Hey Tanzania! 🇹🇿
So many of you have asked me: “When will NALA launch for Tanzanians in Tanzania?” 👀
If you want to store money in USD or receive funds from abroad, we’d love your feedback.
Take 2 mins to share your thoughts to help us build NALA👇
https://t.co/YykthqhY43
@mpenda_TANZANIA@Jambotv_ Umesahau Green guard, polisi na wasiijulikana tena hawa ndio hatari sana kwa nchi yetu. Nakukumbusha tu ongeza hapo kwenye orodha yako.
@fumbokhanJr@Baraza_Kuu Kweli amani ni kitu muhimu sana lakini hatuna amani tunatekwa, tunauawa na kupotezwa, tukiandamana kwa amani tunapigwa na kuvunjwa vunjwa. Hatuna amani. Labda kama sijui tafsiri ya amani mtanisaidia.
Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu, Robert Makaramba atoa tafakari juu tukio la Polisi kuwapiga wafuasi wa CHADEMA katika Mahakama Kuu.
"Nilikuwa nashangaa Polisi ndiye anayepaswa kujua kwamba Mahakama imejaa au ni uongozi wa Mahakama ndiyo unapaswa kusema pamejaa, na kujaa maana yake ni nini?"
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 32
Anaendelea Mhe. Lissu
Sasa Waheshimiwa Majaji wakili wa serikali akaenda kwenye kifungu cha 39(d) cha Penal Code yaani Kanuni ya Adhabu juu ya Uhaini na akarudi kesi za Grey Likungu Mataka.
Na akasema kwa Mujibu wa Grey Likungu Mataka kwamba mambo yanayofanya kosa la uhaini ni matatu makuu ndio alivyosema Katuga.
1. Utiifu kwa jamhuri ya muungano
2. Kutengeneza nia yaani nia ya kutenda kosa la uhaini.
3. Uthibitisho wa kutenda hiyo nia ya kosa la uhaini. Manifestation.
Wakili wa serikali amesema hayo masharti matatu sio pekeee.
Sasa mimi namuuliza so what?
Hayo masharti mengine mimi sijalalamikia.
Utiifu kwa jamhuri mimi sina shida na sharti hilo na hoja yangu haipo hapo.
Hoja yangu ni kwamba kulikuwa na nia ya kuunda kosa la uhaini.
Na pili hiyo nia ilithibitishwa kama inavyotakiwa?
Sharti la pili la hicho kifungu cha 39(2) cha Penal Code. Hati ya mashitaka inapaswa kuonyesha ulitengeneza nia ya kutenda kosa la uhaini.
Taarifa iliyoko mbele yenu waheshimiwa majaji inasema nilitengeneza nia ya kuhamasisha watu kuzuia uchaguzi mkuu.
Anaisoma hapo hiyo taarifa yaani Charge sheet ile hati ya mashitaka.
Wakili wa serikali hajagusa hilo hata kidogo kwamba nilihamasisha watu kuzuia uchaguzi sio kosa la uhaini wala kosa lolote la jinai.
Amekimbia kwenye hili
Hajagusa hata kidogo. Hakuna nia na sijatengeneza nia ya kutenda uhaini.
Ila nimetengeneza nia ya kufanya watu kuzuia uchaguzi wa Tanzania na hiyo sio kosa la uhaini.
Huwezi kuelewa mambo haya kama hujui sheria.
Nilisema mambo yako zaidi ya 10 yanayotengeneza kosa la uhaini wakili wa serikali akasema yako 13 sasa naomba kumuuliza kwenye hayo 13 je ni kitendo gani kinasema kuzuia uchaguzi ndio uhaini? Hakipo na hajasema hapa.
Wakili wa serikali Mkuu alivyokimbia kwenye hoja hiyo akasema kwamba.
Hii taarifa iko sawa sawa kwasababu imetaja jina langu, tarehe, kwamba mimi ni mtiifu wa jamhuri hayo yote wapi nilisema yana shida?
Anasema alitengeneza nia ya kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025. Kama nilivyosema Waheshimiwa Majaji hilo sio kosa wala sio inshu kabisa.
Infact kwa kusema hayo anathibitisha niliyosema nia ni kuzuia uchaguzi. YES. That is not an offence under the laws of the National Republic of Tanzania.
Anasema kwa lengo la kuitisha serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Watu wazuie itishike Serikali. Waheshimiwa majaji naomba angalieni hiyo information kuna mahali nimetaja serikali? Huwezi kusema ana lengo la kuitaja serikali wakati hajaitaja serikali sikutaja hata MWENYEKITI WA KIJIJI sio serikali tu.
Sasa hayo anayosema yalipaswa kuwepo kwenye taarifa yanapaswa kuwepo kwenye hati ya mashitaka.
Iseme ulitisha serikali yenyewe inasema nilikuwa na nia ya kuzuia uchaguzi, hakuna kosa la kumshitakia mtu hapa labda uwe hujitambui.
Akasema haya mambo ni ya ushahidi. Sasa watambue kuwa tukienda kwenye ushahidi hawatakuja kusema ilitishwa serikali wakati humu wamesema walikuwa na nia ya kuzuia uchaguzi.
Wasifikiri tukienda kwenye ushahidi wasifikiri wataenda kwenye UVUVI WA USHAHIDI kwamba waseme lolote.
Na facts zako kwenye Charge sheet hazioneshi chochote kuhusu kutisha serikali na kosa la uhaini.
Hawatatengeneza kosa la uhaini kwenye ushahidi kosa linatengenezwa kwenye hati ya mashitaka.
Part 33 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 34
Anaendelea Mhe.
Kwahiyo kusema tusubiri ushahidi hakuna cha kusubiri ushahidi hapa maana hakithibitishiki na hakipo kabisa.
Na nimalizie hoja hii kwa kusema hivi Mahakama ya rufani kuanzia ile ya Afrika Mashariki na muhimu zaidi hii ya Tanzania. Zote zimesema "usipoweka haya mambo ya lazima kwenye hati ya mashitaka hakuna uhaini na shitaka hilo halipo." Hakuna nafasi ya kwenda nje ya msimamo wa mahakama ya rufani.
Sasa waheshimiwa majaji wakili wa serikali amezungumzia vilevile juu ya utaratibu wa kuandika hati za mashitaka za uhaini.
Ameenda kwenye Sect. 138 ya CPA na amesema haijatoa utaratibu wa namna ya kuandika mashitaka ya uhaini.
Angalau amekubali hilo sasa kama hakuna utaratibu tunaishia kwenye maelekezo ya kifungu hicho cha 138 cha CPA.
Sasa Majaji utaratibu wa kuandika hati za mashitaka haupo kwenye sheria za Tanzania ila upo kwenye maamuzi ya mahakama za Tanzania.
Usipokuwepo kwenye CPA sio kwamba haupo bali Mahakama ya rufani kwenye Khatibu Gandi ukurasa wa 22 na 23 ilisema kwa vile utaratibu huo haupo kwenye CPA utaratibu tutakaoutumia ni utaratibu uliotumika na mahakama ya rufani ya afrika mashariki kwenye Grey Likungu Mataka utaratibu huo uliowekwa kwenye Grey Likungu unasemaje?
1. Hati yamashitaka ya uhaini ionyeshe statement ya kosa.
2. Ionyeshe maelezo ya kosa la uhaini.
3. Lazima matendo ya kuthibitisha (overt act must be pleaded)
Hati ya uhaini ni LAZIMA iwe na mambo hayo matatu haipaswi kuwa kama hati ya mashitaka ya kosa la kuiba kuku.
Hii taarifa imetengenezwa na ofisi ya DPP iliyotengeneza hati ya mashitaka iliyotengeneza kwenye Grey Likungu Mataka na Khatibu Gandi.
Jaji Mkuu nyalali alisema niliulizwa na wakili wa serikali kulwa Masaba nieleze utaratibu ukoje...
Hivyo huu utaratibu unafahamika kwenye ofisi ya DPP. halafu kwenye hii ya kwangu wameleta kwa mujibu wa sheria ambazo hazipo maana utaratibu wanaufahamu na upo maofisini kwao wanachopatwa kukisubiria hapa ni HATI KUFUTWA.
Sasa Waheshimiwa majaji naomba kuzungumzia hicho kinachoitwa Amendment ya hati ya Mashitaka, kifungu cha 295 cha CPA, tumezungumza sana.
Kifungu kinafanya reference ya amendment ya hati ya mashitaka under s. 294 and the accused is not aware/ there must be notice.
Kwa kifupi ni kwamba lazima notice iwepo, kuhusu amendment ya Charge. Na s. 294 inasema mahakama kutoa amri ya kufanya amendment ya Charge.
Hivyo ukitaka kufanya marekebisho ya hati ya mashitaka, tumeambiwa tuende kwenye 294(2) na mahakama ndio inaleekeza hapo nini cha kufanya.
Sasa Mashitaka yalisomwa tar. 10/04 haya ya uhaini. Mahakama ya Kisutu haikuwa na mamlaka ya kufanya chochote ni kweli.
Sasa kifungu cha 295 kinaposema notice ambayo mshitakiwa amepatiwa hiyo notice ni nini?
Hiyo offence ambayo mshitakiwa amepewa nayo kuhusu kosa lake ni ipi kama sio Charge sheet? Hiyo ndio taarifa niliyopewa.
Sasa hiyo taarifa haiwezi rekebishwa kienyeji enyeji kupitia 294 yaani Mahakama lazima itoe ruhusa sio kujifanyia.
Hawajaomba ruhusa wamejifanyia inatakiwa ifutwe.
Na hayo marekebisho waliyofanya sio madogo, wanataka kurekebisha makosa yaliyokuwa kwenye Charge sheet wanafikiri yatawaokoa.
Hata baada ya hayo marekebisho hii hati ya mashitaka bado haiwaokoi wala kuwafikisha kokote.
Kuhusu maelezo ya mashahidi tuendelee hapo sasa.
Waheshimiwa Majaji wakili wa serikali amesema jambo moja kubwa sana.
Amesema kwamba taarifa ya kosa haina uhusiano wowote na maelezo ya mashahidi.
Kwamba taarifa inaweza kusimama yenyewe bila maelezo ya mashahidi. Akatoa ule mfano wa Chamber summons supported by affidavit.
Kwahiyo information sio lazima iwe na maelezo ya mashahidi.
Sasa Lengo kuu la Committal proceedings ni kukusanya maelezo ya mashahidi. Yakikamilika maelezo hayo basi 262(6) of CPA DPP anaandaa tarifa pamoja na maelezo ya mashahidi mahakama inayarudisha committal Court ili mshitakiwa akasomewe huko mahakama ya chini.
Part 35 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 33
Anaendelea Mh. Lissu.
Watu wanafurahi kumsikiliza.
Mawakili wa serikali wamesema hati ya mashitaka kuhusu publication na kifungu cha 39(2) cha Penal Code.
Publication maana yake maneno yaliyochapishwa kwenye karatasi yaani writing au printing.
Nilimsikia anasema nilichapisha na nikaweka kwenye mitandao ya kijamii.
Angalieni kwenye hati ya mashitaka kuwa nilichapisha kwenye mitandao ya Kijamii.
Sasa angalieni hayo maneno kama yapo kwenye hati ya mashitaka kuwa nilichapisha hayo maneno kwenye mitandao ya kijamii.
Kama yapo niambieni ili nikae chini kama maneno hayo hayapo hawawezi kuja kusema wakati wa ushahidi.
Hivyo basi publication by writing or printing haipo kokote sasa Waheshimiwa Majaji kuna kitu nimesikia kwa mara ya kwanza katika maisha yangu.
Kwamba maneno ni matendo. The deed of uttering words. Waheshimiwa majaji maneno sio matendo ieleweke vizuri.
Huyu Katuga ni mtu mwema sana alituletea maana ya deed kutoka Black's law dictionary anaisoma hapa.
Deed sio maneno, something that is done or carried out na sio kusema, kuongea. Hiyo ndio Deed.
😂😂😂😂Katuga alisoma maana ya Deed kwenye blacks law dictionary hakuelewa.
Anaendelea Lissu.
Kwa mara ya kwanza nimesikia kwa Katuga kuwa maneno ni matendo hiyo tafsiri tumuachie Katuga akae nayo mwenyewe ni yake.
Amegundua hili yeye.
Mahakama ya rufani ya Tanzania ilisemaje juu ya maneno na uhaini, nafikiri hata hili Katuga hajalielewa na halifahamu kabisa.
Tutaelekezana pia katika hili.
Mahakama ya rufani ya Tanzania ilisema hivi ...... Kwenye uhaini maneno ni nini?
Ukurasa wa 55 mere words do not amount to overt act on a treason charge na ikasema maneno matupu haitengenezi kosa la uhaini isipokuwa hayo maneno yanaelezea kitendo cha uhaini.
Maana yake ni kwamba wanaopanga uhaini wanakaa vikao na kupeana maelekezo hapo utasema maneno hayo ni vitendo vya uhaini eti kuhamasisha wananchi kuzuia uchaguzi. Hii ni kesi ya Khatibu Gandi.
Sasa kama Mahakama ya Rufani imesema Maneno hayatengenezi matendo ya uhaini nani anayeweza kubisha?
Ni huyu Katuga?
Pia ukurasa wa 67 inasema hivi Francis Nyalali Jaji mkuu anasema kanuni kuu maneno hayatengenezi matendo ya uhaini lakini wakiwa wengi inaweza kuwa vinginevyo na isipokuwa mshitakiwa akiwa mmoja huwezi kusema maneno yake yanatengeneza uhaini.
Kwa kifupi akisema mtu mmoja kama nilivyosema mimi na nikashitakiwa mtu mmoja kama nilivyoshitakiwa mimi basi hakuwezi kuwa na uhaini ndio msimamo wa sheria ya uhaini as we speak today.
Hajalijibia hili amekimbia kimbia tu sasa kwahiyo nimesema hakuna nia ya kufanya kosa na hakuna publication na maneno matupu hayavunji mfupa kwenye uhaini.
Kuna kitu hapa amekisema sana katuga, umma, umma, umma.
Hivi UMMA ni nini? Anaongea ongea tu umma. Umma ni watanzania milioni 63+ hayo majina yanapaswa kuwepo kwenye hati yaje kuwa pleaded nimezungumza na watu fulani usipowataja ni kosa, umekosea kuandaa hati ya mashitaka.
Haya hayahitaji ushahidi, hati ikiwa mbovu inafutwa kabla mshitakiwa hajajibu shitaka, inafutwa kabla ya ushahidi ieleweke hivyo.
Anaendelea Lissu.
Waheshimiwa Majaji kabla sijaondoka kwenye habari ya publishing kwasababu sheria inasema publishing by writing or printing sasa hiyo writing or printing ni lazima iwe pleaded.
Mtakaposoma Grey Likungu mtaona hao waliopanga kupindua serikali walikuwa wanaandikiana baru na kulikuwa na chapisho linaloitwa Ukweli na hayo yote yalikuwa set out kwenye hati ya mashitaka.
Waheshimiwa majaji mkiangalia kwenye kesi hiyo hiyo kwenye ukurasa wa mwisho kabisa, ameainisha hizo overt act zaidi ya 34 because the were pleaded ziliwekwa kwenye hati ya mashitaka.
Huwezi ukasema alichapisha halafu ukaishia hapo, unapaswa kusema alichapisha nini, wapi, akapeleka wapi? Hata walete mashahidi hayapo kwenye information.
Part 34 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako kwenye tweet hii.
@Roma_Mkatoliki CDM ni imani sio vyeti vya msajili, hakuna kukata tamaa hata iweje na sisi hatutashiriki uchaguzi utaona mwanawane. Watu watakuwa busy na mambo yao. Watakaoenda kuchagua watabebwa na mabasi na malori.