Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi, amesema kuwa maendeleo na ukuaji wa biashara ya kaboni nchini yanapaswa kwenda sambamba na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, akisisitiza kuwa sekta hiyo ni miongoni mwa nyenzo muhimu zitakazochochea ukuaji wa uchumi, uhifadhi wa mazingira na ustawi wa wananchi katika kipindi cha miongo ijayo.
Dkt. Muyungi alitoa kauli hiyo leo Juni 6, 2026 mkoani Kagera wakati alipokutana na wadau wa biashara ya kaboni katika kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera. Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi wa serikali, wataalamu wa mazingira, wadau wa sekta binafsi pamoja na wawakilishi wa taasisi zinazojihusisha na biashara ya kaboni.
Nikihitimisha ziara yangu ya Kitaifa katika Shirikisho la Urusi, leo pamoja na mambo mengine nimepata fursa ya kuhutubia Jukwaa la Biashara kati ya Tanzania na Urusi pamoja na Jukwaa la 29 la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg (SPIEF), ambayo yamekutanisha viongozi, wataalamu wafanyabiashara na wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali.
Nimewahakikishia wawekezaji kuwa Tanzania ni sehemu salama na bora kwa mitaji yao, tukijivunia mazingira wezeshi ya kisheria, amani na utulivu, miundombinu bora, ukuaji imara wa uchumi, uwepo wa nguvu kazi na fursa ya kufikia soko la zaidi ya watu milioni 500 ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika. Pia, nimebainisha sekta za kimkakati ambazo ni kipaumbele katika uwekezaji zikijumuisha madini, kilimo, nishati safi, mafuta na gesi, afya pamoja na usafiri na usafirishaji.
Habari njema zaidi ni kuwa, kuanzia Julai 2026, Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) itaanza safari za moja kwa moja kati ya Dar es Salaam, Zanzibar na Moscow. Hatua hii muhimu itaimarisha zaidi utalii, biashara na uwekezaji, na kufungua ukurasa mpya katika historia ya uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Urusi.
𝐌𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐙𝐈 𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐓𝐈𝐁𝐔 𝐖𝐀 𝐍𝐄𝐂, 𝐈𝐓𝐈𝐊𝐀𝐃𝐈, 𝐔𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐍𝐀 𝐌𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐎 𝐂𝐂𝐌, 𝐍𝐃𝐔𝐆𝐔 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐋𝐀𝐁𝐀𝐍 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈, 𝐎𝐅𝐈𝐒𝐈 𝐙𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐘𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈
Arusha Mjini, Arusha | 06 Juni 2026
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Ndugu Kenani Laban Kihongosi, amepokelewa na viongozi pamoja na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi katika Ofisi za CCM Wilaya ya Arusha Mjini leo tarehe 06 Juni, 2026, kuanza rasmi ziara yake ya kikazi wilayani humo.
Ziara hiyo inalenga kuimarisha uhai wa Chama, kusikiliza wananchi, kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM na kujionea maendeleo yanayopatikana kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
MTUMISHI WA WOTE
Tembelea: https://t.co/XFsl2Qg9M9
________
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#CCMIpoKazini
#KaziInaendelea
𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐘𝐀𝐀𝐌𝐁𝐈𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐂𝐇𝐀𝐆𝐔𝐀 𝐌𝐀𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐎 𝐁𝐀𝐃𝐀𝐋𝐀 𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐀𝐍𝐃𝐀𝐌𝐀𝐍𝐎
Arusha Mjini, Arusha | 06 Juni 2026
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Ndugu Kenani Laban Kihongosi, amewataka wananchi wa Arusha kuendelea kulinda amani, umoja na mshikamano wa Taifa kwa kutokubali kushawishiwa na siasa za chuki, migawanyiko na maandamano yasiyo na tija kwa maendeleo ya wananchi.
Akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi wa Shina la Wakereketwa Noah Saccos, Arusha Mjini, Ndugu Kihongosi amesema nguvu za vijana na wananchi zinapaswa kuelekezwa katika uzalishaji, ujasiriamali na kushiriki kikamilifu katika fursa zinazotokana na miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Amesisitiza kuwa Arusha ina kila sababu ya kujivunia mafanikio ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika sekta mbalimbali, huku akiwataka wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali na kushiriki katika kujenga uchumi imara kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
"Maendeleo yanajengwa kwa kazi, umoja na amani; si kwa migogoro na maandamano."
MTUMISHI WA WOTE
Tembelea: https://t.co/OpBqKYw71X
________________
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#MtumishiWaWote
#CCMIpoKazini
#ArushaMjini
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐋𝐄𝐀 𝐊𝐈𝐓𝐔𝐎 𝐂𝐇𝐀 𝐀𝐅𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐋𝐎𝐋𝐄𝐍𝐈, 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Ndugu Kenani Laban Kihongosi, ametembelea Kituo cha Afya Kaloleni jijini Arusha na kujionea huduma zinazotolewa pamoja na maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Watumishi wa afya katika kituo hicho wamemshukuru na kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwekeza katika sekta ya afya kupitia uboreshaji wa miundombinu, upatikanaji wa vifaa tiba vya kisasa na mazingira bora ya utoaji huduma kwa wananchi.
Akizungumza na watumishi hao, Ndugu Kihongosi amewapongeza kwa uzalendo, weledi na kujituma kwao katika kuwahudumia wananchi, akisisitiza kuwa huduma bora wanazozitoa ni ushahidi wa mafanikio ya Serikali na sababu kubwa inayozidi kujenga imani ya wananchi kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Amesema matokeo ya kazi nzuri katika vituo vya afya, hospitali, shule na maeneo mengine ya utoaji huduma za kijamii ndiyo kioo kinachoonesha utekelezaji wa Ilani ya CCM na dhamira ya Serikali ya kuboresha maisha ya Watanzania.
Katika kuonesha mshikamano na kuguswa na changamoto ya mgonjwa aliyekuwa akihitaji msaada wa matibabu, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa msaada wa fedha taslimu kiasi cha shilingi 500,000 kwa ajili ya kuchangia gharama za matibabu yake.
"Huduma bora kwa wananchi ndiyo sura halisi ya maendeleo na msingi wa imani ya wananchi kwa Serikali yao."
MTUMISHI WA WOTE
Tembelea: https://t.co/XFsl2Qg9M9
__________
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#CCMIpoKazini
#MtumishiWaWote
𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀 𝐍𝐈 𝐌𝐎𝐉𝐀, 𝐓𝐔𝐒𝐈𝐁𝐀𝐆𝐔𝐀𝐍𝐄 𝐊𝐖𝐀 𝐓𝐎𝐅𝐀𝐔𝐓𝐈 𝐙𝐀 𝐕𝐘𝐀𝐌𝐀: 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈
Arusha, Kaloleni | 06 Juni 2026
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Ndugu Kenani Laban Kihongosi,Leo Katika mwendelezo wa ziara yake mkoani Arusha, amepita katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Arusha Mjini, ikiwa ni pamoja na eneo la Kaloleni, Tawi la CHADEMA Kaloleni (mita 200), ambapo amezungumza na vijana aliyowakuta kwenye tawi hilo.
Ameendelea kusisitiza kuwa msingi wa maendeleo ya Taifa ni amani, umoja na kuheshimiana kwa Watanzania wote bila kujali itikadi zao za kisiasa.
"Tanzania ni moja, tusibaguane kwa tofauti za vyama."
MTUMISHI WA WOTE
Tembelea: https://t.co/XFsl2Qg9M9
_________
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#CCMIpoKazini
#MtumishiWaWote
#Arusha
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐒𝐈𝐌𝐀𝐌𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐒𝐀𝐅𝐀𝐑𝐀 𝐊𝐔𝐒𝐀𝐋𝐈𝐌𝐈𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐍𝐀 𝐊𝐈𝐉𝐈𝐖𝐄 𝐂𝐇𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐃𝐄𝐌𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈
Katika kuonesha mfano wa siasa za ustaarabu, umoja na mshikamano wa kitaifa, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Ndugu Kenani Laban Kihongosi, alisimamisha msafara wake na kusalimiana na wananchi pamoja na vijana waliokuwa katika kijiwe cha CHADEMA jijini Arusha tarehe 06 Juni, 2026.
Hatua hiyo imeendelea kuakisi falsafa ya CCM ya kuimarisha amani, kuheshimu tofauti za kiitikadi na kuendeleza mshikamano miongoni mwa Watanzania. Ujumbe mkubwa ukiwa ni kwamba tofauti za kisiasa hazipaswi kuwa sababu ya kugawanyika, bali ziwe chachu ya kujenga hoja na kushindana kwa sera kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
Tanzania yetu imejengwa juu ya misingi ya umoja, upendo na amani. Hivyo, jukumu la kila kiongozi na mwananchi ni kuilinda hazina hiyo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
“Umoja Wetu ndiyo Nguvu Yetu. Amani Yetu ndiyo Mtaji Wetu.”
MTUMISHI WA WOTE
Tembelea: https://t.co/XFsl2Qg9M9
_____________
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#CCMIpoKazini
#MtumishiWaWote
#SiasaZaUstaarabu
#UmojaNiNguvu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amehitimisha Ziara yake ya Kitaifa ya kihistoria nchini Urusi tarehe 05 Juni 2026 na kurejea nchini leo tarehe 6 Juni, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tarehe 06 Juni, 2026 baada ya kuhitimisha Ziara yake ya Kitaifa, St. Petersburg nchini Urusi tarehe 05 Juni, 2026 kufuatia mwaliko wa Rais wa Nchi hiyo Mhe. Vladmir Putin.
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐓𝐔𝐍𝐔𝐊𝐈𝐖𝐀 𝐒𝐇𝐀𝐇𝐀𝐃𝐀 𝐘𝐀 𝐇𝐄𝐒𝐇𝐈𝐌𝐀 𝐔𝐑𝐔𝐒𝐈
Moscow, Urusi | 04 Juni 2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu (Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi (RUDN), ikiwa ni kutambua mchango wake katika uongozi, maendeleo ya jamii na kuendeleza sekta ya elimu.
Akizungumza baada ya kupokea heshima hiyo, Rais Samia amesema tuzo hiyo si yake binafsi bali ni ya walimu, wanafunzi, wazazi na wote wanaoamini kuwa elimu ni msingi wa maendeleo ya watu na mataifa.
Rais Samia amesisitiza umuhimu wa elimu katika kuandaa jamii kukabiliana na mabadiliko ya dunia ya sasa, hususan katika maeneo ya sayansi, teknolojia na ubunifu, akieleza kuwa ushirikiano wa kimataifa ni muhimu ili mataifa yaendelee kunufaika na maendeleo hayo.
Hii ni miongoni mwa shahada za heshima ambazo Rais Samia ameendelea kutunukiwa kutoka vyuo vikuu mbalimbali duniani kutokana na mchango wake katika maendeleo, uongozi na ustawi wa jamii.
Tembelea: https://t.co/XFsl2Qg9M9
_______________
#KazinaUtuTunasongaMbele #SamiaSuluhuHassan
#CCMIpoKazini l
#ElimuKwanza
𝐌𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐎 𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐀 𝐖𝐀 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐑𝐀𝐓𝐔 - 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀
Karatu, Arusha | 04 Juni 2026
Wananchi wa Wilaya ya Karatu leo wamejitokeza kushiriki katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Ndugu Kenani Laban Kihongosi, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani Arusha.
Ziara hiyo inaendelea kuimarisha mawasiliano kati ya Chama na wananchi pamoja na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya CCM na maendeleo yanayotekelezwa katika maeneo mbalimbali.
Ziara inaendelea kesho Wilaya ya Arumeru.
MTUMISHI WA WOTE
Tembelea: https://t.co/XFsl2QgHBH
_________________
#KazinaUtuTunasongaMbele
#CCMIpoKazini
#KaziInaendelea
#Arusha
𝐁𝐈𝐋𝐀 𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐇𝐀𝐊𝐔𝐍𝐀 𝐌𝐀𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐎: 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈
Karatu, Arusha | 04 Juni 2026
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Ndugu Kenani Laban Kihongosi, amewahimiza wananchi wa Wilaya ya Karatu kuendelea kulinda amani na utulivu, akisisitiza kuwa maendeleo ya wananchi yanategemea mazingira salama na yenye utulivu.
Akizungumza katika Mkutano wa Hadhara, Kihongosi amesema bila utulivu hakuna biashara, hakuna kulima, hakuna utalii, hakuna kuendesha bodaboda wala bajaji, hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kushiriki katika kulinda amani ya Taifa.
Ziara inaendelea leo katika Wilaya ya Arumeru.
Tembelea: https://t.co/XFsl2Qg9M9
________
#KazinaUtuTunasongaMbele
#CCMIpoKazini
#AmaniKwanza
#KaziInaendelea
𝐌𝐒𝐈𝐈𝐍𝐆𝐈𝐄 𝐌𝐓𝐄𝐆𝐎 𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐁𝐄𝐁𝐀 𝐀𝐉𝐄𝐍𝐃𝐀 𝐙𝐀 𝐌𝐒𝐈𝐎𝐖𝐀𝐉𝐔𝐀, 𝐋𝐈𝐍𝐃𝐄𝐍𝐈 𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈: 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈
Karatu, Arusha | 04 Juni 2026
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Ndugu Kenani Laban Kihongosi, amewataka wananchi kuendelea kulinda amani, umoja na mshikamano wa Taifa kwa kutokukubali kubebwa na ajenda za watu wasio na nia njema na maendeleo ya nchi.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara Wilaya ya Karatu mkoani Arusha, Kihongosi amesema amani na utulivu ndiyo msingi wa maendeleo, hivyo kila mwananchi ana wajibu wa kushiriki katika kuilinda na kuitunza.
Amesisitiza kuwa wananchi waendelee kushiriki katika shughuli za uzalishaji na maendeleo huku wakiepuka vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama, umoja na ustawi wa Taifa.
Tembelea: https://t.co/XFsl2Qg9M9
________
#KazinaUtuTunasongaMbele
#CCMIpoKazini
#AmaniKwanza
#KaziInaendelea