@SuluhuSamia Mhe Rais naendelea kushauri kwa dhati Tundu Lissu aachiwe huru kwani kesi haikamiliki. Hekima na busara iliyokufanya kutangaza sera ya 4Rs mara ulipoingia madarakani ikuongoze tena katika jambo hili. Simulizi hizi za kutisha za vyombo vya habari vya kimataifa, zinaibua hisia kali hasa kwa vijana, hata wazee tumekumbushwa kadhia ya operation Sogeza iliyounda vijiji vya ujamaa 1974 -1976. Taarifa hizi zinaathiri kikubwa taswira ya taifa letu na maslahi yake. Athari ni kubwa. Tutafute muafaka kupitia uwajibikaji na maridhiano. Tuwe na hofu ya Mungu na kutambua miujiza yake mfano wa risasi 16 kushindwa kukomesha uhai ingawa maumivu ni makubwa. Tutubu na kusali kuliombea taifa letu kila mtu kwa imani yake.
HERI YA SIKU YA KUZALIWA, MHE. @HecheJohn ✌️
Leo tunaungana na maelfu ya Watanzania kumtakia Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Mhe. John Heche, heri na baraka tele katika kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa.
Katika siku hii ya kipekee, zawadi yenye thamani zaidi tunayoweza kumpatia si maneno pekee, bali ni kuendelea kuunga mkono wito wake wa kujenga chama imara kwa kuchangia kufanikisha Baraza Kuu la Umma.
Mhe. John Heche amekuwa mstari wa mbele akihamasisha Watanzania kushiriki katika ujenzi wa chama. Hivyo, tunawaalika wanachama, wapenzi na marafiki wa CHADEMA kuadhimisha siku hii kwa kutuma mchango wao kwa ajili ya Marathon ya kufikia TSh. Milioni 334.
Zawadi bora kwa Mhe. John Heche ni kuona Watanzania wakijitokeza kwa wingi kuchangia Baraza Kuu la Umma. Kila mchango, mkubwa au mdogo, ni sehemu ya mafanikio ya chama chetu.
Heri ya kuzaliwa Mhe. John Heche! Mwenyezi Mungu akupe afya njema, hekima, nguvu na ulinzi unapoendelea kulitumikia Taifa na CHADEMA.
Mkristo Vs Nikki Mbishi.
Freestyle battle hizi tulikuwa tunazisikiliza zamani kwenye radio ,sasa hivi kila Alhamisi ni live pale Micasa Tabata kuanzia saa moja usiku,hakuna kiingilio.