Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu ametembelea na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi hiyo zilizopo Mji wa Serikali, Mtumba Mkoani Dodoma leo Mei 13,2026.
Aidha, Waziri Sangu aliambatana na Naibu Waziri Mhe. Dkt.Evaline Munisi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Dkt. Evaline Wilbard Munisi kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma, tarehe 06 Mei, 2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu wakipokea Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Machi 13, 2026 baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.
Aidha, ziara ya Mhe. Sangu katika mkoa huo inalenga kushirikiana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi ya Maendeleo ya Jamii kutembelea na kukagua Kiwanda cha Bidhaa cha Ngozi Kilimanjaro (KLICL) kilichopo Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huyo leo Machi 13, 2026 Mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Clement Sangu amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Saudi Arabia na Jordan, Suleimani Ali katika Hoteli ya Ritz Carlton, Jijini Riyadh, Saudi Arabia.
Kikao hicho kililenga kupitia na kujadili nyaraka muhimu za Mkutano wa Soko la Ajira Duniani (Global Labour Market Conference) utakaofanyika Saudi Arabia tarehe 26 hadi 27 Januari, 2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Clement Sangu akizungumza na Viongozi wa Watanzania wanaoishi nchini Saudi Arabia (Diaspora), katika hoteli ya Ritz Carlton, Jijini Riyadh, Saudi Arabia tarehe 25 Januari, 2026.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Rahma Kisua akizindua kitabu cha mwongozo wa uratibu mafunzo ya kuongeza Ujuzi kwa wafanyakazi tarehe 23 Januari 2023 katika ukumbi wa Royal Palm Mkoani Iringa.
Afisa Hifadhi ya Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano kupitia Idara ya Kinga ya Jamii Sohela Mabeyo akitoa elimu kuhusu sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa wanachuo wa Chuo cha Afya cha Kange jijini Tanga katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa.
Kikao hicho kililenga kujadili fursa mbalimbali za ajira zilizopo katika nchi za Falme za Kiarabu (UAE), kutathmini changamoto zinazojitokeza, pamoja na kuweka mikakati ya kuboresha upatikanaji na usimamizi wa fursa za ajira kwa Watanzania.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, amekutana na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Falme za Kiarabu (UAE), Mhe. Luteni Jenerali (Mst) Yacoub Mohamed, tarehe 3 Januari, 2026 jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Rahma Kisuo ameshuhudia Pambano la Ngumi liloandaliwa na Kampuni ya Mafia Boxing Promotion maarufu kama Knock out ya Mama 2025 lililofanyika Viwanja vya Posta Kijitonyama, jijini Dar es Salaam Disemba 31, 2025.