Binafsi nakuelewa mzee sana tu hicho unachosema
"Na kila alipozidi kwenda kutafuta msaada huko alizidi kwenda chini"hii kauli imebeba tafsiri kubwa ya vijana na wazee kujifunza
Nina jamaa yangu anafanya biashara ya genge yenye mtaji usiozidi 2M.
Ameoa, amekodi chumba na ana watoto 2.
Matumizi yake ya siku kwenda kuchukua mzigo sokoni hauzidi 300K na mauzo yake ya siku ni almost 130K mpaka 200K.
Kipindi cha nyuma hapa alipata changamoto ya ku loose kwenye biashara yake na kuanza kuporomoka mpaka hata kodi ikafikia wakati haimudu, si ya chumba wala frem
Baada ya kupata changamoto hio akaenda kwa waganguzi kumtazamia tatizo nini mpaka biashara yake haiendi.
Jamaa alitumia gharama sana kusafiri kwenda maeneo tofautitofauti kusafisha nyota na kuondoa zindiko ambalo ameambiwa limewekwa na majirani zake
Kadiri alivyokua akitoka kutafuta ufumbuzi ndivyo alikua anazidi kuporomoka. Mpaka sasa frem kaifunga na chumba karejesha na mke kamuacha sasaivi anapiga deiwaka.
Ukweli mim nashindwa kumshauri kuhusiana kuachana na dhana za ushirikina maana mwenyewe ndio imani yake.
Kuna ile hali ambayo una mshahara wa laki 800,000 lakini ndoto zako zina thamani ya milioni 500.
Nyumba unayotaka ni milioni 120.
Biashara unayotaka ni milioni 50.
Gari unalotaka ni milioni 55.
Hiyo ni kawaida ukiwa kijana wa Tamisemi .