The Civic United Front was formed on 28 May 92 through a merger of two formerly existing movements - KAMAHURU, a pressure group for democratisation in Zanzibar.
Viongozi wanawake majasiri wa #CUF waliofuatana nami katika ziara yangu wakisalimiana na wanachama na wananchi wa Kitope ikiwa ni sehemu ya ziara yangu ya kikazi ya Wilaya ya Kaskazini 'B" leo. #ZiaraUnguja
Nikiwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu (Tanzania Bara) wa CUF, Mhe. Joran Lwehabura Bashange @joran_bashange kwenye Ukumbi wa Msekwa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa #Tanzania tayari kwa ajili ya kuwasilisha maoni na mapendekezo ya #CUF kuhusiana na #MuswadaWaVyamaVyaSiasa.
Jeshi la Polisi kituo cha polisi Madema mjini unguja wamempatia dhamana Katibu mtendaji wa Jumuiya ya Vijana wa CUF -JUVICUF Mhe.Mahmoud Ali Mahinda mchana huu. Uongozi wa chama ukiwakilishwa na Mkurugenzi wa Habari Mhe.Salim Bimany wamehakikisha kiongozi huyo anapata haki yake.
Polisi @tanpol imemkamata Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa #CUF ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama Mhe. Abdalla Khatau tokea Jumanne, tarehe 15 Januari, 2019 huko nyumbani kwake Masasi. Hadi sasa hawajasema sababu ya kumkamata wala kuruhusu kumuona.
Katibu mtendaji JUVICUF Mhe.Mahmoud Ali Mahinda amekamatwa na Polisi mchana wa leo 16.01.2019 nyumbani kwake Mkunazini mjini Unguja. Jeshi la Polisi kituo cha Polisi Madema wamekataa kumpatia dhamana kiongozi huyo na wamekataa kusema sababu ya kumkamata kwao.
Maalim @SeifSharifHamad awasili Pemba kwa ziara ya kikazi ya siku 4. Alipowasili kisiwani Pemba Maalim alipokewa na viongozi wa chama wa Wilaya nne za Pemba katika uwanja wa Ndege wa Chake Chake.
Katibu Mkuu wa CUF Maalim @SeifSharifHamad akutana na Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr @Vicent_mashinji na kufanya mazungumzo ya kina kuhusu muelekeo wa vyama na namna bora ya kutekeleza #AzimioLaZanzibar.
Naibu Katibu Mkuu wa #CUF - Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui @MazruiNassor ameanza ratiba ya ziara yake ya kufuatilia utendaji kisiwani Pemba kwa kukutana na viongozi wa Wilaya, Majimbo na Matawi yaliyomo katika wilaya ya Mkoani Pemba.
Naibu Katibu Mkuu wa #CUF -Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui @MazruiNassor jioni ya leo amekamilisha siku ya kwanza ya ziara yake ya kiutendaji katika Mkoa wa Kusini Pemba kwa kukutana na Viongozi wa Chama wa Wilaya, Majimbo na Matawi kutoka katika Wilaya ya Chake Chake.
2/3 - Kwa ruling hiyo, Mahkama imekataa ombi la Mawakili wa Serikali waliotaka wapewe siku 21 kuwasilisha utetezi wao wa maandishi. Kwa siku 7 walizopewa wametakiwa wawe wamewasilisha utetezi wao ifikapo tarehe 9 Januari ili Mahkama isikilize kesi tarehe 11 Januari, 2019.
1/3 - Mahkama Kuu ya Tanzania Masjala ya DSM katika Kesi Na. 31 ya 2018 - Zitto Kabwe, Salim Bimani & Joran Bashange v/s Mwanasheria Mkuu wa Serikali - imetoa ruling kwamba Mawakili upande wa Serikali wanapaswa kuwasilisha utetezi wao wa maandishi ndani ya siku 7 kuanzia leo.
3/3 - Mahkama imesema maombi ya kumzuia Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuuwasilisha mswada Bungeni kwa sasa hayahitajiki, kwa sababu kesi itasikilizwa tena tarehe 11 Januari, 2019 kabla ya Mswada kuwasilishwa kwa kusomwa kwa mara ya pili tarehe 15 Januari, 2019.
Mahakama imewaomba waleta maombi @zittokabwe, @salimbimani2 Bwana Bashange wawe na subira juu ya ombi lao la zuio kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kusitisha kuupeleka Muswada husika Bungeni, kwa sababu kesi itasikilizwa kabla ya tarehe 15 Januari 2019.