
M-PESA: CHADEMA HQ - 0744446969
CHADEMA NMB: 22606600140