Leo tunashukuru: robo karne; miaka ishirini na tano ya upendo wa agano, ushirikiano, na uangalizi wa Mungu. Kwa mioyo yenye shukrani tunasherehekea Silver Jubilee yetu, tukisema pamoja na Samweli: ‘Hata sasa Bwana ametusaidia.’ (1 Sam. 7:12). Tunamwamini Mungu kwa kila kesho.
Sabato Njema
https://t.co/k3JNV17evT
Sabato inaanza vyema kwa sauti ya wimbo huu mtakatifu…
“Njoo Kwenye Kanisa Jirani’ – ni mwaliko wa upendo kutoka kwa Yesu mwenyewe. Tazama sasa, ruhusu roho yako iguswe.”
Usisahau:
🔴 SUBSCRIBE
🔴 SHARE
🔴 LIKE
🔴 COMMENT
@ChriStanzas
Moja ya maana ya kina ya kutimizwa kwa mapenzi ya Mungu ni kupokea kitu tofauti na kile tulichoomba — hata kama tumeomba kwa imani. Tunaruhusu mapenzi Yake yashinde matakwa yetu, tukiamini kwamba Yeye anajua kilicho bora kwetu kuliko sisi wenyewe.
— Chris Ungani,
Nyayo za Imani
Sabato Njema!
“Wapo wanaosema Mungu hajawaacha kwa kutaja mafanikio yao makubwa. Lakini wapo wanaosema Mungu hajawaacha kwa kuonyesha makovu ya majeraha makubwa miilini mwao; Makovu ni ushuhuda kwamba waliumia sana, lakini hawakufa.”
— Chris Ungani, Nyayo za Imani, May 9, 2025
Sabato Njema!
“Walipomwagwa kama manemane madhabahuni, ardhi ikanywa damu ya wenyehaki, ikanyunyiziwa machozi ya wateule. Katika kimya cha mateso, mbegu ya haki ilizikwa, na kutoka mavumbini, mti wa matumaini ukaanza kuchipua, ili uzae matunda kwa watakaoirithi nchi ya ahadi.”
Sabato Njema!
Si kwamba Mungu hayuko karibu nasi tunapolia, bali mara nyingi makelele ya maumivu yetu huwa makubwa kiasi cha kuzuia kumsikia anapotunong’oneza kwa sauti ya utulivu."
— Christopher Ungani, Nyayo za Imani, Aprili 18, 2025
“Mhubiri akimbiliaye kila madhabahu punde aonapo kusanyiko, hajaitambua sauti ya Mwitaji. Maana hukuagizwa kwa kila kusanyiko, wala si kila sikio limekusudiwa kusikia kutoka kwako. Ngoja majira yako, usije ukasema mahali ambapo Mungu hakukutuma.”
Nyayo za Imani, April 20, 2025
@Nakkumary2oo25 Happy Saturday!
"It’s not that God is not near us when we cry, but often the noise of our pain is so loud that it drowns out His gentle whisper."
— Christopher Ungani, Nyayo za Imani, April 18, 2025
Sabato Njema!
"Si kwamba Mungu hayuko karibu nasi tunapolia, bali mara nyingi makelele ya maumivu yetu huwa makubwa kiasi cha kuzuia kumsikia anapotunong’oneza kwa sauti ya utulivu."
— Christopher Ungani, Nyayo za Imani, Aprili 18, 2025